johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,965
- 141,969
Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye
Waziri Mkuu Mstaafu mzee Sumaye amesema Bunge la chama kimoja halina afya kwa maendeleo ya nchi na kwamba bunge la namna hiyo huifanya Serikali ilale usingizi.
Sumaye amesema unapoubana upinzani nje ya chama maana yake ni kuwa unakaribisha upinzani ndani ya chama ambao ndio mbaya na hatari zaidi.
Ni lazima CCM iwe na uvumilivu wa kisiasa ili iweze kulikuza taifa letu ambalo kimsingi ni moja.
Chanzo: Star tv