Mzee wa upako aiita serikali na CCM 'washenzi'

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,679
7,242
Nipo live kwenye kanisa la Mzee wa Upako hapa Kibangu, haya ni machache aliyoyasema leo.Alianza kama utani, akikemea tabia ya watznzania kupenda misaada katika kujenga makanisa badala ya kutoa sadaka ili makanisa yajengwe.

Baadae akasema ana mtoto mdogo anaitwa Elshadai ana mwaka mmoja akauliza miaka 30 ijayo ataikuta Tanzania ipo salama?
Mwishowe akasema CCM na Serikali ni Chama cha washenzi na wamejaa ushenzi. Hatuwezi kuongozwa na wahuni waliojaa viroboto kichwani.

Akasema ni kwa nini ndege ya jeshi ije uwanja wa ndege usiku ibebe wanyama alafu kina Pinda wamekaa kwenye nafasi zao bila kuwekwa ndani. Amesema Pinda na serikali nzima wanapaswa kukaa pembeni.

Amesema atawaroga na hawaogopi. Atawaroga kwa sababu CCM na serikali imejaa washenzi, wapumbavu.
Akasema nchi imejaa rushwa na ndio maana watu wa Zanzibar wamekufa. Amesema hata rais kutoa pole ni unafiki tu kwa sababu waliozembea wote walipaswa kuwekwa ndani.

Haogopi mtu na ameshangaa ni kwa nini CCM hiyo hiyo imwite Rostam Gamba, Rostam aachane na siasa uchwara alafu Rostam huyo huyo ampigie debe mgombea Igunga, Rostam ana midomo ningapi? Amesema sisi watanzania tumerogwa na CCM kwakuwa sio wazima.

Anasema hakatai kuna maendeleo lakini maendeleo hayalingani na raslimali. Anasema Nepi ni nguo lakini akivaa mtu mzima si ni kituko? Sasa Tanzania imevaa nepi. Anasema hapigi siasa kwakuwa jambo hilo linagusa maslahi ya watu.

Amewaagiza watu wa usalama wa taifa waliopo kanisani wakawaambie viongozi wao kuwa wasipojirekebisha ndani ya siku saba atawaroga. Amekasirishwa sana na kuuzwa kwa wanyama hai na kuzama kwa meli Zanzibar.

Anasema CCM ni chama kilichoiharibu Tanzania. Nyumba walizouziana za serikali wazirudishe, wasiandike urithi kwa watoto wao. Amewaagiza wanajeshi kuwa anaapa kuwa uamuzi wa kuuza nyumba ulikuwa uamuzi wa kishetani na wajiandae ipo siku zitarudi.

Wakati wote akizungumza hayo watu wote walikuwepo ndani ya kanisa walikuwa wanalipuka kwa kushangiklia. Anasema nchi hii ni kama mwanamke asiye na mwenyewe anayeingiliwa kwa zamu na kila mwanaume
 

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,899
3,390
mkuu kama ni k weli basi naamini binadam anabadilika,huyu mzee wa upako alikuwa supporte mzuri ma magamba,sasa inakuwaje??una uhakika na hayo maneno kwamba yalitamkwa na yeye?
 

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,679
7,242
mkuu kama ni k weli basi naamini binadam anabadilika,huyu mzee wa upako alikuwa supporte mzuri ma magamba,sasa inakuwaje??una uhakika na hayo maneno kwamba yalitamkwa na yeye?

Mkuu mimi nipo Ibadani aliyoyasema mengine ni makali zaidi speed yangu ya kuandika kwa kutumia cm ilikuwa haiendani na maneno yake. Hata mke wake wnayetangaza TBC alikuwa akirukaruka kwa shangwe kila mume wake anapoteremsha nyundo
 

Shomari

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,113
239
ama kweli kwenye Janga la kitaifa lazima tuunganishe nguvu pamoja bila kujali itikadi zetu.
 

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,679
7,242
Hiyo sentensi yake ya mwisho! du!

Alikuwa anamaanisha kila mtu anayepata nafasi ya kuiibia tanzania anaiba bila woga, na aliota ndoto kuwa kulikuwa na mwanamke aliyekuwa akimwita mama akaona anaingiliwa hovyo. Ndo akasema Tanzania ni mama yake na amesisitiza atawaroga wote wanaoshiriki kuifisidi hii nchi.
 

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
4,968
7,995
Mzee bado unaingia makanisa ya hao matapeli? Mchungaji ana gari la mil. 200 halafu kuna waumini wake wanakosa nauli ya kutoka buguruni to ubungo! I think kabla hajawanyoshea kidole ccm ajichek kwanza mwenyewe! Halaf mkuu inaonyesha haupo siriazi na ibada, yaani unajamiiforuming inside the ibada! Huyo mchungaji wako anafikiri kwa kutumia masanilo!!!
 

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,489
907
Mimi nadhani asilimia kubwa sana ya watanzania wamechoshwa sana na mwenendo na jinsi inchi inavyoendelea. Wakati ambao uongozi wa nchi ukiwa haueleweki, wanasiasa na viongozi wakicheza mchezo tusioujua, wimbi la ukame na ugumu wa maisha unazidi kuwakumba wakazi wake.

Nadhani watanzania wengi hawapendi hali hii.. Kama kungekuwa na uwajibikaji wa kweli, wananchi wangefunguka.

sidhani kama kuna kuna mwana JF, mwenye akili timam ambaye anapendelea hali ya nchi yake.. Kila anayejitokeza kuunga mkono Uozo huu wa uongozi nchini, LAZIMA awe ananufaika kwa namna moja au nyingine na uongozi uliopo.

Sasa pale ambapo mrija UKIKATWA, lazima alipuke na kukigeukia chama chake, na ubaya wake huwa sio siri tena, na sumu yake mbaya sana.
 

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,424
1,029
....Ni haki yake kutoa maoni yake Binafsi kulingana na Ibara ya 18 ya Katiba yetu. Sioni tatizo. Isipokuwa sijaelewa anaposema ATAWAROGA alikuwa anamaanisha nini, ukizingatia huyu ni Kiongozi wa Dini.
 

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,679
7,242
Mzee bado unaingia makanisa ya hao matapeli? Mchungaji ana gari la mil. 200 halafu kuna waumini wake wanakosa nauli ya kutoka buguruni to ubungo! I think kabla hajawanyoshea kidole ccm ajichek kwanza mwenyewe!

Halaf mkuu inaonyesha haupo siriazi na ibada, yaani unajamiiforuming inside the ibada! Huyo mchungaji wako anafikiri kwa kutumia masanilo!!!

Mimi nipo kazini broda, au ulitaka niende masjid gani?
 

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,679
7,242
....Ni haki yake kutoa maoni yake Binafsi kulingana na Ibara ya 18 ya Katiba yetu. Sioni tatizo. Isipokuwa sijaelewa anaposema ATAWAROGA alikuwa anamaanisha nini, ukizingatia huyu ni Kiongozi wa Dini.</font></b>

Hata mimi mwanzoni nilishtuka lakini alirudia neno kuroga zaidi ya mara 5 baadae akafafanua kuwa maombi yake dhidi ya wanaodhulum nchi ni sawa na kuroga tu
 

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
6,786
1,633
Hata mimi mwanzoni nilishtuka lakini alirudia neno kuroga zaidi ya mara 5 baadae akafafanua kuwa maombi yake dhidi ya wanaodhulum nchi ni sawa na kuroga tu

MAOMBI NI KWA MUNGU NA KUROGA NI KWA SHETANI, ye aseme waziwazi kw miujiza yake inahusika na nguvu za giza
 

Sabung'ori

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
2,130
1,107
mkuu kama ni k weli basi naamini binadam anabadilika,huyu mzee wa upako alikuwa supporte mzuri ma magamba,sasa inakuwaje??una uhakika na hayo maneno kwamba yalitamkwa na yeye?

Director ndugu yangu eaujui!?,iki chama cha magamba ni pepo,sasa huyo mzee wa upako hilo pepo limemtoka hivyo faham zimemrejea.Na wapo wengi tu watafuata kwani hata walewaliotwambia zama-zile kwamba huyo msafiri aka vasco dagama kuwa ni chaguo la God b'shaka wanazijutia nafsi zao OVA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

6 Reactions
Reply
Top Bottom