Mzozo wa CHADEMA na TBC: Nitasema mimi kiazi, wewe muhogo una mzizi'!

Siasa ni maisha unayoishi binaadamu yeyoye siasa inaweza amua ukaishi kama digi digi siasa inaweza amua ukaishi kama upo peponi unataiacha siasa siku utakapo ingia kaburini mtu unaposema wewe sio mwanasiasa wakati siasa hizo hizo ndio zinakuendeshea mfumo wako wa maisha kila siku huwa nakushangaa sana nikuweke kwenye kundi gani kilazaaa au mbulula
Sasa unalia nini!
 
ZERO BRAIN tu ndiye anayeweza kuandika upuuzi kama huu.

Mbowe na genge lake la wahuni waliogopa drones za TBC maana zilikuwa zinarusha kila kitu hewani wakaona wataumbuka kwa mwitikio kiduchu wa watu ndo wakaamua kuwafukuza TBC wakati tukiwa tunaanaglia live
 
MZOZO WA CHADEMA NA TBC: 'NITASEMA MIMI KIAZI, WEWE MUHOGO UNA MZIZI'!

Wiki iliyopita nilihudhuria Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Tundu Lissu katika Viwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam. Kama kawaida yangu, nilitoa nasaha au hotuba fupi kabla ya kuufungua Mkutano ule kwa Sala. Baada ya hapo viongozi kadhaa wa CHADEMA walihutubia akiwemo Mwenyekiti wake Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Kulikuwepo na vyombo kadhaa vya Habari likiwemo Shirika la Utangazaji la Tanzania, TBC. Yapo matendo yaliyoonyeshwa au kufanywa na TBC yaliyopelekea Mheshimiwa Mbowe kuwafukuza mkutanoni siku ile. Kama Askofu nilishtuka na kushangaa kwa kuwa tukio lile halikuwa la kawaida ingawa kwa tulio wengi lilikuwa na tafsiri yake katika 'ulimwengu wa roho'. Mwitikio (reactions) kutoka kwa Mbowe ulikuwa wa ghafla (instant) ambao hata hivyo ulionekana kujengwa katika misingi ya kihistoria ya mahusiano kati ya CHADEMA au Viongozi wake na TBC.

Askofu ni mtetezi wa haki na haki haina upendeleo! Lakini katika tukio lile, Askofu alijikuta akikutana na mwitikio (reactions) kutoka kwa watu wanaodhani kuwa hawakutendewa haki na TBC. Kwa kuwa Askofu alikuwa ameukabidhi Mkutano ule mikononi mwa Mungu na kusafisha anga lote la Mbagala, akiendelea kuwa mtulivu kwa kuwa aliamini kuwa mbingu zilikuwa kazini.

TBC ni taasisi ya Umma inayoendeshwa kwa kodi za wananchi wa Tanzania wakiwemo wafuasi wa CHADEMA na vyama vyote vya Upinzani. Huko nyuma niliwahi kuisema TBC hadharani kupitia ukurasa wangu kuwataka waache upendeleo. Ni dhahiri kuwa baadhi ya matokeo ya hisia za upendeleo ni yale tuliyoyaona kule Mbagala wakati TBC ilipofukuzwa Mkutanoni. Watangazaji, Wapiga Picha, na Waandishi wa Habari wa TBC ni watoto wa nchi hii. Wao hawahusiki sana kwa kuwa wako chini ya watu wanaotoa maelekezo. Kama kuna shida ye yote kuhusiana na utendaji wa TBC wasilaumiwe hao, bali walaumiwe waliokabidhiwa kuongoza TBC akiwemo Mkurugenzi wake Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi.

Mara kadhaa TBC imerusha hewani maudhui ya viongozi wa serikali inayotokana na CCM pasipo kukatisha matangazo hayo hata kama baadhi ya viongozi hao wametoa kauli ambazo kwa muono wetu kauli zile zinadharirisha watu wengine! TBC na Vyombo vingine vya Habari kwa pamoja vimevumilia maudhui kama hayo kurushwa mubashara pasipo kukatizwa. Hivi karibuni nimewasema Star TV kwa kuruhusu maudhui yaliyokuwa yanamfedhehesha Mgombea Urais wa CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu kupitia kipindi cha 'Agenda 2020' kinachoongozwa na Aloyce Nyanda 'Mtozi'! Star TV haikukatiza matangazo yale ingawa huko nyuma iliwahi kukatiza matangazo ghafla wakati mmoja wa viongozi wa CHADEMA akitoa hoja.

Vitendo vya kuchagua maudhui ya kurusha kwa upande wa Upinzani na kutokuchagua maudhui ya kurusha kwa upande wa CCM na Serikali yake ndivyo vinavyopelekea baadhi ya Vyombo vya Habari ikiwemo TBC walaumike na kuhisiwa kuwa wana upendeleo. Haijawa mara moja baadhi ya Vyombo vya Habari kusitisha matangazo kwa muda endapo yanayoongelewa na Wapinzani yanaonekana kuwa tishio kwa CCM na Serikali yake. Lakini vyombo vya Habari havitakiwi kufika huko. Vyama vya Siasa vyote vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu ni vyama halali na chama chochote kati ya hivyo kinaweza kushika dola. Hakuna Chama cha Kigaidi katika hivyo, la sivyo visingelisajiliwa na kuruhusiwa kushiriki Uchaguzi Mkuu.

Vyombo vya Habari na hasa TBC watende haki na watimize wajibu wao pasipo upendeleo hasa ikizingatiwa kuwa wao wanaendeshwa kwa kodi za Watanzania wote.

Tunatoa wito kwa TBC na CHADEMA kuketi na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. Tunahimiza uvumilivu kwa pande zote mbili wakati wa kushughulikia jambo hilo. Taasisi zote mbili yaani TBC na CHADEMA wajizuie kuendelea kutoa kauli endelezi hadharani kuhusiana na suala hilo zaidi ya kutafuta suluhu.

Wazaramo wana msemo usemao: "Sema wewe kiazi, nikisema mie muhogo nina mzizi'! Na mimi kama Askofu nimeamua kusema yale ambayo wengine wanaogopa kuyasema!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Nina kubaliana na wewe unaposema kwamba TBC wame onyesha upendeleo mkubwa kwa muda mrefu ila kitu ambacho wana CHADEMA wana shindwa ku tambua ni kwamba shirika hilo lina rusha matangazo yanayo tizamwa na watanzania wengi kuliko mashirika mengine. Huu sio muda muafaka kwa wana CHADEMA ku angalia ya zamani. TBC wana weza ku wasaidia sana kwenye kampeni zao
 
Back
Top Bottom