Mimi nadhani asilimia kubwa sana ya watanzania wamechoshwa sana na mwenendo na jinsi inchi inavyoendelea. Wakati ambao uongozi wa nchi ukiwa haueleweki, wanasiasa na viongozi wakicheza mchezo tusioujua, wimbi la ukame na ugumu wa maisha unazidi kuwakumba wakazi wake.
Nadhani watanzania wengi hawapendi hali hii.. Kama kungekuwa na uwajibikaji wa kweli, wananchi wangefunguka.
sidhani kama kuna kuna mwana JF, mwenye akili timam ambaye anapendelea hali ya nchi yake.. Kila anayejitokeza kuunga mkono Uozo huu wa uongozi nchini, LAZIMA awe ananufaika kwa namna moja au nyingine na uongozi uliopo.
Sasa pale ambapo mrija UKIKATWA, lazima alipuke na kukigeukia chama chake, na ubaya wake huwa sio siri tena, na sumu yake mbaya sana.