Mzee Warioba na hoja fikirishi ya Mwalimu Nyerere kutohutubia Kanisani

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Nilimsikiliza vyema Waziri Mkuu mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba pale alipopewa nafasi ya kuhutubia nyumbani kwa Mwalimu Nyerere pale Msasani kama sehemu ya sherehe ya kufikisha miaka 100 ya hayati Mwalimu.

Aliongea kwa lugha nzuri kama mwanasheria na mtu muungwana. Akamuelezea Mwalimu Nyerere jinsi alivyokuwa akimfahamu tangu alipokuwa kijana kabisa. Tukumbuke kuwa mwaka 1961 Mzee Warioba alikuwa ni mmoja wa vijana waliokuwepo pale uwanja wa Uhuru siku ya tarehe 9 mwezi Desemba. Hivyo anamfahamu vyema hayati Mwalimu.

Akiwa anaendelea kujenga hoja ya unyenyekevu(humility) wa hayati Baba wa Taifa akaongelea suala moja lililoniacha nikiwa nimezama katika fikra nyingi aple aliposema kuwa Mwalimu Nyerere hakuwahi hata mara moja kuhutubia kanisani.

Nikaona kamera ikizungushwa na akaonyeshwa Amani Karume mdogo wake na rais wa zamani wa Zanzibar, macho yake yakawa yanatazama juu hewani kama alikuwa na mawazo fulani yaliyomjia kichwani muda huo.

Kwamba Mwalimu Nyerere alipenda mno kujishusha na hakulewa na madaraka.Siku zote alikuwa tayari kujiweka katika nafasi ya mtu wa kawaida pasipo uwepo wa dalili wala viashiria vya makuu, ni kama Mzee Warioba aliamua kusisitiza kwa viongozi wa sasa waendelee kujishusha wawe ni watu wa kawaida wasiwe ni Miungu watu.

Nikakumbuka miaka ile ya 1980 pale kanisani Saint Joseph Hayati Baba wa Taifa alikuwa siku moja moja akipenda kusali. Kilichokuwa kikituonyesha kwamba yeye ni rais ni kwamba kile kiti chake kirefu kilikuwa kikikaliwa na watu watatu tu. Yeye mwenyewe katikati kushoto mlinzi mmoja na kulia mlinzi mwingine. Hakuwa na mbwembwe za kutaka kupewa kipaza sauti wakati misa ikiwa inaendelea ili eti aanze kutoa maagizo mle mle kanisani.

Hoja kama hii ya Warioba ni nzito na pengine katika utu uzima wake alionao kwa sasa ni wakati muafaka kufikisha ujumbe kama ule ule aliousema Askofu Niwemugizi kwa Samia kule Kagera. Kwamba cheo chako kipo leo na kesho kinakwenda kwa mtu mwingine, hivyo tumia busara siku zote katika maamuzi yako.

Nakumbuka JK katika kumuongelea akasema kitu alichojifunza kwake ni kauli yake kwamba hoja hujibiwa kwa hoja na siku zote haipigwi bunduki. Kutoipiga bunduki hoja ni pamoja na kuwa na uwezo wa kujifanya wewe ni wa kawaida tu hata kama yanayosemwa dhidi yako yanaiumiza nafsi yako.

Pia ni kama ile picha maarufu ya Bilionea Bill Gates aliyoipiga akiwa kapanga foleni huko USA kavaa jeans yake kama vile ni mtu wa kawaida tu.

Anajishusha na kutojikweza siku zote, jaribu kumuweka Gates na pesa zake na ushawishi wake katika nafasi ya hawa matajiri wanaomiliki mabasi ya mikoani na vituo kadhaa vya kuuza petroli, namna wanavyotaka wanyenyekewe kama vile wao ndio wanaowapa binadamu wengine uhai na kuuondoa!.

Tutamkumbuka sana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu wa kawaida mwenye ucheshi mwingi na busara nyingi. Lakini ndani kabisa ya nafsi yake akiwa mtu wa kawaida kabisa.

Ukikutana nae pale ikulu katika zile koridoo karibu na yule Simba aliyekaushwa miaka ile anakuwekea mkono kichwani na kukuuliza hujambo mwanangu!?. Ni kama jana tu lakini inakaribia miaka 40 sasa.
 
Nyerere alihudumu kipindi cha mfumo wa chama kimoja.

Na hata kura alikuwa hashindanishwi na yoyote ndani ya CCM

Hata mzee Malecela pale St Alban Upanga utaratibu ulikuwa ni huo huo.

Mfumo wa vyama vingi unahitaji mambo mengi pia.

Huyo huyo Nyerere alimwingiza Mandela Ikulu wakati ameshastaafu, ingekuwa leo maneno yangekuwa mengi sana!
 
Nilimsikiliza vyema Waziri Mkuu mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba pale alipopewa nafasi ya kuhutubia nyumbani kwa Mwalimu Nyerere pale Msasani kama sehemu ya sherehe ya kufikisha miaka 100 ya hayati Mwalimu...
Nyerere alikuwa msomi wa falsafa, kamsoma John Stuart Mill Edinburgh Scotland na kumuandikia papers, anajua separation of church and state ni nini.

Ndiyo maana hakuhubiri kanisani.

Kuhusu humility, kuna siku Mama yangu alivyokuwa anafanya kazi Ikulu, alikuwa anakata kona kwenye corridor moja ya Ikulu. Ikawa bado kidogo agongane na Nyerere uso kwa uso, kwa sababu hakumuona kwenye kona.

Basi Mama akawa ameogopa sana akaona atakaripiwa na Nyerere. Akaja kumkuta Nyerere mwenyewe ndiyo yuko so concerned kuhusu hali ya Mama, alimuona Mama kama kapanic hivi, Nyerere akawa anamtuliza anamuuliza kama yuko poa.

Nikasema, mtu mwenye cheo kikubwa anavyo ji conduct akiwa peke yake na staff wake inaonesha mambo mengi sana kuhusu integrity yake.

In this capacity, Nyerere was the consummate gentleman.
 
Nyerere alikuwa msomi wa falsafa, kamsoma John Stuart Mill Edinburgh Scotland na kumuandikia papers, anajua separation of church and state ni nini.

Ndiyo maana hakuhubiri kanisani.

Kuhusu humility, kuna siku Mama yangu alivyokuwa anafanya kazi Ikulu, alikuwa anakata kona kwenye corridor moja ya Ikulu. Ikawa bado kidogo agongane na Nyerere uso kwa uso, kwa sababu hakumuona kwenye kona.

Basi Mama akawa ameogopa sana akaona atakaripiwa na Nyerere. Akaja kumkuta Nyerere mwenyewe ndiyo yuko so concerned kuhusu hali ya Mama, alimuona Mama kama kapanic hivi, Nyerere akawa anamtuliza anamuuliza kama yuko poa.

Nikasema, mtu mwenye cheo kikubwa anavyo ji conduct akiwa peke yake na staff wake inaonesha mambo mengi sana kuhusu integrity yake.

In this capacity, Nyerere was the consummate gentleman.
Mkuu Kiranga wewe unaweza kuwa kaka yangu fulani wa miaka ileeee. Mama kufanya kazi ikulu umenishtua kidogo.
 
You should have seen the pain portrayed by Magufuli's assistants the day he was pronounced dead; you then would have realized how much they revered him! Hakuna Rais anayechukiwa na watu wanaofanya kazi IKULU!
Hayo ni mambo public, of course watu watataka kujionesha wana pain.

Kujua ukweli inabidi ukae nao private kama mimi nilivyokaa na Mama yangu.

Inawezekana kuna watu walikuwa wanakaripiwa kama watoto walikuwa hawapendi.

Magufuli alikuwa na hulka hiyo.
 
Back
Top Bottom