Mzungu angeongoza Tanzania!

Upinzani unapokuwa ni wa kutetea wauza madawa ya kulevya ni bora kuminywa tu.
Demokrasia ni nzuri kama kuna wapinzani wa kweli na principled. Sio hawa wanaounganishwa na CCM kwenye MADAWA YA KULEVYA.
Udikteta unaweza kufaa sana unapokuwa na wapinzani wa hovyo kama hawa ambao badala ya kuunga mkono juhudi zilizoanzishwa na kushauri njia mbadala itakayofaa ili kurekebisha makosa ya Makonda, wao wanaungana na miCCM kudai Makonda asulubiwe kwa kujaribu kupambana na wauza madawa ya kulevya.
Tuna MAPINZANI ya HOVYO sana Tanzania kwa hivi sasa. Mapinzani ambayo ukisema Lowasa ni FISADI eti leo ndo yamejua kuwa kabla hujatuhumu unatakiwa uwe na USHAHIDI. Mapinzani ambayo yapo tayari kuungana na MiCCM kupinga juhudi za kupambana na madawa ya kulevya yanhitaji kudhibitiwa kwa nguvu zote. Yakiachiwa Taifa litaangamia.
 
Kama mtoto wa Kikwete anauza unga mbona hamjamwita polisi ? Mabavu ya Magufuli yakowapi kama unasema mtoto wa Kikwete anauza unga na hakatwi?
 
Ki ukweli wazo lako ni sawa na mfu.Luna madhara makubwa sana akili ndogo kuongoza akili kubwa na kuruhusu watu wakuwazie wakufikilie nalo ni janga
 
Hili suala mi naona ni mpana sana ila huwa halijadiliwi kwa kina,si wenye kuona kuwa afrika haina maendeleo kwa sababu hakuna demokrasia wala wenye kuona demokrasia ndiyo inatucheleweshea maendeleo afrika wote hawaelezi kwa kina hoja zao.
Mkuu enzi za kudai uhuru ni kweli demokrasia ingerudisha maendeleo.kikubwa ni kuwa jamii ilikuwa haina uelewa mkubwa,elimu ndogo na ingeweza kudanganywa kiurahisi.Mfano Kadi ya ukabila ilikuwa na nguvu sana kwa waovu kujifichia humo.
Kwa mazingira ya sasa demokrasia ni muhimu sana.wananchi wengi wana uelewo.wanaweza kuchanganua data vizuri tuu na kufikia hitimisho.Kutopatikana kwa data ni tatizo,inaturudisha Kwenye enzi za kudai uhuru wakati mazingira yamebadilika.
Wajanja ,Wezi ni wengi Kwa sasa.Angalia m ikataba ya uficho inavyotuliza.Uwazi katika shuguli za Bunge ina faida nyingi sana kuliko hasara.
 
Sawa Mkuu lakini bado nadhani demokrasia ingetusaidia kuwajua vizuri hao wabunge.tungejua nani wa kwetu na nani si wakwetu.
 
Mnahitaji wewe na nani? Unatueleza au unamshutumu rais kuendesha nchi kibabe?
 
Unazungumzia hizi vita za kupeleka watu mahakamani kwa ushahidi wa msokoto mmoja wa bhangi wakati matangazo yaliunguruma huku na kule hadi watu wakaaminishwa kwamba "...kumbe yule nae ni drug dealer!"

Source: Mwananchi.

Na according na Wakili anayemtetea Wema, mzigo uliokutwa kwa mteja wake ni 1.83gm!!!


That's one but second, na wewe ingawaje unawaita hao wengine ni mi-CCM lakini bado fikra zako ni kama za hao maCCM! Hao unaowaita miCCM kutokana na uCCM wao wanashindwa kuona hoja ya watu! Hakuna anayepinga vita dhidi ya dawa za kulevya bali watu wanapinga approach inayotumika! Lakini miCCM na wewe mnataka kuaminisha watu kwamba kuna watu wanapinga vita dhidi ya dawa za kulevya wakati kinachopingwa ni approach!!

Na matokeo yake ndo haya!! Unapewa live tv coverage huku ukijigamba kwamba "ukiona mtu anaitwa basi fahamuni huyo mtu tumemfanyia uchunguzi wa kutosha lakini unaishia kuwa na ushahidi wa 1.83 g of bhang wakati tayari umeshaitengazia dunia kwamba "huyo ni drug dealer!"

Huwezi kujua maana ya wanachokipigania watu hadi siku uwe na status fulani kwa jamii!!!!!

Si kwamba status ya mtu inampa exlussive right lakini hata sheria inasema hivyo in other way round!!! Kama tuhuma ile ile nimepewa mimi kwa upande mmoja na mtu kama Reginald Mengi kwa upande mwingine; endapo tunashitaki, rule out ya mahakama inaweza kuwa tofauti!

Si kwamba nitakuwa nimebaguliwa kwavile mimi ni maskini na Mengi ni tajiri, la hasha! Ninapofanyiwa defamation mimi; defamation hiyo itakuwa tu ni dhidi yangu towards small population, defamation kwa familia yangu na watu wengine wachache sana!

Kinyume chake, defamation kwa Mengi ni defamation against Mengi personally towards big population, defamation kwa familia yake, biashara zake, partners wake...!!

Kwahiyo unless kama una ushahidi usio na shaka yoyote kwamba mtuhumiwa huyu ana kesi kubwa ya kujibu lakini kama unaenda kumtangaza hadharani kwamba anahusika na dawa za kulevya halafu unakosa au hauna ushahidi; no please, bora tuitwe tunatetea wauza unga kuliko kutetea ujinga kama huo!!!

I know, wapo wenye akili zao timamu ambao wanaona kabisa this's not right lakini kwavile wanaogopa kuambiwa wanatetea wauza unga, wameamjua kunyamaza!!!!

Kwahiyo, acheni kupotosha ili kutetea mambo yasiyo na msingi!! Hata ukimuuliza teja kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya; atakuunga mkono tu! Lakini watu wanachopinga ni approach! Approach ambayo, si tu kwamba inaweza kuchafua image ya watu wakati ushahidi hakuna lakini pia ni poor approach inayoweza kuwafanya wapoteze ushahidi!!!

Kwa mfano, wamemtaja mmiliki wa Slipway! Kama kweli wapo serious na wanaamini ni muingizaji mkubwa wa dawa za kulevya! Kwanini hawakuomba search warrant kimya kimya kisha wakamuibukia na kuanza kumpekua badala ya kwenda kwenye TV na kupiga yowe?! Hivi hata kama kweli ni muingizaji mkubwa wa dawa za kulevya; leo hii wakienda pale Slipway wanaweza kukuta japo kijiko kimoja cha heroin au cocaine?!

Hayo hamuyaoni kwavile mmezoea political drama!!!!
 
Siasa hujui ila wewe ni mtalaamu wa majungu. Sijawahi kuona post yako yenye akili timamu
 
Kwanini mnaamini ni ccm tu ndiyo wanatumia ujinga wa wananchi?

Sasa kama ccm inanunulia watu wali, sukari, kugawa tshirt na kofia inapewa kura bila kupeleka huduma muhimu unategemea nini. Angalia sehemu zenye watu wenye uelewa mpana jinsi ccm inavyoshindwa na hata ikishinda unakuta ni kwa kutumia nguvu ya dola.
 
Hivi wazungu walikubaka au!
cc barbarosa
 
Ndiyo maana nikasema hili jambo ni pana ila wengi hamlielezi kwa kina,wengi mnaishia kulalamika tu.
 

1. Hivi sheria inataka mtuhumiwa akamatwe na gram au tani ngapi ndo ifae kuwa ushahidi mahakamani?
2. Hivi hizo approach sahihi za kudeal na wauza madawa ya kulevya ndo mmezijua leo au zilikuwepo siku zote? kama zilikuwepo ni kwa nini hazijafanikiwa na vijana wetu bado wanaendelea kuangamia?
3. Wapinzani wanapaswa kutoa constructive criticism - walipaswa japo kuitambua na kuiheshimu DHAMIRA ya Makonda kwanza, halafu ndipo washauri the right approach. Mwanzoni wakasema ametaja vidagaa eti Chid Benz na RayC, alipoongeza list wakahama eti kalidharau bunge. Hivi wewe unayedai una akili hata kutapatapa huku kumekushinda kukuona?
3.Inawezekana kabisa kuwa Makonda kakosea approach. Lakini kama sote tunaguswa inatupasa kumsaidia na sio kumkejeli na kumtishia.
 
Sasa kama ccm inanunulia watu wali, sukari, kugawa tshirt na kofia inapewa kura bila kupeleka huduma muhimu unategemea nini. Angalia sehemu zenye watu wenye uelewa mpana jinsi ccm inavyoshindwa na hata ikishinda unakuta ni kwa kutumia nguvu ya dola.
Huo uelewa mpana wa unaupima kwa vipimo vipi?

Ujinga wa wananchi unatumiwa na pande zote mbili za upinzani na ccm.
 
Huo uelewa mpana wa unaupima kwa vipimo vipi?

Ujinga wa wananchi unatumiwa na pande zote mbili za upinzani na ccm.

Wajinga hawawachagui wapinzani wameambiwa wataleta vita kama ya Rwanda. Pia ni vizuri wajinga waendelee kuwepo kwa ajili ya amani kwani ni mtaji wa chama king'ang'anizi kisichotaka kutoka nadarakani kwa kura. Rejea uchaguzi ZnZ, hiyo ni kwa uchache wa mifano halisi.
 

Hapa kuna hoja mbili ambazo haziingiliani kabisa. Wewe unajaribu kupotosha kwa kuwa hoja zote mbili zinamhusu mtu mmoja. Hakuna Mbunge yeyote aliyesimama kutetea madawa ya kulevya. Hoja za wabunge hapa ni kudharauliwa kwa mhimili huo muhimu wa Taifa hili hivyo wabunge wanataka aliyedharau afike kuhojiwa na akipatikana na kosa aadhibiwe kwa mujibu wa kanuni na sheria.

Hoja ya pili ni approach iliyotumika kuanzisha vita hii ya madawa ya kulevya. Kwa uelewa wangu, uchunguzi wowote hufanyika kwa siri ili mtuhumiwa asipate nafasi ya kupoteza ushahidi. Unapomtuhumu mtu na kumpa muda wa kufika kuhojiwa maana yake unamfanya kujiandaa kupoteza ushahidi kama kweli ni mhusika. Kwa hiyo basi kinachopingwa ni approach iliyotumika ambayo ukiiangalia kwa jicho makini la mbali inaweza kutafsiriwa kuwa muanzishaji ni mtuhumiwa mkuu kwa kuwa anajitahidi kusaidia ushahidi kupotezwa. Kwa kuwa kuna vyombo vingine vilikuwa vinaendesha vita hii kwa approach ya usiri inaweza kuwa baada ya kugundua ushahidi unakaribiwa basi ili kuuvuruga ikaanzishwa hii kwa nia ya kuvuruga wa awali. Kwa kuwa vyombo hivi rasmi vinajulikana ilikuwa ni vema kushirikiana navyo badala ya kilichofanyika. Tufikiri zaidi na zaidi, Miluzi Mingi Humpoteza Mbwa!!!
 
Wajinga hawawachagui wapinzani wameambiwa wataleta vita kama ya Rwanda. Pia ni vizuri wajinga waendelee kuwepo kwa ajili ya amani kwani mtaji wa chama king'ang'anizi kisichotaka kutoka nadarakani kwa kura. Rejea uchaguzi ZnZ.
Ina maana kuchagua upinzani ndiyo kipimo cha uelewa upinzani na ujinga ni kinyume chake?

Hao ccm wana wajinga wao wanaowapelekesha watakavyo na upinzani nao wanawapelekesha wajinga wao watakavyo.
 
Kuna uzi hapa nimeuweka kwamba sitashangaa wapo watakaohoji "kwani 1.83g sio dawa za kulevya!" Sioni sababu ya kurudia tena hapa!

That's one but two, hakuna anayemkejeli Makonda bali inayokejeliwa ni approach yake! Na si kwamba hafahamu kwamba approach yake ni mbovu, anajua na kama alikuwa hajui sina shaka watu walio chini yake walimwambia this's wrong approach! Siamini mtu kama Simon Sirro anaamini kutoa tip hadharani kwamba XYZ ni drug dealers kabla hujaenda kumpekua na kupata ushahidi wa kuanzia hiyo ndiyo best approach!!!

Lakini kama Makonda aliingia kwenye game na ile tabia yake ya kuanza kuonesha watu hawajui kazi ; inawezekana kabisa kabisa akina Sirro walikata shauri la kumuitikilia kila analosema...!! Huyo Sirro mwenyewe keshawahi kutuhumiwa na Makonda kwamba inawezekana amechukua 50 million za shisha... sasa ya nini mtu ati mdomo wake halafu aambiwe anajengwa ghorofa na wauza dawa za kulevya!!!!

By the way, ikiwa ameshindwa kumsilikiza Waziri wa serikali anayeitumikia, ndo atakuja kusikiliza ya Wapinzani?! Nini alichoambulia Nape baada ya kusema this's wrong zaidi ya kashifa toka kwa wafuasi uchwara kwamba Nape anatetea wauza dawa za kulevya?! Ndo maana hata mawaziri wanaohusika na hili jambo wameamua kupiga kimya!!!!
 
Sisi tunapiga domo wenzetu kenya wanpiga hatua za maendeleo sijui lini tutabadilika wabongo sisi inakera sana kwakweli
 
Mtu sahihi wa kupambana na madawa ya kulevya nchini ni;
1.Rais wa Jamhuri
2.Waziri Mkuu wa Jamhuri
3.Waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Wengine ni maigizo na kupotezeana muda tu.
Mkuu nyuma ya mkuu wa mkoa yupo Rais ulimuandika hapo juu. Kumbuka kuwa asilimia zaidi ya 90 ya biashara ya Unga inafanyika pwani ya Afrika ya mashariki, jiji la Dar linaongoza kwa hapa Tanzania.

Makonda ni mkuu wa mkoa, ni Rais wa jiji la Dar kwa maneno mengine. Inawezakana wakuu wa mikoa waliotangulia walizoea kuwa ni ceremonial tu, watu wa kuwapokea viongozi pale airport na kutangaza kesho njia fulani na fulani itafungwa.

Huo ulikuwa ni upande mmoja tu wa cheo cha ukuu wa mkoa, upo upande mwingine wenye mamlaka, ni lazima tujifunze kuuzoea.
 
Kuna uzi hapa nimeuweka kwamba sitashangaa wapo watakaohoji "kwani 1.83g sio dawa za kulevya!" Sioni sababu ya kurudia tena hapa!
Hata kwenye huo uzi hukusema zinatakiwa gram ngapi ili iwe significant evidence. acha kukwepa swali kinapenape.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…