Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) jijini Dar es Salaam, Bishop Zachary Kakobe ni miongoni wa watu wenye umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania, kutokana na huduma zake za kiroho kama Mtumishi wa neno la Mungu.
Lakini si hivyo tu, Bishop Kakobe ni mmoja wa watu wenye ushawishi hasa kwa waumini wake na hata wale wasiokuwa waumini lakini wanapenda kumfuatilia.
Katika kumbukumbu mwaka 2010, Askofu Kakobe aliwahi kuingia kwenye mvutano mkali na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akipinga utekelezaji wa mradi wa kupitisha umeme wenye msongo mkubwa mbele ya Kanisa lake lililopo eneo la Lufungira-Mwenge jijini Dar es Salaam.
Si hivyo tu, Askofu Kakobe amewahi kukumbana na matukio mengi nje ya Injili kama;
- Kudai Serikali ya Tanganyika
-Kuhojiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
- Kushtakiwa kwa kesi madai ya ubadhirifu
-Kushawishi watu kukubaliana na chanjo ya Corona
Pamoja na hayo machache kuhusu Askofu Kakobe, katika kipindi hiki ambacho Tanzania inapitia misukosuko ya matukio mabaya kama utekeji, watu kupotea, kuingiliwa kwa uhuru wa kuabudu, ufisadi kushika hatamu, kukandamizwa kwa uhuru wa vyombo vya habari, utoaji maoni na waandamanaji kuuliwa hajawahi kusikika popote akizungumza aidha kuwa kutoa maoni yake au akikemea wala kuzungumzia lolote juu ya hayo na sio kawaida yake.
Kuna nini kinaendelea? hata asipoongelea kuhusu yanayoendelea hapa nchini basi hata Kanisani kwake tumsikie.