Mzee wa Upako aishukia serikali

Mbinguni kutakuwa na Mchanganyiko wa Wakatoliki, Walutheri, Wasabato, Walokole,Waanglikana, wa TAG, wa EAGT nk provided that wameyashika na Kuyaishi Maisha ya Kikristo

Jehanam kutakuwa na Mchanganyiko wa Wakatoliki, Walutheri, Wasabato, Walokole,Waanglikana, wa TAG, wa EAGT nk provided that hawakuyashika na Kuyaishi Mafundisho ya Yesu

Biblia inasema watu wataangamia kwa Kukosa Maarifa, Maarifa ya kwenda Mbinguni ni Kumtumikia Mungu kwa Moyo wako wote, kumpenda jirani yako kama unavyojipenda wewe, Kuwanyia/kutowanyia wengine mambo ambayo wewe ungependa/usingependa wakufanyie/wasikufanyie

Kukaa hapa na Kupoteza Muda wa Kubishana lipi ni kanisa na lipi si kanisa la Kistro inaonyesha ni jisni gani tulivyofilisika na namna gani tusivyojua ABC za kuurithi Ufamle wa Mungu Yohana Mtakatifu 14:6 na kuendelea!

Tusipokuwa makini Yesu atatukuta tukiwa bize kutafuta ukweli wa lipi ni kanisa lake

Mtakatifu paulo na Anasema dini iliyo ya Kweli ni kwenda kuwatazama wagonjwa nk, yaani kufanya Matendo ya Upendo kwa Wenzetu

Ndugu zangu ili muweze kuurithi Ufalme wa Mungu ni Lazima mpendane kama Yesu alivyotupenda, kama Mungu alivyotupenda hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila amwamiaye asipotee bali apate uzima wa milele

Mtakatifu Paulo anasisitiza juu ya Upendo, anasema kwama Hata nikinena kwa Lugha za Wanadamu na Malaika kama sina Upendo mimi si kitu kabisa na sifai Mbele za Bwana, hata nikiwa na Imani ya Kuhamisha Milima kama sina Upendo mimi si kitu na sifai Mbele za Bwana.

Ndugu zangu katika Kristo ikibidi hata Tuwachallenge Viongozi wetu wa Kanisa ambako wanahamisha sana juu ya Utoaji je Wanawakumbuka Vipi Ndugu zetu katika Kristo wanaoteseka Kilosa kwa Mafuriko? Au wao kuomba Utukufu kwa Serikali za Kibinadamu ndiyo Kipaumbele? Wana JF wenzangu wapendwa katika Kristu je Tumehamasika vipi kuchangia Wahanga wa Mafuriko ya Kilosa au tunakesha hapa tukishabia hizi lebbel zetu za Ukatoliki, Ulokole n.k Je Bwana Yesu anapendezwa nasi?

Tujichunguze Ndugu zangu tuone ni kwa namna tunatekeleza yale aliyotuagiza Bwana wetu Yesu Kristo, Yesu aliwafariji Wagonjwa hata Wafiwa yatupasa kufanya hivyo ili tuweze kuurithi Ufalme ambao tumeahidiwa katika Ile Sura ya 14:2-4 ya Injili ya Mtakatifu Yohane

Mwisho: Changia wahanga wa Mafuriko Kilosa ili Tuonyeshe Upendo ambao Bwana wetu Yesu Kristo amekuwa akiuhubiri katika miaka yake 33 ambayo aliishi katika hii Dunia

Tumsifu Yesu Kristo, Milele Amina
 
Achana na Hii Thread

Njoo huku

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ia-zaidi-ya-watanzania-1-200-wamechangia.html

Hata Yesu na Malaika zake watafurahi maana utakuwa unatimiza/unafanya Jambo ambalo Yesu amekuwa akilisisitiza

Acha Kuwapigania akina Lusekelo, Pengo, Kakobe wao wako huko wankula Kuku kwa mrija kwa kutumia michango tunayotoa.

Njoo huku

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ia-zaidi-ya-watanzania-1-200-wamechangia.html

Weka Mgomo kutoa Sadaka Kanisani au Msiktini na Uwatolee hawa Wahitaji

Yesu alisema Msipowapenda Jirani zenu ambao mnaishi nao kila siku na kuwaona utakuwa ni UNAFIKI kusema tunampenda Mungu ambaye hata hatujawahi Kumwona. Mpende Mungu wako kwa kutumia hawa wa Kilosa walio Sura na Mfano wake yeye

Kwa Mara nyingine Yesu anakuita

Huku
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/49373-harambee-saidia-wahanga-wa-mafuriko-tanzania-zaidi-ya-watanzania-1-200-wamechangia.html

Kristu ndiye Tumaini letu
 
It's amazing what some people will do in the name of imported spiritual garbage.
 
Ndugu Waberoya,
Tafadhali, unaweza kufafanua hapo kwanini Lusekelo aliogopa? (ref red font)

Si kwa ubaya, Kulola na Lazaro ndio fathers wa makanisa ya kilokole, Lusekelo akisema jambo negative kwa hawa tu, waumini watamkimbia!!! aha aha aha, kwani hana akili? ndiyo nika challenge kuwa naye Kulola anapata attention ya serikali, data tunazo, na inajulikana yet Lusekelo hakumwona akawataja wengine! anaheshimiwa sana

Nadhani ukiwa high school na vyuo is even worse.But believe me I have been born again christian for 8 yrs, na moja ya vitu ambavyo wachungaji wanahimiza ni watu kunodokana na hizo tabia. Ni makosa from bible point of view, na wote wanaofanya hivyo, huwa tunawachukulia ni wachanga au ujinga, wa kutoelewa neno la Mungu, wakifundishwa baadae hubadilika.

kisaokolojia unapomtenga mtu ni alama ya kujikweza kwani unajiamini wewe ni mtakatifu sana, wakati in the sight of God we are all equally, tofauti yetu ni zile priveleges tunazopata kutokana na kuacha tabia fulani mbaya.

I repeat your concern is valid those people are wrong, lakini kumbuka sio wote. wazazi wangu mimi wakatoliki, marafiki wengi walutheri, wadogo zangu wakatoliki na lutheri, can I possibly excommunicate them simply by the name of Jesus??? definitely not!

Ukiwaona ujue hawajajua bado maandiko...
 

Message received,

stay blessed,

Thanks.
 
Hawa wagawa upako nao mara nyingine mtihani. Wanalazimisha uheshimiwa badala ya kufanya kazi vizuri ili matokeo ya kazi zao ziwajengee uheshimiwa. Mi na shaka sana na hawa self made bishops. Credetials zao zinatakiwa kufanyiwa tafiti vinginevyo watulie wakisali huko makanisani mwao.
 

MATAYO 10:34 'MSIDHANI NIMEKUJA KULETA AMANI DUNIANI LA! SIKUJA KULETA AMANI BALI UPANGA 35 KWA MAANA NALIKUJA KUMFITINI MTU NA BABAYE, NA BINTI NA MAMAYE, NA MKWE NA MKWE MTU 36 NA ADUI ZA MTU NI WALE WA NYUMBANI MWAKE 37 APENDAE BABA AU MAMA KULIKO MIMI, HANISTAHILI, WALA APENDAE MWANA AU BINTI HANISTAHILI,WALA MTU ASIECHUKUA MSALABA WAKE AKANIFUATA HANISTAHILI 39 MWENYE KUIONA NAFSI YAKE ATAIPOTEZA, NAE MWENYE KUIPOTEZA NAFSI YAKE KWA AJILI YANGU ATAIONA' --Kweli waweza kuwa ndani ya wokovu kwa miaka nane au hata ishirini ukiwa na utapiamlo wa kiroho(spiritual amnesia). Mtoto wa mwezi anyweshae maziwa yasiyoghoshiwa ana afya kiroho kukuzidi mbali!!

**ATTENTION P/SE -THE MASSAGE HAS BEEN SENT BY PEASANT, AND QUOTED WITH WABEROYA
 
Hii ndio historia sahihi ya mgawanyiko huu wa Wakristo. Kanisa Katoliki mpaka leo leo limakiri kuwa Martin Luther alikuwa na hoja za msingi na ndio maana baadaye zikafanyika juhudi za kurekebisha mambo kadhaa wa kadha kupitia Mitaguso mikuu. Hata hivyo yeye mwenyewe huko alikokwenda yaaliyaparaganya ndio maana wakatokea akina Calvin.

Very true

Hizo sehemu nilizo highlight kwenye blue na red ndio tatizo nitaji nukuu hapo chini

Huu sasa ndio ukweli wenyewe. Anayebisha kuhusu hili ana personal grudge na kanisa Katoliki kwa sababu tu aliyejitoa huko alimlisha maneno ya kuhalalisha kuondoka
 
Wewe ni wa kuonea huruma hujayaelewa maandiko hayo. Yesu kusema kwamba hakuja kuleta amani bali upanga hakumaanisha waamini (wafuasi wake) wawatenge wale wasioamini au wawachukie. Alimaanisha kwamba wafuasi wake watatendwa vibaya na wasioamini. Kumbe wawe tayari kuteseka kama Yeye alivyoteseka. Wasitetereke katika imani. Kumbe ukosefu wa amani ulitegemewa uletwe na wasioamini, na siyo kinyume chake.
 
 


.
NI KWELI KABISA KWAMBA UKOSEFU WA AMAANI ULITEGEMEWA ULETWE NA WASIIOAMINI. Hakuna waliowahi kuwakosesha amani wafuasi wa kweli wa Kristo na kiwaua kama lilivyofanya kanisa la RC. Ukisoma historia ya Shumaker CLORIOS REFORMATION unakuta kanisha la Rc limewaua mashahidi wa Kristo walioorodheshwa milioni sitini na nane Note Shumaker ni mkatolic. Pia ukisoma historia huru kabisa ya Dean A Peterson kitabu cha kwanza na cha pili utakuta jinsi Rc iliwachinja mamilioni ya mashahidi wa Kristo bila huruma. Mabaraza yao ya Inguisition yamefanya ukatili usiomithilika. Mauaji haya yaliyokuwa yalipate kanisa la Kristo mbeleni Yesu aliyazungumzia kwa kumwonyesha Yahana mtume wake. Ufun 6:7 kwenye mhuri wa kwanza mpaka wa nne. Mauaji haya yaliwahusisha pia wayahudi na tulimshuhudia papa paulo wa pili mwaka 1999 akiwaomba radhi wayahudi kwa mauaji waliyowafanyia. Ila cha msingi ambacho papa paulo wa pili hakuelewa ni kwamba sio mtu aliua kama mtu bali fundisho la RC ndilo lililosababishia mauaji haya ya halaiki kuu. Sasa alichopaswa kufanya ni kuyafutilia mbali makanuni ya imani ya Rc yaliyo kinyume na biblia. Kufanya hivyo kungeepusha mauaji mengine yanayoweza tokea. Lakini haiwezekani neno la Mungu lisitende kusudi lake. Zitakuwepo kwa vita ya hermagedon
 
Wasalaam!
Mchango wangu kwa mzee wa upako ni kwamba, kwa ufupi huwa nabarikiwa sana na vipindi vyake maana pamoja na kuonekana anapiga porojo sana lakini kama ni mtu makini na wa kujifunza lazima utaondoka na kitu. Tatizo ni kwamba watu hawajui kwamba, NO BODY IS PERFECT UNDER THE SUN(EXCEPT JESUS ONLY) hivyo Mzee wa Upako anaweza kosea lakini ni mapungufu ya kibinadam kama binadam wengine wanavyokosea.
Nafikiri kinachotakiwa ni kwamba mzee wa upako anatakiwa kujua watu anaoongea nao wengine ni wachanga kiroho na wengine ni wazima kiroho hivo ajaribu kubalance wakati anahubiri otherwise utakuta wanaolalamika wengi ni wale wachanga maana hawamuelewi vyema jinsi anavyohubiri , inakuwa kama anawachanganya .
Ukweli ni kwamba Lusekelo anahubiri kwa namna ambayo wale wenye ukomavu wa maswala ya kiroho tu ndo watakaomwelewa vyema anamanisha nini.
Kwa sisi tunaomuelewa mzee wa upako tunafaidi mengi sana mtu asikwambie.

Thanks in advance!!!

Contacts zeepipo@yahoo.com
 

Ndg yangu wacha dharau kama alivyosema Mzee wa upako! Nina hakika wewe unakwenda kanisani kama ulivyo sema Jumapili wala huna shida ya kulisoma neno la Mungu na kupata maarifa ya kiroho.
Cha msingi hapa Mzee wa upako yuko sawa kwa sababu watu kama wewe hamtambui huduma inayofanywa na hawa wahubiri. Maana injili inahitajika ifike kote ulimwenguni na hopo ndipo mwisho utakapo fika. Hivyo hizo zote ni huduma iwe chini ya mti ua barabarani kwenye magari lazima watu wapewe neno. Hivyo hawa watumishi wanahitaji msaada pia wa serikali maana wanahubiri amani upendo na kuacha kufanya uovu. Mbona serikali inaweka jeshi polisi na etc.Serikali ya USA inatoa msaada kupitia hizi huduma. Bila shaka umenielewa ndugu yangu.
Hizi huduma zitambuliwe bila ubaguzi na kusaidiwa.
 

Ina maana basi Kanisa la RC liko kinyume na mafundisho ya Biblia?? Basi mwenye macho haambiwi tazama ataona mwenyewe ukweli uko wazi,na mapambano bado ni yale yale!
Ya Kaisari mwachie Kaisari na ya Mungui mpe Mungu!!!!!!!!!!!!
 

nikweli ww unamwelewa vzuri na unatoka na kitu kwa maana unapenda porojo kama ulivyosema ila ufalme wa mungu sio porojo na kuwakashifu wenzako na kuwatukana awajui kuhubiri na kujisifu na kujipa majina ya ajabu ajabu hayo sio mambo waumini wanayaitaji ili waende mbinguni funguka acha ushabiki wa wahubiri tafuta mchungaji wa kweli na sio wa mshahara barikiwa
 
  1. Naombeni cv yake.
  2. Makinisa ya vichochoroni ni Lutherani/Katoliki maana yapo hadi Kilimasera, Idodi, Sumve, Kibondo, Paramawe...
  3. Baada ya muda nitakuwa askofu wa kanisa langu na nitaomba passport ya kidiplomasia. Ameen.
 
Kwani naye mzee wa upako anaweza kujiita ana kanisa ,hilo si kanisa bali ni kijiwe cha watu waliokwaza na msongo wa maisha
 

Heshima kwako Mtumishi wetu,

Mkuu umesoma post yangu vizuri au umekimbilia keyboard !
 
Kwa hili Mh. Lusekelo umechemka. Yesu mwenyewe unayedai kuendeleza mafundisho yake alisema kwamba; ufalme wake siyo wa wadunia hii. Kama hivyo ndivyo, inakuwaje basi mh. Lusekelo ajiangaishe na sifa za hapa duniani! katika matahyo 18:4 Yesu alisema ya kuwa yeyote ajinyenyekezaye kama mtoto mdogo huyo ndiye mkuu katika ufalme wa mbinguni. Kuhusu heshima wanayopewa viongozi wa madhehebu ya katiliki na Lutheran, Mh. Lusekelo hana budi kujua kwamba kwa vigezo vya ufalme wa duniani, heshima ya mtu inategemea wafuasi walio nyuma yake. na hivyo, kwakuwa dhehebu lake lina wafuasi kiduchu haingii akilini anavyoweza kudhubutu kujilinganisha na madhehebu hayo kongwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…