Mzee wetu Mohamed Said, kesho una nini?

nasaluka

Senior Member
Jun 20, 2015
149
184
Bila shaka kesho(12/1/2017) ndio ile siku ambayo serikali halali ya Zanzibar ilipinduliwa na kuingia mikononi mwa wanyang'anyi na hiyo shughuli ambayo inasadikiwa uligharimu maisha ya watu wasiopungua elfu tano(5000) kati ya watu wasiozid elfu hamsini(50000), ilianza mida hii ya maghribi na ilidumu kwa siku zisizipungua miezi miwili.

Inasemekana shughuli hii ilisimamiwa na yule anaejulikana kama mungu wa Afrika .

Mzee wetu tunataka taarifa zaidi juu ya tukio hili la kuhistoria na tunataka toka kwako maana kwa sasa umekuwa ukiaminika sana katika uga huu wa historia ingawa wengi wao ni ngumu kukiri hili.

Ni matumaini yangu kwamba utandaa kitu katika hili

Ahsante.
 
Huyu Mzee ni Kiboko wa Historia ya Wazee wake waliokuwa wanaishi Dar es Salaam halafu anawaita eti ndio wapigania uhuru wa Tanzania.
Anachekesha sana huyu mzee.
 
Hilo halina ubishi mkuu kwamba kwa sasa huyu ndie mwamba wa historia ya uhuru wa tanganyika, anachowazidi wengi ni kuwa na primary data nyingi ambayo ndio source namba moja ya historia yeyote ile

Kwa hiyo hata ukaonge kwa kubeza ni kazi bure na ye anaendelea kufichua tusiyoyajua.

Tunakusubiri mzee!!
 
Huyu Mzee ni Kiboko wa Historia ya Wazee wake waliokuwa wanaishi Dar es Salaam halafu anawaita eti ndio wapigania uhuru wa Tanzania.
Anachekesha sana huyu mzee.
Farudume,
Haiwezekani mimi kuwa mchekeshaji.

Wazee wangu wamefanya mengi nakuwekea hapa historia fupi
ya babu yangu Salum Abdallah ili wote waamue kati yetu mie na
wewe nani mchekeshaji:

Uncle Jei Jei:
Tatizo Nyerere si muislam kwa dini wala mmanyema kwa kabila.
Na kibaya zaidi, baba wa mwandishi huyu, aliwahi kuwekwa rumande na serikali ya Nyerere baada ya kuleta chokochoko za kidini zilizoanzishwa na AMNUT.
Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo
akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.
 
Nasaluka,
KIPINDI MAALUM CHA KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 1964 TV AZAM NA UHAI FM 107.30[/paste:font]
Kesho Mapinduzi Day In Sha Allah nitakuwa na Kipindi Maalum Azam TV kuhusu Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar 1964 saa moja unusu asubuhi. Wakati huo huo Uhai FM 107.30 watarusha kipindi ambacho walinirekodi leo kuhusu hayo hayo mapinduzi.

CXHC0D4hyhS1G-UWet3BrtzgtnbtDHS1C7nJ-qKshO0zD7gjnbhFnFjPybU3dpE0eHX4f9cvE-32uWeoyTwwildBV0DtuTUb7Y0q4A-GcZOrrzDHASpKKpLmOTCSJbUntSKZuxVqrSmzOxMg66v0dHO4V880qdX2buMqJUj1MGjS_wnd7rhnW92AmkuW9MvtKWiVyudUl2ru_GQxMlwdOJHZQGAS4MfLlRybRdoWqAw6qZQTKFEFaqkjNQSCtWLM1bfQyxcHS6i9o2Mq2rt6Z0V7k1kNYXciMKCGzQHFYziGIoAHEthwdP1gNoTE4luQTERH3IF7cVFbcw1ZU_3kL6aKqdKPE18S3BJOVPfpkjzz4UPnL2lJHHrCIPs_CcFp6zlzSx1dgUQxRI1BiuC3QVdUrmgjyHx9mlHAm8vZiYbVPG3zB1MZLX0JyFbji5p93ibEdn5JNO0DvxiQwcUdYXYyRaRz3py7gydMOP4tz2LxxS2YqB_8PoH-dL0a0n7oLSjSQHqtIrcAjaD7xoBnBodFajPuaMtr5-pWcowaCafiKgssqnQ71GxWjcK0VoIe_W_akZCcdogozgu3_ZLGvsysaTqWmY0_zE_bFONWAUGUl1qhiA=w1231-h692-no

Mtangazaji Fadhili Haule wa Uhai FM 107.30 akifanya mahojiano na Mwandishi Kipindi Maalum Cha Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar 1964

Ingia hapa kuangalia picha:
Mohamed Said: KIPINDI MAALUM CHA KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 1964 TV AZAM NA UHAI FM 107.30
In Sha Allah tutafuatilia na kuleta humu mrejesho.
Paskali
 
Farudume,
Haiwezekani mimi kuwa mchekeshaji.

Wazee wangu wamefanya mengi nakuwekea hapa historia fupi
ya babu yangu Salum Abdallah ili wote waamue kati yetu mie na
wewe nani mchekeshaji:

Uncle Jei Jei:
Tatizo Nyerere si muislam kwa dini wala mmanyema kwa kabila.
Na kibaya zaidi, baba wa mwandishi huyu, aliwahi kuwekwa rumande na serikali ya Nyerere baada ya kuleta chokochoko za kidini zilizoanzishwa na AMNUT.
Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo
akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.
Daaaaah huwa najifunza mengi sana kutoka katika maandiko yako we mzee. Kweli nilikua sijui kitu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom