Mzizi wa fitna: Pacome vs Chama, nani zaidi?

Kama Chama ana class kwanini hakuna timu yeyote ile inayomuhitaji? Katoka Berkane karudi Simba na hapandi daraja ya kutakiwa na timu nyingine za daraja la juu?
Kwasasa kila mwana Yanga anaingia mashaka, huenda Pacome akakosekana msimu ujao. Na hili nakuhakikishia Pacome akiendelea na performance yake hiyo hiyo hatobakia Yanga msimu ujao ila Chama utasikia tetesi zake za kutakiwa na Yanga pekee basi.

Wachezaji wazuri huwa wanaonwa na timu zingine uwezo na ubora wake. Sasa mchezaji anaishia kuimbwa na watanzania pekee kila msimu. Usikii tetesi yoyote ya kutakiwa na timu nyingine za nje.
Messi akiwa Barca ile ya akina Iniesta ,timu gani ilituma ofa kumsajili?
 
Messi kaishacheza timu tatu mpaka sasa. Hata alipokuwa anachezea Barcelona ndiye alikuwa mchezaji ghali zaidi kumsajili. Na timu nyingi sana zilikuwa zinamuhitaji. Sasa mara mwisho kusikia tetesi ya Chama kuhitajika ni lini? Ukisikia tetesi basi anahusishwa na Yanga pekee na sio kuhusishwa na vigogo vya soka Africa.
Taja timu iliyomhitaji Messi mwaka 2009-2014 na kitita walichoweka mezani usilete blahblah
 
Pakome umri unamruhusu anaweza kwenda timu nyingine na Hata kubakia Yanga na kufanya makubwa zaid ya chama, Chama ana miaka zaid ya 30 inawezekana Hata asifanye vzr kama mwanzo ila kashafanya makubwa mwa muda mrefu ila Kwa Pakome miez hii 8 tu aliyochezea Yanga haitoshi kumuweka daraja Moja na chama Bado ana safari ndefu sana. Otherwise chama atabakia kuwa mchezaji Bora wa muda wote kwenye ligi kuu ya tz
Hayo makubwa kafanya akiwa na timu gani?
 
Hawa wachezaji wote muhimu kwenye timu zao, Pacome kaisadia timu yake kumfunga Simba 5 Chama akiwa uwanjani na pia kufuzu robo CCL
Chama kaisaidia Simba kushinda 6 kwa Jwaneng Pacome hakuwepo na kufuzu robo CCL.
Hata timu zao zilipokutana misimu ya nyuma Simba alishinda 2 Dar akaenda kupigwa 3 ugenini kinara akiwa Aziz K.
Sina kumbukumbu kama Chama ni MVP kwenye ligi yetu au alipokuwa kwao Zambia, wenye takwimu mtusaidie, ila Pacome kaja akiwa MVP huko kwao na kwa performance yake kwenye ligi sitashangaa akiwa MVP wa msimu huu.
Kila mmoja ni mzuri kwa nafasi yake na kama mnataka kujua thamani zao wawekeni sokoni leo wataalamu watawasadia kuwaambia nani ana thamani kubwa kwasasa.
Hatukarai Pakome kuweza kuhitajika zaid sokoni sababu ya umri wake. Tunachosema Ili afananishwe na chama acheze Kwa ubora Huu Kwa miaka zaid ya mitano. Ni kama kama Halland au mbape kufananishwa na Mess Au Ronaldo. Sio kwamba wabovu ila wanahitaji kuprove Kwa kuonyesha kiwango Chao Kwa muda mrefu kufikia daraja la kina Ronaldo.
 

Attachments

  • Screenshot_20240303-102508.png
    Screenshot_20240303-102508.png
    160 KB · Views: 3
Hatukarai Pakome kuweza kuhitajika zaid sokoni sababu ya umri wake. Tunachosema Ili afananishwe na chama acheze Kwa ubora Huu Kwa miaka zaid ya mitano. Ni kama kama Halland au mbape kufananishwa na Mess Au Ronaldo. Sio kwamba wabovu ila wanahitaji kuprove Kwa kuonyesha kiwango Chao Kwa muda mrefu kufikia daraja la kina Ronaldo.
Hii misimu miwili yanga anachukua kombe la nbc chama kaonyesha ubora gani
 
Embu nitajie timu zinazomuhitaji pacome, nyie yanga kama mliweza kumchukua nungunungu ndio mtakuwa hamumtaki chama kweli?
Ulisoma ukaelewa au umekimbilia ku comment? Nimekwambia mashindano haya ya klabu bingwa yakiisha sio ajabu kuona Pacome akiwaniwa na vilabu mbalimbali huku Chama ikawa kama kawaida yake, hakuna timu yenye aja nae.
 
Ulisoma ukaelewa au umekimbilia ku comment? Nimekwambia mashindano haya ya klabu bingwa yakiisha sio ajabu kuona Pacome akiwaniwa na vilabu mbalimbali huku Chama ikawa kama kawaida yake, hakuna timu yenye aja nae.
Kwa hiyo unatembea kwa hisia?
 
Back
Top Bottom