Tape measure
JF-Expert Member
- Nov 26, 2015
- 1,980
- 3,579
Habarini wakuu wa jukwaa,
sitaki kupoteza muda tena nimeamua kuishi peke yangu na siitaji uhusiano na mtu yeyote,, Natumai utakuwa umenielewa Kevi!!!! Kisha akanikatia simu hii ndio kauli aliyoniambia mpenzi wangu nilipompigia simu usiku ili kumtakia usiku mwema.
Maskini Kevi mimi kauli ya huyu mrembo haikuwa geni sana kwangu kwani ni miezi michache tu imepita tokea nimwagwe na mrembo wa chuo niliyejitahidi kufungua pochi mpaka nikaitwa lofa wa malovido na mkasa huu ulitokea baada ya kumwambia kua pesa unayoomba sina ila nina kiasi kidogo kama laki 2 ambacho nilitarajia kununulia stand ya TV lakini kwa kuwa nakupenda nitakutumia mpenzi wangu akanijibu Asante darling mwaaaaah.
Nakumbuka baada ya kwenda tigo pesa nakumtumia 195,000/ akanijibu bby mbona haijafika laki 2 nikamwambia 5,000 nimeibakiza katika accounti yangu. Akanijibu sitaki kupoteza muda tena nimeamua kuishi peke yangu na siitaji uhusiano na mtu yeyote Kevi Mungu akupe nguvu katika maisha yako ufanikiwe mpaka ushangae, Nakuomba usinisumbue tafadhali. Nilihisi kuchoka gafla nikahisi kama mapigo ya moyo yanashuka na malaika mtoa roho ananinyemelea. Sijui kwa nini ile hali ilinitokea kwa sababu laki 2 haikuwa kiwango kikubwa sana cha pesa kunisumbua mimi kiasi kilee.
Uhusianao wa nyuma sitaki kukumbuka kwa sababu baada ya kumtumia tu mpenzi wangu pesa ya kusuka aliniomba nimtumie pia na pesa ya nauli nayo nilituma. Chakushangaza hakupokea tena simu yangu wala kujibu message. Nasikitika sana kwani nilifuta namba yake na hakuwahi kunitafuta tena Maskini kevi mimi.