foxolox
Member
- Nov 24, 2015
- 14
- 3
Acha nikupe ubuyu, Mzee Yusuf akiwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa leo ametoa ya moyoni kuhusu wake zake wawili. Taarifa za chini ya kapeti zinasema mashabiki wamefanikiwa kuwaweka wake hao kwenye tofauti kiasi cha wao wenyewe kuwekeana bifu za kutofautiana na kufanyiana tambo hadi kwenye mitandao ya kijamii.
Akiongea Mzee Yusuf Mwenyewe anasema "Labda hao wake zangu mie wananiona mimi fala na hawanipi heshima yangu na hasa huyo anaetaka kufanya mambo ya vituko vituko, binafsi sipendi na sifurahii vile vitu najaribu kuwaasa tena humo humo kwenye instagram nawaambia angalieni hawa washabiki maandazi hawa waangalieni lakini sasa utakuta mtu mwenyewe anapenda vile vitu".
Aliendelea kusema "Itakuja siku na mimi ntafanya ninalolitaka mimi mtu asije akalalamika mimi ntachoka vilevile. Mi siongei, mi sibahatishi, mi najiamini si bahatishi, alafu mimi siogopi mwanamke tatizo langu, mimi sijawahi kuogopa mwanamke. Saa zingine mtu labda anaona aaa mimi nishazaa nae bwana hawezi akanifanya chochote"
Nawasihi kwamba waache vituko wafikirie maisha yao wasifikirie kwamba mimi ndo mzuri sana sijui mi ndo fulani mi ndo mzuri zaidi, tambo za kijinga hizi haina haja, Ameongeza Mzee Yusuf'

Last edited by a moderator: