Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,615
Nipo live kwenye kanisa la Mzee wa Upako hapa Kibangu, haya ni machache aliyoyasema leo.Alianza kama utani, akikemea tabia ya watznzania kupenda misaada katika kujenga makanisa badala ya kutoa sadaka ili makanisa yajengwe.
Baadae akasema ana mtoto mdogo anaitwa Elshadai ana mwaka mmoja akauliza miaka 30 ijayo ataikuta Tanzania ipo salama?
Mwishowe akasema CCM na Serikali ni Chama cha washenzi na wamejaa ushenzi. Hatuwezi kuongozwa na wahuni waliojaa viroboto kichwani.
Akasema ni kwa nini ndege ya jeshi ije uwanja wa ndege usiku ibebe wanyama alafu kina Pinda wamekaa kwenye nafasi zao bila kuwekwa ndani. Amesema Pinda na serikali nzima wanapaswa kukaa pembeni.
Amesema atawaroga na hawaogopi. Atawaroga kwa sababu CCM na serikali imejaa washenzi, wapumbavu.
Akasema nchi imejaa rushwa na ndio maana watu wa Zanzibar wamekufa. Amesema hata rais kutoa pole ni unafiki tu kwa sababu waliozembea wote walipaswa kuwekwa ndani.
Haogopi mtu na ameshangaa ni kwa nini CCM hiyo hiyo imwite Rostam Gamba, Rostam aachane na siasa uchwara alafu Rostam huyo huyo ampigie debe mgombea Igunga, Rostam ana midomo ningapi? Amesema sisi watanzania tumerogwa na CCM kwakuwa sio wazima.
Anasema hakatai kuna maendeleo lakini maendeleo hayalingani na raslimali. Anasema Nepi ni nguo lakini akivaa mtu mzima si ni kituko? Sasa Tanzania imevaa nepi. Anasema hapigi siasa kwakuwa jambo hilo linagusa maslahi ya watu.
Amewaagiza watu wa usalama wa taifa waliopo kanisani wakawaambie viongozi wao kuwa wasipojirekebisha ndani ya siku saba atawaroga. Amekasirishwa sana na kuuzwa kwa wanyama hai na kuzama kwa meli Zanzibar.
Anasema CCM ni chama kilichoiharibu Tanzania. Nyumba walizouziana za serikali wazirudishe, wasiandike urithi kwa watoto wao. Amewaagiza wanajeshi kuwa anaapa kuwa uamuzi wa kuuza nyumba ulikuwa uamuzi wa kishetani na wajiandae ipo siku zitarudi.
Wakati wote akizungumza hayo watu wote walikuwepo ndani ya kanisa walikuwa wanalipuka kwa kushangiklia. Anasema nchi hii ni kama mwanamke asiye na mwenyewe anayeingiliwa kwa zamu na kila mwanaume