Na hili la asilimia 33% mafao uzeeni badala ya asilimia 25% (kwa iliyokuwa PPF na NSSF) na badala ya asilimia 50% (kwa iliyokuwa PSPF na LAPF)

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
Hapa imetumika chenga ya mwili!! Kwenye taarifa moja kutolewa habari ya ongezeko la mishahara kwa asilimia 23.3 kwa kima cha chini na habari ya kupandisha mafao ya uzeeni huko PSSSF toka asilimia 25% iliyokuwa imekataliwa na waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF (waliokuwa wakipata asilimia 50%) na kuwa asilimia 33%.

Naomba ieleweke kuwa, kwa waliokuwa wanachama wa LAPF na PSPF hiki kiwango cha pensheni KIMESHUKA toka asilimia 50% kwa malipo ya mkupuo na kuwa asilimia 33%. Kiwango kimeshuka kwa asilimia 17%. Lakini kwa watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF (ambao kwa sasa wote wapo PSSSF) wao mafao ya uzeeni ya mkupuo yamepanda toka asilimia 25% hadi asilimia 33% (yamepanda kwa asilimia 8%).

Naomba ifahamike kuwa mpaka sasa watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF (ambao kwa sasa wote wako PSSSF) wanapostaafu hulipwa kwa asilimia 25% kwa malip[o ya mkupuo, wakati watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF (ambao kwa sasa wote wako PSSSF) wanapostaafu hulipwa kwa asilimia 50% kwa malipo ya mkupuo.

Kwa maneno mengine, mabadiliko haya yana faida kwa watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF maana yanawapandisha "kidogo" toka 25% hadi 33%. Lakini mabadiliko haya yana hasara kwa waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF maana yanawashusha "siyo kidogo" toka 50% hadi 33%.

Nimesema ni chenga ya mwili kwa sababu watu walijadili na kusemea sana na kusifia sana kuhusu nyongeza ya mshahara hata kusahau hili la mafao ya uzeeni na kupita bila mjadala ulioshiba kwenye mitandao ya kijamii!!

Kwa upande wangu nianze na shukrani kwa Serikali yetu kwa kuondoa hii DOUBLE STANDARD iliyokuwepo kweye mafao ya uzeeni ya watumishi wa umma. Mtumishi wa umma aliyekuwa PPF au NSSF yeye aliendelea kupata mafao KIDUCHU ya asilimia 25% kwenye malipo ya mkupuo wakati watumishi wenzake wa umma waliokuwa PSPF na LAPF wakiwa wanapewa asilimia 50%. Hii tofauti ni kubwa mno! Lakini serikali ilifumbia macho jambo hili ambalo liliendeleza kuwaumiza watumishi hawa wa umma, utadhani wanatumikia serikali mbili tofauti au utadhani ni watoto wa baba tofauti!! Kwa hiyo kwa kusawazisha malipo kwa wote hilo napongeza.

Vitu vingine ambavyo huwa vinaathiri kiasi cha mapato havijaainishwa kwenye taarifa hiyo. Vitu hivyo ni:
1. Pension factor. Hii ni namba ambayo huwa inagawiwa kwenye kikokotoo cha mafao (ni denominator). Kwa kadri namba hii inavyokuwa kubwa ndivyo mafao yanavyozidi kupungua. Kwa kadri numba hii inavyokuwa ndogo ndivyo mafao yanavyozidi kuwa makubwa. Pension factor iliyokuwa inatumika PSPF na LAPF ni 580. Je hii pension factor imebaki kuwa 580 au imeongezeka au imepungua. Kama imeongezeka italamba itapunguza kiasi cha mafao! Ni vizuri wahusika wakaliweka wazi hili vinginevyo ni sawa na kuonezewa na kupunguziwa wakati huo huo na mabadiliko kutokuonekana.

2. Mshahara unaotumika kwenye kukokotoa mafao. Kwa PSPF na LAPF mshahara wa mwisho ndio ulikuwa unatumika kwenye kukokotoa mafao. Hii ina faida kwa mstaafu maana mara nyingi mshahara wa mwisho huwa ni mkubwa zaidi, hasa kama mhusika atapandishwa cheo karibu na kustaafu au serikali kuongeza mshahara. Kwa PPF na NSSF wao walikuwa wanatumia WASTANI wa mishahara "mizuri" ya miaka 3 kati ya miaka 10 ya mwisho. Hii ni mbaya sana, maana hata kama mtu atapandishiwa mshahara mwishoni, huu mshahara hautatumika kwenye kikokotoo!

Wakitafuta wastani wa mishahara wa miaka mitatu, ile miaka aliyokuwa na mshahara mdogo itameza ile aliyoongezewa kwenye kutafuta wastani. Sasa hili pia serikali lazima iliweke wazi, vinginevyo furaha ya kupandisha toka 25% hadi 33% ikawa ni furaha hewa. Lakini pia kilio cha kushuka toka 50% hadi 33% kinaweza kuwa ni kikubwa zaidi! (maana hapa kuna wanaolia waliokuwa PSPFna LAPF pia kuna wanaocheka kidogo waliokuwa PPF na NSSF).

Samahani nimelazimika kutoa andiko refu kama jitihada za kueleweka zaidi. Karibuni kwa mjadala.
 
Kiwango cha mkupuo kikiwa juu kiwango cha monthly pension cha kulipwa huwa chini.Vizuri kubakiza nyingi ili kupata monthly Pension kubwa.

Anyway ile percent 50 percent ilikuwa nzuri kuchukua mkupuo lakini monthly Pension ilikuwa ndogo mno .

Anyway mtu chake Serikali inajaribu kuongeza monthly Pension kwa kushusha mkupuo kuwa mkubwa sababu mbeleni huko kilio kikubwa ohhh monthly Pension ndogo!!! Wakati unachukua 50 percent ulikenua meno ukidhani uko vizuri wakati umeishusha monthly Pension utakayopokea miaka mingi hadi kifo
 
Mtoto akililia wembe mpe
Pension ukichukua ya mkupuo kubwa monthly Pension huwa ndogo

Serikali imesikia kelele za wafanyakazi wakilia mkupuo za mkupuo ziwe nyingi imewapa wembe wao wanaolilia ila wajiandae monthly Pension kuwa ndogo

Kwa Serikali imekaa vizuri unalipa kikubwa sasa mbeleni huko unalipa kiduchu monthly Pension maisha yanaendelea .
 
Unajua utaishi kwa muda gani?
 
Maoni yangu ni kwamba ili kuweka uwiano ya malipo ya kustaafu,kikokotoo kitumike kulingana na vyeo vya watumishi na siyo MISHAHARA ya uteuzi.

Viongozi wote wa umma huteuliwa wakiwa ngazi ya TGS g na h ngazi zinazoendelea hutokana na uteuzi.Pension inayotokana na kazi za uteuzi ni mzigo mkubwa kwa walipakodi wakati utumishi wao hautokani na utalaamu na ujuzi.

Kuhusu kutofautiana kwa asilimia ya vikokotoo vya watumishi wa serkali na mashirika, asilimia ya kikokotoo kwa watumishi wa Serkali ilikuwa juu kulinganisha na mashirika ya umma kwa sababu MISHAHARA ya wtm wa umma ilikuwa mikubwa kuliko ya watumishi wa serkali katika ngazi sawa. Hivyo sioni kama kulikuwa na upendeleo.Haya ni maoni yangu tu
 
Mtoto akililia wembe mpe
Pension ukichukua ya mkupuo kubwa monthly Pension huwa ndogo

Serikali imesikia kelele za wafanyakazi wakilia mkupuo za mkupuo ziwe nyingi imewapa wembe wao wanaolilia ila wajiandae monthly Pension kuwa ndogo

Kwa Serikali imekaa vizuri unalipa kikubwa sasa mbeleni huko unalipa kiduchu monthly Pension maisha yanaendelea .
Unaposema kiwango cha mkupuo kikiwa kikubwa monthly pension inakuwa ndogo unamaanisha nini, watumishi wa serikali walikuwa wanapata mkupuo 50% na monthly pay ilikuwa karibu robo ya basic salary yao ya mwisho, hao wa private sector walikuwa wanapata mkupuo 25%, monthly pension yao ilikuwa ngapi?
 
Ni almost 72% ya basic salary.
 
Unaposema kiwango cha mkupuo kikiwa kikubwa monthly pension inakuwa ndogo unamaanisha nini, watumishi wa serikali walikuwa wanapata mkupuo 50% na monthly pay ilikuwa karibu robo ya basic salary yao ya mwisho, hao wa private sector walikuwa wanapata mkupuo 25%, monthly pension yao ilikuwa ngapi?
Monthly Pension ilikuwa 72%
 
Mibunge ya CCM iliyotunisha matumbo kama vyura kule bungeni na mimacho yao mkiubwa kama ya bundi ndiyo iliyosababisha U.SENGE huu usiovumilika kwa watumishi wa umma.
 
Hapa imetumika chenga ya mwili!! Kwenye taarifa moja kutolewa habari ya ongezeko la mishahara kwa asilimia 23.3 kwa kima cha chini na habari ya kupandisha mafao ya uzeeni huko PSSSF toka asilimia 25% iliyokuwa imekataliwa na waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF (waliokuwa wakipata asilimia 50%) na kuwa asilimia 33%.

Naomba ieleweke kuwa, kwa waliokuwa wanachama wa LAPF na PSPF hiki kiwango cha pensheni KIMESHUKA toka asilimia 50% kwa malipo ya mkupuo na kuwa asilimia 33%. Kiwango kimeshuka kwa asilimia 17%. Lakini kwa watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF (ambao kwa sasa wote wapo PSSSF) wao mafao ya uzeeni ya mkupuo yamepanda toka asilimia 25% hadi asilimia 33% (yamepanda kwa asilimia 8%).

Naomba ifahamike kuwa mpaka sasa watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF (ambao kwa sasa wote wako PSSSF) wanapostaafu hulipwa kwa asilimia 25% kwa malip[o ya mkupuo, wakati watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF (ambao kwa sasa wote wako PSSSF) wanapostaafu hulipwa kwa asilimia 50% kwa malipo ya mkupuo.

Kwa maneno mengine, mabadiliko haya yana faida kwa watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF maana yanawapandisha "kidogo" toka 25% hadi 33%. Lakini mabadiliko haya yana hasara kwa waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF maana yanawashusha "siyo kidogo" toka 50% hadi 33%.

Nimesema ni chenga ya mwili kwa sababu watu walijadili na kusemea sana na kusifia sana kuhusu nyongeza ya mshahara hata kusahau hili la mafao ya uzeeni na kupita bila mjadala ulioshiba kwenye mitandao ya kijamii!!

Kwa upande wangu nianze na shukrani kwa Serikali yetu kwa kuondoa hii DOUBLE STANDARD iliyokuwepo kweye mafao ya uzeeni ya watumishi wa umma. Mtumishi wa umma aliyekuwa PPF au NSSF yeye aliendelea kupata mafao KIDUCHU ya asilimia 25% kwenye malipo ya mkupuo wakati watumishi wenzake wa umma waliokuwa PSPF na LAPF wakiwa wanapewa asilimia 50%. Hii tofauti ni kubwa mno! Lakini serikali ilifumbia macho jambo hili ambalo liliendeleza kuwaumiza watumishi hawa wa umma, utadhani wanatumikia serikali mbili tofauti au utadhani ni watoto wa baba tofauti!! Kwa hiyo kwa kusawazisha malipo kwa wote hilo napongeza.

Vitu vingine ambavyo huwa vinaathiri kiasi cha mapato havijaainishwa kwenye taarifa hiyo. Vitu hivyo ni:
1. Pension factor. Hii ni namba ambayo huwa inagawiwa kwenye kikokotoo cha mafao (ni denominator). Kwa kadri namba hii inavyokuwa kubwa ndivyo mafao yanavyozidi kupungua. Kwa kadri numba hii inavyokuwa ndogo ndivyo mafao yanavyozidi kuwa makubwa. Pension factor iliyokuwa inatumika PSPF na LAPF ni 580. Je hii pension factor imebaki kuwa 580 au imeongezeka au imepungua. Kama imeongezeka italamba itapunguza kiasi cha mafao! Ni vizuri wahusika wakaliweka wazi hili vinginevyo ni sawa na kuonezewa na kupunguziwa wakati huo huo na mabadiliko kutokuonekana.

2. Mshahara unaotumika kwenye kukokotoa mafao. Kwa PSPF na LAPF mshahara wa mwisho ndio ulikuwa unatumika kwenye kukokotoa mafao. Hii ina faida kwa mstaafu maana mara nyingi mshahara wa mwisho huwa ni mkubwa zaidi, hasa kama mhusika atapandishwa cheo karibu na kustaafu au serikali kuongeza mshahara. Kwa PPF na NSSF wao walikuwa wanatumia WASTANI wa mishahara "mizuri" ya miaka 3 kati ya miaka 10 ya mwisho. Hii ni mbaya sana, maana hata kama mtu atapandishiwa mshahara mwishoni, huu mshahara hautatumika kwenye kikokotoo!

Wakitafuta wastani wa mishahara wa miaka mitatu, ile miaka aliyokuwa na mshahara mdogo itameza ile aliyoongezewa kwenye kutafuta wastani. Sasa hili pia serikali lazima iliweke wazi, vinginevyo furaha ya kupandisha toka 25% hadi 33% ikawa ni furaha hewa. Lakini pia kilio cha kushuka toka 50% hadi 33% kinaweza kuwa ni kikubwa zaidi! (maana hapa kuna wanaolia waliokuwa PSPFna LAPF pia kuna wanaocheka kidogo waliokuwa PPF na NSSF).

Samahani nimelazimika kutoa andiko refu kama jitihada za kueleweka zaidi. Karibuni kwa mjadala.
Hapo umetoa ufafanuzi mzuri sana, maana kinachotajwa ni kupanda kutoka 25% kwenda 33% tu, lakini hawataji kushuka kutoka 1/540 kwenda 1/580 na kushuka kutoka miaka 15.5 kwenda miaka 12.5 ambavyo vinapunguza sana mkupuo.
 
Kiwango cha mkupuo kikiwa juu kiwango cha monthly pension cha kulipwa huwa chini.Vizuri kubakiza nyingi ili kupata monthly Pension kubwa.

Anyway ile percent 50 percent ilikuwa nzuri kuchukua mkupuo lakini monthly Pension ilikuwa ndogo mno .

Anyway mtu chake Serikali inajaribu kuongeza monthly Pension kwa kushusha mkupuo kuwa mkubwa sababu mbeleni huko kilio kikubwa ohhh monthly Pension ndogo!!! Wakati unachukua 50 percent ulikenua meno ukidhani uko vizuri wakati umeishusha monthly Pension utakayopokea miaka mingi hadi kifo
BORA MKUPUO UKAWA MKUBWA ILI UWEZE HATA KINUNUA NYUMBA KWA WALE AMBAO HAWAKUWAHI KUJENGA WAKIWA KAZINI kuliko Pensheni ya kila mwezi ikawa kubwa kwani hata KODI ya Nyumba haitamudu
 
Back
Top Bottom