MpangoA
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 360
- 233
Kusema ukweli Mzumbe ni moja ya shule yenye watu watulivu na upendo kuanzia kwa wanafunzi hadi walimu. Ni shule yenye nidhamu ya kipekee miongoni mwa shule za serikali. Kila mtu akifika pale mazingira yanambadilisha. Ukiona hali imefikia hapa ujue mambo yamefika ukomo.
Mazingira ya shule ni mabaya, maji machafu. Kipindi cha mvua hasa kuanzia April - June, kunakuwa na magonjwa ya mlipuko kama kuhara na ugonjwa maarufu mpaka ukatungiwa jina, Zongwe, au jina la kisayansi 'Zongwelisis Mzumbeata'. Ugonjwa huu uambatana na watu kuvimba usoni, na kuwashwa sehemu za siri.
Kwa wanafunzi na shule wao ni "Determination is Our Motto". Wao ni kitabu tu kwenda mbele despite the difficulties.
Majengo ya shule yapo toka mkoloni, makuukuu hakuna matengenezo. Naungana na wengine kuiomba serikali kusikiliza kilio cha Wanamzumbe. Mchango wa shule hii katika ujenzi wa taifa ni mkubwa hasa kwa kuzalisha madaktari, waandisi na wanasheria kabla ya miaka ya hivi karibuni vijana wake kubadilisha muelekeo na kupendelea fani za uchumi na biashara.
"Shule yetu Mzumbe Sekondari, yasifika kote Tanzania, malezi ya Mzumbe, elimu yake, ni kamilifu ya kitanzania, daima mbele nyumba mwiko"..nukuu ya maneno kutoka wimbo wa shule.