Mzee wa upako: CCM ya Kikwete ni mbaya kuliko rais Gaddafi

Hao watu wa gazeti la nyakati leo, nao ni wanafiki. Nadhani nao ni wanamtandao wa Lowassa. Inakuwaje wanakurupuka kuandika habari controversial kama hii? Wangekuwa na akili wangegundua kuwa lazima wasomaji wao watahiji juu ya huu msimamo wa askofu vs msimamo wake wa kumtetea na kumpaka mafuta Kikwete mwaka jana. Wangemuuliza hilo ili kubalance habari..

Hakuna kilichosalimika. Hata magazeti yanayotakiwa kuhubiri masuala ya kiimani nayo yameingia kwenye mnada uliowapelekea kupakatwa na mafisadi. Kama imewezekana kwa wakubwa zao, kishindikane nini kwenye vyombo vya habari wanavyoviendesha?
 
Njooni kwenye kanisa langu ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Fuatilia mahubiri na ibada zangu online.
Ni mimi mchungaji wako mpendwa,
Bujibuji
 
nikumbusheni kipi ni kibaya kuchanganya siasa na dini au kuchanganya dini na siasa?
kwa maana hapo huwa wananiacha gizani.
 
nikumbusheni kipi ni kibaya kuchanganya siasa na dini au kuchanganya dini na siasa?
kwa maana hapo huwa wananiacha gizani.

Hamna kibaya hapo kwani kuna ubaya gani kujamba wakati unakunya?? wote wanatumia watu kupata hela na hamna kingine.
 
nesahau mkulu aliwaweka wazi waache kuleta madawa ya kulevya? ndo maana wanamchukia sasa. mamvi ndiyo kazi yake ya siku nyingi na yaweza kuwa kawahakikishia wataendelea kuyaleta akiwa mkulu wa nji. na hawa ni wale maaskofu uchwara. namaanisha wa kupigiwa kura kama wanasiasa.
 
Huyu anayejiita Mzee wa Upako ni kibaraka tu na mtumwa wa fedha za mafisadi, nyie mnaosali kwake mumchunguze asije akawafanyia ya Kibwetere.
 
Mzee wa upako amejitokeza hadharani na kuishambulia CCM na viongozi wake,
  • Amesema maendeleo ya CCM ndani ya miaka 50 ni sawa yapo mbali sana na kuyafananisha na mtu mzima kuvaa nepi.
  • Amesema CCM imekuwa inalindwa na vombo vya dola na usalama wa taifa ndio unaohusika na kuiweka madarakani!
  • Amesema bila watu wa usalama wa taifa mtu hawazi kushinda!
Source : Gazeti Nyakati leo

Miezi iliyopita mzee wa upako alihubili kanisani kwake akisema kuwa viongozi wa juu CCM wana viroboto kichani na kwamba wasipobadilika muda mfupi ujao atawaroga!

Watafiti wa mambo ya kisiasa wanasema mzee wa upako amekuwa kampeni manaja wa rais kikwete katika uchaguzi wa mwaka 2010 lakini baada ya dhana ya kujivua gamba yeye alimshauli kikwete asifanye hivyo lakini hawakukubaliana.

Kutokana na mgogoro huo mzee wa upako akaamua kumuunga mkono Lowassa na sasa yupo kambi ya Lowassa. Kambi ya Lowassa inamhusu askof Thomas Laizer, Askof Mgullu Kilimba, askofu Mokiwa na wengine

Mpaka sasa Lowassa amefanikiwa kupata mtandao ndani ya makanisa kupitia viongozi hawa wa dini.

Ziara za Lowassa makanisani zinaendelea na wiki hii alipanga kwenda mkoa wa Mara lakini wana CCM wamepiga kelele na ziara yake kuahirisha ambapo itaendeshwa na mh. Kabaka .

Ukweli ni kwamba baadhi ya wachungaji wanapokea pesa za anasiasa kwa maslahi ya uchaguzi 2015.
......MZEE WA UPAKO, kigeugeu, anamgeukia Kikwete kigeugeu, .......alisema Kikwete ni chaguo la Mungu, ooh, huyu jamaa kigeugeu....
 
Maaskofu wengine bwana!

Well, ana uhuru wa kutoa maoni yake lakini sidhani presentation ya hivi inastahili kuwakilishwa na ASKOFU.
Hana uaskofu wowote wala upako hana. ana matatizo makubwa huyu jamaa. kama mtu anabisha aje tu hapa maeneo ya kibangu. anamung'unya sadaka kwa kuwaongopea watu eti atawaombea wapate magari!
 
Hana lake jambo. Askofu uchwara. Sadaka zimepungua kanisani, hali mbaya, sasa anaanza siasa.
 
Jana nimeangalia kipindi cha mzee wa upako naona ameanza kampeni za kuonesha kuwa wanawake hawapaswi kupewa madaraka makubwa maana amesema wanawake wana roho mbaya na hata sehemu za kazi ambazo mabosi ni wanawake kuna unyanyasaji wa wafanyakazi kwa kiwango cha juu saana ukilinganisha na sehemu ambazo mabosi ni wanaume. Hebu wafanyakazi wa bunge tupeni ya Mama Spika.
 
huyu mzee wa upako ni kigeugueu halisi,upako na kurogana wapi na wapi
kama sio uchawi wa kinegiria? akivua pete hawezi kuponya huyu kama sio kweli avue tumwone akiponya
hana toafuti na hawa
Raila Kigeugeu - YouTube
 
kumbe anaongea hayo kwasababu alipingana na Kikwete kuhusu kujivua gamba! Hana mpango wala nini. Nalog off
 
Wale wale,anafikiria namna ya kupanua biashara zake
Mara aishambulie serikali mara amsifie JK
 
Nchi inaelekea wapi mara Bakwata na Sasa maaskofu uchwara nao wanakuwa wanasiasa aibu gani hii nyie mnaotumia viongozi wa dini kwa ajli ya kutaka madaraka
 
Back
Top Bottom