Mzumbe Sec Waandamana

Mzumbe Sec Waandamana

Haikuwa kwenda bunge Dodoma, walikuwa waende mjini kwa mkuu wa mkoa, ukitoa taarifa hakikisha ni sahihi ucpotoshe umma. Mzumbe ni vipaji kwa hakika.
Siasa hazihusiki katika hili swala.

Mnubi Simba, mimi ndiye niliyetoa taarifa na sikutoa taarifa hiyo kwa nia kama hiyo unayofikiri kwasababu mimi nikipotosha umma tena kwa jambo kama hilo sipati faida yoyote. Katika Mkakati wao hao wanafunzi ndivyo ulivyokuwa, kwenda Dodoma ingawa nakubaliana si tu na wewe bali na wote wanaosema mpango wa kwenda dodoma ilikuwa ni matishio ya wanafunzi. Walipokamatwa na kuhojiwa ndipo wakasema wanaandamana kuelekea kwa Mkuu wa mkoa ambaye ni rais wao hapa mkoani.

Tukio hilo limenifanya niongee na baadhi ya wanafunzi na pia na baadhi ya wafanyakazi, walimu na wasio walimu. Nimeuona upuuzi wa wanafunzi hao, mfano hawataki kile kitengo cha Mzumbe Book Project kiwepo eneo la shule kwa vile hakiwanufaishi wao moja kwa moja. Kitengo hicho ni cha siku nyingi hapo Mzumbe na wanafunzi wengi wamepita hapo bila malalamiko Kama hayo, hawa wa leo wana nini? Katika hali kama hiyo hata upumbavu wa kutishia kwenda Dodoma unaweza kujitokeza. Mtoa taarifa naomba nieleweke vizuri.
 
Tatizo mnaongea kiuanaharakati.

Hapo ulipo hujui mimi personally ninafanya jitihada gani kuhusu kuboresha Mzumbe. Kwa hiyo shutuma zako ziweke akiba kwanza.

Ukisoma vizuri na kuweka uanaharakati pembeni utaelewa ninachosema. Ila kama lengo lako ni kupindisha taarifa ili kuhalalisha uanaharakati basi endeleeni, lakini kuweki aware kuwa HAMTAFANIKIWA kwa njia mliyochagua.

Ninachosema ni hiki:
1. Matatizo ya miundombinu ni matatizo ya muda mrefu. Je, ni kwanini wanafunzi wamesubiri mpaka kipindi cha mitihani ndio waamue kuandamana?
2. Je, tathmini iliyofanywa na wanafunzi hao inaonyesha kuandamana kutawezesha vipi kutartua matatizo ya miundombinu?
3. Je, ni jitihada gani zimeshafanyika mpaka kufikia uamuzi huo wa kuandamana? Mwali Msuka wa Mzumbe aliwafundisha wanafunzi siku zote kwa ukifanya mambo kwa kufuata "right channel" utafanikiwa. Je, ni channel ipi mmefuata?

Hawa wanafunzi mimi ni wadogo zangu, na wewe kama ni miongoni mwao basi ni mdogo wangu na ni vema mkawa watlivu kusikiliza ushauri tunaowapa.

Mwanafunzi wa sekondari anatumia kati ya miaka 2 na 4 shuleni. Kwa kipindi hicho ni muhimu sana kubalance vipaumbele.
Kufanya maandamano kwa mguu mpaka Dodoma kwanza kunaashiria tatizo la fikra na pili inaashiria kushindwa kupanga vipaumbele ipasavyo. Kipindi cha mitihani ni kipindi maalum ambacho wanafunzi hata muda wao wa kula na kulala unategemewa kubadilika, huu sio muda wa kuandamana kwa matatizo chronic.

Hatujatofautiana, ninacho penda unielewe na ambacho hata wewe unakubaliana nacho ni kusahaulika shule hiyo kama zilivyosahaulika shule zingine ili hali mabilioni ya fedha yanafichwa Uswisi! Tofauti ya shule hii na shule zingine ni kwamba zingine zimejengwa baada ya Mzumbe enzi hizo ikiitwa Kichwere. Vijana wanaopita hapo wameonyesha jitiada ya kuwasikia walimu hata wakati fulani enzi za Mzee Mwasha (headmaster aliyemfuata Mzee Msuka) walipata kiburi wakadai kufanya vizuri katika mitihani kunatokana na juhudi zao wenyewe na si walimu!

Wanafunzi hawa si wa kwanza kuandamana na kuandamana si jambo jipya hapa nchini na nje ya nchi yetu. Kuandamana ni hatua ya mwisho inayochukuliwa na wahusika katika kufikisha ujumbe kwa ngazi nyingine na kwa jamii. Kama nawe una kiri kuwa Mzumbe kuna chronic problems, serikali iko wapi kuwaweka wanafunzi hao katika hali nzuri? Baada ya maandamano haya naomba uniamini, ujumbe umesogea na utaona kitu fulani kimefanyika shuleni hapo japo kitakuwa kidogo. Na sehemu zingine walikoandamana tuliona mabadiliko, na Mzumbe utaona yatakayotokea.

Labda nikuulize, kuna raha gani kufanya mitihani ili hali una matatizo? Mfano, pale Mzumbe pana wanafunzi 700 na wanafunzi hao wawapo darasani hutumia tundu moja la choo! Kuna wakati unakuta wamepanga foleni kwenda kujisaidia. Ni nini hiyo? Mitihani hiyo si ya taifa, inaweza kuahirishwa na hiyo haitakuwa mara ya kwanza. Tatua matatizo kwanza, mitihani baadae.

Unauliza kwanini hawajatoa madai hayo muda mrefu uliopita, hapa natamani ungeongea nao usikie kilio chao. Mpaka wamefika hapo hakika wametoka mbali kutoa madai yao. Lakini madai yao ni mengi na karibu yote yanahitaji fedha toka serikalini na serikali yetu nawe unajua hali yake kifedha. Na Mkuu wa shule Bw. Njawa hawezi kutoa mshahara wake ili atatue matatizo ya wanafunzi, jambo ambalo hata wewe usingeweza kulifanya. Ingawa katika hoja zako unadai una namna unayotaka kuisaidia Mzumbe. Naamini hutatoa mshahara wako kwani kwa mshahara wako kamwe huwezi kutatua matatizo yaliopo hapo.

Ushauri unapotolewa hupokelewa na si lazima utumike. Na udogo si kigezo cha kila utakachoshauriwa basi ukipokee tu. Na mimi si mwanafunzi wa Mzumbe Sekondari. Kiumri inawezekana nimekuzidi, mimi ni mtumishi wa serikali ninayehesabu miaka iliyobaki ili nisitaafu maana ndiyo michache na rahisi kuhesabu kuliko niliyotumikia nchi hii. Na si mwanaharakati, kama umeona kauli za kiuharakati; hiyo ni kwasababu ya maonezi hasa ya uongozi wa serikali yetu hasa ya sasa kwetu watumishi.

Aidha naomba nikueleweshe kuwa nimeongea na baadhi ya wanafunzi, walimu na wafanyakazi wasio walimu. Hakika Mzumbe ina matatizo makubwa lakini miongoni mwa madai ya wanafunzi ni ya kipuuzi mno. Mfano, tundu moja la choo lingeweza kutatuliwa na wanafunzi wenyewe. Kwa umri wao wangeweza kuchimba mashimo ya choo na wakaomba msaada aw serikali iwajengee sehemu itakayokuwa imebaki, hili sisi tulilifanya wakati tunasoma shule ya msingi na liliwezekana. Wanadai kile kitengo cha Mzumbe Book Project kiondoke kwa vile hakiwapi faida wao! madai Kama hiyo Mimi nimeyadharau bila kudharau maandamano yao.

Kama nimekukwaza, nisamehe sana Mkuu wangu
 
Kiukweli kuna ukiritimba sana wa wakuu wa shule wanaojifanya munguwatu kwa wadogo zetu hata ilboys kuna kipindi waliandamana hadi yule mkuu wao akaamishiwa pugu,poleni sana wadogo zangu kikubwa komaeni katika masomo.
 
Kwa vile unasema wewe sio mwanafunzi hakika unachochea kuwapotosha wanafunzi.

Na mnachokifanya kuwaharibia wanafunzi ratiba za mitihani ni jambo baya sana.

Halafu acha UONGO. Unasema wanafunzi wa Mzumbe wanatumia tundu moja la choo. Huu ni UZANDIKI. Si ukweli. Na hapa unadhihirisha kuwa hauna malengo mema, kwa sababu hukuwa n haja ya kutoa taarifa za UONGO.

Shule ina matatizo. Matatizo hayo yanapaswa kutatuliwa, lakini si sahihi kutumia matatizo hayo kwa maslahi ya watu wengine ya kisiasa.
 
Jamaa yangu, nafikiri una lingine na pengine unadhani na mimi ni mtu ninayejihusisha na ambiguous hayo unayoyasema SIASA! Kwasababu mimi siko uliko, naomba nitulie bila kujibizana na mtu wa aina yako na hilo litakuwa ndiyo jibu linalo kufaa.
 
Ni bora ukae kimya na tena usirudie tena kuleta uzandiki, eti Mzumbe wana tundu moja la choo...
 
Ni nyuma kidogo ya Kasanga, Maliasili. Matatizo yao ni mengi. Ujue shule ya Mzumbe ni ya siku nyingi, imechoka! Na Headmaster, Njawa, ni kijana na hana uwezo wa kuwavuta wakubwa huko serikalini ili waendelee kujali shule hiyo. Hivyo matatizo yaliopo Mzumbe ni makubwa kuliko umri wa huyo headmaster. Na serikali inataka kuziweka shule zote kuwa za kata kwa ukata! Inaumiza hata shule zake za wanafunzi wenye vipaji?! Bogus government!

Ujana au uzee wa mtu siyo hoja, hoja ni uwezo wa mtu katika kuongoza taasisi hiyo. Acha mtazamo finyu wa mambo. Joseph Kabila analiongoza li DRC na ni kijana lakini anajitahidi kulingana na hali ya kisiasa huko DRC. Sioni kikwazo kwa huyo Headmaster kijana kushindwa kuongoza iwapo uwezo anao.
 
Matatizo Mzumbe kweli yapo.

Nimeona picha za Mzumbe za hivi karibuni, hali si nzuri.

Hata hivyoi, bado sijaelewa uamuzi wa kwenda Bungeni umedhamiria vipi kutatua matatizo yaliyopo.

Je, ni kwanini wameamua kwenad leo? kwanini hawakwenda jana au kesho? Nategemea kusikia hatua mbalimbali zilozofuatwa mpaka kufikia uamuzi huo wa kwenda Bungeni.

Mara nyingi terminal exams zikikaribia kuna wanafunzia ambao wanabehave abnormally. Je, hiki ni kipindi cha mitihani ya muhula? If yes, kwanini harakati hizo zifanyike kipindi cha mitihani?
Hiyo ilikuwa nyakati zileeeeeeeeeeeee za kukimbia mitihani ama kuogopa, Mzumbe haijafikia hatua hiyo, Ni kilomita 200 tu toka Dar Mkuu unaweza kwenda kujionea kumbuka wengine ni wa kutoka maeneo ya Ngerengere na Mkuyuni na Kinole, mie nilikuwa nawasubiri hapa Magubike niwashauri.
 
Magimbi mwaka huu mmevuna?
 
hlw...kwanza nawapongeza vijana shupavu wa mzumbe secondary kwa walichokifanya..kwa tuliosoma pale na hata kuwa viongozi wa juu wa wanafunzi tunaelewa matatizo ya walimu wa ngazi za juu(WATAWALA),,na kwa kawaida wanafunzi wa mzumbe ni wapole na waelewa sana na mpaka kufikia hapo nafahamu kwa hakika kuwa hali si shwari..mimi nawaunga mkono wadogo zangu.. tupo pamoja daima mbele nyuma mwiko.....DETERMINATION IS OUR MOTTO
 
Ujana au uzee wa mtu siyo hoja, hoja ni uwezo wa mtu katika kuongoza taasisi hiyo. Acha mtazamo finyu wa mambo. Joseph Kabila analiongoza li DRC na ni kijana lakini anajitahidi kulingana na hali ya kisiasa huko DRC. Sioni kikwazo kwa huyo Headmaster kijana kushindwa kuongoza iwapo uwezo anao.

Uzee dawa Ndg yangu. Kijana hapa kwetu na hasa katika hali hii mbaya ya kiuchumi, anakosa uwezo ushawishi kwa walioshika mpini. Kila akisemacho anaambiwa fedha hakuna. Matokeo yake hali imefika wanafunzi kuandamana kwasababu matatizo yamekua, yamekomaa na sasa yanazaa matunda aina ya maandamano. Ngoja tusubiri hatima ya yote.
 
Magimbi mwaka huu mmevuna?

Kinole ndizi zao zinaishia Mkuyuni na pale Kinole penyewe kwa bei ya chini sana, achilia magimbi ambayo wataanza kuuza wakati wa mfungo, agenda 2015 ni pamoja na hiyo ya kutafuta soko la uhakika kwa maagimbi unayoulizia, nilifika Lumumba leo, naona vijana wengi wameenda katika chaguzi na kusimamia ziara ya wakubwa kule Njombe, teh teh teh!
 
Kinole wana SACCOS iliyokuwa very successful. Ni mfano wa kuigwa. Changamoto kubwa kwao ni barabara.

Wanayo mpaka mafuso ya kusafirishia ndizi, mashelisheli, magimbi na bidhaa nyingine ila mvua zikinyesha magari yanakwama na kupata ajali. Hii inawaletea hasara.

Jitihada zimefanyika kurekebisha "maeneo korofi" kwa kuweka slabs, lakini hiyo haitoshi.

Kuboresha barabara ipitike mwaka mzima ni LAZIMA iwekwe kwenye agenda ya halmashauri iwapo tunataka maendeleo yaende kwa kasi.
 
Mbona kwa news wamesema wanataka onana na RC Bendera sasa hayo ya dodoma yanatoka wapi tena?
Atlast waliamu akuonana na RAS
 
Ni bora ukae kimya na tena usirudie tena kuleta uzandiki, eti Mzumbe wana tundu moja la choo...

Hii yote ni sababu ya kulamba ------ ya wakubwa serikalini ili maisha yaende. Kafanye kazi kijana humu JF utakufa siku si zako kwa BP. Unatoka povu na mambo ya Mzumbe Sekondari as if Mzumbe Sekondari haina matatizo na kama ni mali yako au ya ukoo wako! Kweli umasikini mbaya sana! Kama hujalipwa njoo tuendelee kulumbana na kama umelipwa endelea kutafuta kibarua kipya, na nitakusamehe.
 
Mbona kwa news wamesema wanataka onana na RC Bendera sasa hayo ya dodoma yanatoka wapi tena?
Atlast waliamu akuonana na RAS

Mleta mada ni mzandiki.

Anataka kuwadhalilisha wanafunzi wa Mzumbe ili waonekane hawajui kufanya maamuzi sahihi.
 
Uzandiki wangu uko wapi? Mzumbe sec hawakuandamana? Au hawana matatizo? Au ulitaka niandike uvitakavyo wewe? Hasira za ugumu wa maisha na hasira za ugomvi wenu nyumbani, msizilete JF.
 
teh maswaiba wetu bwana?vipi tena hii ndo serikali mliyoiweka madarakani
 
Back
Top Bottom