OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,045
- 114,500
Jana wabunge wetu bila kujali vyama vyao waliazimia kuitwa bungeni wateule wawili wa rais Magufuli ambao ni RC Makonda na DC wa Arumeru. Wabunge wote ikiwemo mawaziri waliunga mkono hoja ya Mbunge wa Chadema Mwita Waitara kwamba Makonda na mwenzake wamedharau mamlaka ya Bunge
Wachangiaji walienda mbali sana,Mbunge kutoka Tabora Chief Kadutu alieleza kiundani sana jinsi wateule wa Magufuli wanavyodharau wengine,alitolea mifano mingi lakini akasisitiza ukitaka kumtoa jinsi hutakiwi kulibembeleza "jini toooka(kwa sauti ya kubembeleza)". Hivyo lazima bunge litoe maazimio mazito
Hoja yangu ni kwamba wakati wa kuazimia wabunge na mawaziri ambao ni watetezi wa rais na serikali walikuwa kimya. Licha ya Mama Mhagama kujikakamua lakini wakati wakusema ndiyoooo wote waliitikia ikiwepo mawaziri.Na hakukuwa na sioooo pengine toka kwa mawaziri.
Hii ina maana nzito,mawaziri wamechoka na dharau toka kwa wale wanaojinasibu kuwa wapo karibu na rais. Wamechoka na A one man Show
Hongereni mawaziri. Kimya cha Waziri Mwigulu kina mengi

Ni lazima waunge mkono!! Hata viongozi wa majeshi yetu nao wangepewa nafasi hiyo, nao wangeunga mkono!
Makonda alimtuhumu hadharani Kamanda Sirro kwamba huenda kazipiga za wauza shisha! Nadhani moja ya mambo yanayomkera hivi sasa Kamanda Sirro ni pamoja na kukaa jirani na Makonda lakini ndo vile tena hana jinsi!!!
PM Majaaliwa nae alitiliwa shaka shaka kidogo na Makonda kuhusu suala hilo hilo la Shisha!
Mwigulu Nchemba yamepokwa madaraka yake ya Uwaziri wa Mambo ya Ndani na hivi sasa anaonekana ni kama asiyestahili kuwapo hapo alipo! Atastahili vipi ikiwa "madudu" yanayoibuliwa yalipaswa kuibuliwa na watu wa chini yake?! Hapa Makonda ni kama ameonesha Mwigulu ameshindwa kazi!
Above fact leads us to IGP Mangu!!!
Ingawaje IGP Mangu alisifiwa na JPM hivi majuzi lakini kama atatuliza kichwa sawa sawa alifahamu salamu zile ni kejeli kubwa dhidi yake! Anachofanya Makonda kilitakiwa kufanywa na watu walio chini ya Mangu! Sasa kama Mangu amesimamisha kazi maaskari waliotuhumiwa na RC wakati ni Mangu na timu yake ndio walitakiwa kuwafahamu maaskari hao kabla ya RC! Hakuna tafsiri yoyote ya hayo zaidi ya kwamba Makonda amemuonesha Mangu kwamba hajui kazi!!!
Kuna tume inaitwa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya! Chairperson wa tume ile ni PM na inaundwa na mawaziri kadhaa lakini hakuna RC!!!
Makonda ameteka mamlaka ya wote hao na hata ukimsikiliza anadhihirisha jambo moja tu! Kwamba anayofanya ni one-man show isiyo na msaada toka kwa yeyote zaidi ya rais! Hapa anaonesha wengine wote wapo wapo tu! Matokeo yake, hapahitaji kuwa na shahada kufahamu kwamba watu wamemsusia kiutu uzima!!
Kwavile kwa ujumla dunia ina wajinga wengi zaidi ukilinganisha na werevu, so to our country... kuna wajinga wengi zaidi kuliko werevu!!! Wajinga hawa wanadhani watu wanapinga vita dhidi ya dawa za kulevya... kutokana na ujinga wao hawafahamu kwamba watu hawapingi vita dhidi ya dawa za kulevya bali wanapinga approach inayotumika!
Kutokana na poor approach ndio pale tena ni majuzi tu hapa Tanzania imetangaziwa kwamba Wema Sepetu anajihusisha na dawa za kulevya lakini wanaishia kumpeleka mahakamani na ushahidi wa msokoto mmoja wa bhangi!!!
Lakini kama nilivyosema hapo awali, kwavile wajinga ndio wengi zaidi; wajinga hao wataendelea kuhoji "kwani msokoto mmoja wa bhangi sio dawa za kulevya!"
Kwa akili za kijinga msokoto mmoja wa bhangi wenye 1.83 gm unatosha kabisa kuwa dawa za kulevya na kwenda kutangaza through live tv coverage!
Na ni kutokana na kusheheni kwa akili hizi za kijinga, ndio maana hata wale walio na werevu wa kujua what's right and what's wrong; hivi sasa wamefunga mdomo kwa hofu ya kuambiwa na wajinga hawa kwamba wanatetea wauza dawa za kulevya!!!