Mzee Mwinyi: Robert Mugabe aliisaidia Tanzania wakati wa shida, ni rafiki wa kwanza wa Tanzania

Maisha yanaenda kasi sana..kwahiyomwe bibi siku hizi mpinzani...mh kweli siku zote teknoloji na mda haudawahi danganya

RIP comrade MUGABE true son of Africa
Kwa hiyo mzee Mwinyi aliyesema hayo ni mpinzani?
 
Mara nyingi huwa nnaikumbusha hotuba ya "mikuki miwili" ya Mzee Mwinyi. Hotuba hiyo aliitoa mwaka tu baada ya kuapishwa Urais.

Hotuba hiyo ndiyo Mzee Mwinyi alifunguka na kusema hazina kaikuta haina kitu kabisa. Kaachiwa nchi haina akiba hata kidogo.

Hotuba hiyo imepotezwa kabisa na aliongea hayo Diamond Jubilee na wazee wa Dar.

Alikuwa kimya kwa hilo muda mrefu sana, naona kaamua kuuweka ukweli (usiopendwa) wazi.
 
Mara nyingi guwa naikumbusha hotuba ya "mikuki miwili" ya Mzee Mwinyi. Hotuba hiyo aliitoa mwaka tu baada ya kuapishwa Urais.

Hotuba hiyo ndiyo Mzee Mwinyi alifunguka na kusema hazina kaikuta haina kitu kabisa. Kaacjiwa nchi haina akiba hata kidogo.

Hotuba hiyo imepotezwa kabisa na aliongea hayo Diamond Jubilee na wazee wa Dar.

Alikuwa kimya kwa hilo muda mrefu sana, naona kaamua kuuweka ukweli (usiopendwa) wazi.
Acha unaaa wewe huwez izima historia ya baba Wa taifa our fore father Nyerere ,ebu nioneshe dar hapa mali yoyote aliyojilimbikizia Nyerere hata moja ama mtoto Wa Nyerere alive kwenye siasa alafu linganisha na Mwinyi unipe jibu ,
 
Hayo yako wewe. Wapi nimeandika kajilimbikizia chochote?

Unaongelea watoto wa Nyerere? Mbona wanasema wanaishi kama "Royal Family", bishana nao, ushahidi huu hapa...

Sikusema Mexico,nimesema New Mexico. New Mexico ni jimbo mojawapo la USA.

Kuhusu hilo jembe,ni quite uncessary, Sisi hapa tunaishi kama Royal Family,kwa ruzuku ya Serikali.
 
Nina uhakika kwa asilimia mia kuwa Mugabe hakuwahi kuisaidia Tanzania hata senti tano. Mugabe kama Mugabe hakuwa na uwezo wowote wa kifedha kusaidia Tanzania. Mzee Mwinyi samahani sana, usidhalilishe taifa letu. Mtu hawezi kuisaidia nchi. Yeye kuidhinisha kutoa msaada wowote ni nchi imetoa na siyo mtu (Mugabe) katia mfukoni make, la hasha.

Hata USAID wanakuandikia kabisa ni msaada wa watu wa Marekani, lakini umeshindwa kuelewa hilo Mzee wangu? Pole sana mzee, mimi nakupinga japo sijawahi kuwa rais wa nchi. Tumia lugha stahiki, angalau basi sema serikali ya Zimbabwe iliamua kutusaidia, lakini siyo mtu aliyetusaidia. Mtu ananufaika na nchi, kamwe hawezi kuisaidia nchi. Na akipata mamlaka hufanya kwa niaba ya nchi na wananchi wote.
Marehemu mzee Nyerere alimwambia Mwinyi nenda kwa Mugabe au alimwambia nenda Zimbabwe ukaombe ombe?
 
hadhara anayotaka kuilenga Mwinyi haipo kwenye YOUTUBE, iko Maneromango na Gezaulole na Tandahimbo ambako hawana cellphone towers, wala smart phones wala access ya news za ndani, achilia mbali za dunia! (kumbuka kuna watu Kagera hawakusikia Morogoro tanker limechoma wachota mafuta, wiki iliyofuata na wenyewe wakachota!)

Wala hawajui Mugabe alishafurushwa, alishakufa, alifanya nini kabla ya kufa, na alishawekwa kwenye jalala la historia.

Mwinyi anatakiwa awafuate hao watu huko aongee nao live jukwaani, ndio watamsoma

Hapa, kwa sababu tuna vyanzo vya mizania mbali mbali ya habari, tunamwona mzee Mwinyi ashapoteza 70% ya brain cells zake kwa uzee, ashakuwa senile, anapalilia ajira ya mwanae kwa ku sapoti kila kinachoamuliwa kama kushusha bendera siku tatu kwa jitu ambalo liliua Wazimbabwe 27,000 kwa sababu wao Ndebele yeye Mshona
 
Uko sahihi kimantiki lakini sio kiuhalisia, kwa hizi katiba zetu rais ndiyo mwenye maamuzi ya kutoa pesa hazina bila ruhusa ya yoyote na asifanywe lolote. Rejea manunuzi ya ndege hapa nchini, je yaliidhinishwa na bunge? Huoni siku hizi hapa kwetu rais anatoa pesa kwenye miradi mbalimbali na inatajwa kuwa yeye ndio katoa, na kuna kejeli fulani kwamba huo mradi kama sio yeye mbona watangulizi wake hawakufanya?
Kwa upande mmoja uko sahihi kuwasahihisha wanaokataa kuwa Mugabe hakutusaidia. Rais ana nguvu kubwa sana ya kuwashawishi viongozi wenzake kufanya jambo. Nitoe mfano wa kimataifa. Ktk miaka ya 1960 na 1970, tulipokuwa na viongozi wa Amerika na Uingereza, ambao 'wanamilki' Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, waliokuwa tayari kuridhia mahitaji ya nchi maskini, viongozi hao waliwezesha IBRD na IMF kuwezesha nchi hizo kifedha kwa masharti nafuu. Ktk miaka ya 80, iliyo'tawaliwa' na Reagan wa Amerika na Thatcher wa Uingereza, ambao walichukia mwelekeo huo, walizifanya IBRD na IMF kuwa chungu kwetu kwa masharti yao magumu. Vivyo hivyo. Viongozi wa India, Zimbabwe na Uganda wa wakati huo waliisaidia Tanzania kipindi kigumu kwa sababu ya mwelekeo na ushawishi wao. Ni nchi zao zilizotoa msaada, ndiyo, lakini ni kwa kuwa viongozi hao walitaka hivyo. Kwa upande wa pili, utaona tayari upande mmoja uko sahihi kuwasahihisha wanaokataa kuwa Mugabe hakutusaidia. Rais ana nguvu kubwa sana ya kuwashawishi viongozi wenzake kufanya jambo. Nitoe mfano wa kimataifa. Ktk miaka ya 1960 na 1970, tulipokuwa na viongozi wa Amerika na Uingereza, ambao 'wanamilki' Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, waliokuwa tayari kuridhia mahitaji ya nchi maskini, viongozi hao waliwezesha IBRD na IMF kuwezesha nchi hizo kifedha kwa masharti nafuu. Ktk miaka ya 80, iliyo'tawaliwa' na Reagan wa Amerika na Thatcher wa Uingereza, ambao walichukia mwelekeo huo, walizifanya IBRD na IMF kuwa chungu kwetu kwa masharti yao magumu. Vivyo hivyo Viongozi wa India, Zimbabwe na Uganda wa wakati huo waliisaidia Tanzania kipindi kigumu kwa sababu ya mwelekeo na ushawishi wao. Ni nchi zao zilizotoa msaada, ndiyo, lakini ni kwa kuwa viongozi hao walitaka hivyo. Kwa upande wa pili, utaona tayari kuwa uwezeshaji wa kiongozi wa nchi fulani namna hii hautegemei yeye kujichukulia madaraka au kuwa na katiba mbovu, hata kama hilo lipo kwa baadhi. Tukirudi kwa mchango wa Mugabe kiujumla, ana mengi mengine makubwa mazuri. Limo hilo la ardhi. Ni yeye hasa aliyehakikisha kuwa suala la ardhi kwa 'wazawa' linakuwa hai. Turejee historia. Ukoloni Zimbabwe uliambatana na unyang'anyi wa ardhi wa kutisha. Si tu kuwa ardhi nzuri ilichukuliwa na wazungu, bali walihakikisha wanachukua juu ya mito (upper part of rivers), kisha wakakata maji (damming) na kuacha mabonde ambako tayari Waafrika walikaa kuwa makame ajabu. Pia si kweli kuwa Wazimbabwe walinyang'anya ardhi yote waliyokuwa nayo Wazungu. Walichukua ardhi isiyotumika, ambayo ilikuwa nyingi tu. Hata hivyo iliwachukua miaka 20 baada ya uhuru kufanya hivyo. Ni hivi: Katiba ya Zimbabwe iliyokubaliwa na Waingereza iliridhia kuchukuliwa kwa ardhi hiyo baada ya miaka 10 ya uhuru kwa Uingereza kuwalipa fidia washika ardhi Wazungu. Uingereza ikakiuka makubaliano hayo mwaka 1990. Wananchi wakakasirika, wakaidai ardhi. Uongozi wa Mugabe ukawaomba wavute subira kwa kuwa itawatisha Wazungu wa Afrika Kusini waliokuwa wanamshikilia Mandela. Wakati huo Mugabe na viongozi wengine wa Kusini na kwingine Afrika walikuwa wanakaribia kukamilisha mpango wa kumtoa Mandela jela. Mugabe alichelea kuwa ardhi ikichukuliwa 1990 Zimbabwe, huenda Wazungu Afrika Kusini wasimtoe Mandela jela. Hayo yote yalipita na miaka mingine 10 zaidi ikapita kabla ya sehemu ya 'ardhi ya Wazungu' Zimbabwe kuchukuliwa. Jambo hili linajulikana wazi Zimbabwe. Linajulikana kidogo tu nje kwa sababu ya nguvu ya propoganda ya Wazungu, wanaomiliki vyombo vyote vya habari vya kimataifa. Ndiyo, utawala wa Mugabe pia ulikanyaga haki za binadamu na kuvuruga chaguzi, na Mugabe alizidisha muda kukaa madarakani, lakini alifanya mengine makubwa mazuri, likiwemo la msaada kwa Tanzania.
 
Nina uhakika kwa asilimia mia kuwa Mugabe hakuwahi kuisaidia Tanzania hata senti tano. Mugabe kama Mugabe hakuwa na uwezo wowote wa kifedha kusaidia Tanzania. Mzee Mwinyi samahani sana, usidhalilishe taifa letu. Mtu hawezi kuisaidia nchi. Yeye kuidhinisha kutoa msaada wowote ni nchi imetoa na siyo mtu (Mugabe) katia mfukoni make, la hasha.

anufaika na nchi, kamwe hawezi kuisaidia nchi. Na akipata mamlaka hufanya kwa nia...
Kwani katiba ya zimbabwe inasemaje kuhusu hili.!?
 
Kwa upande mmoja uko sahihi kuwasahihisha wanaokataa kuwa Mugabe hakutusaidia. Rais ana nguvu kubwa sana ya kuwashawishi viongozi wenzake kufanya jambo. Nitoe mfano wa kimataifa. Ktk miaka ya 1960 na 1970, tulipokuwa na viongozi wa Amerika na Uingereza, ambao 'wanamilki' Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, waliokuwa tayari kuridhia mahitaji ya nchi maskini, viongozi hao waliwezesha IBRD na IMF kuwezesha nchi hizo kifedha kwa masharti nafuu. Ktk miaka ya 80, iliyo'tawaliwa' na Reagan wa Amerika na Thatcher wa Uingereza, ambao walichukia mwelekeo huo, walizifanya IBRD na IMF kuwa chungu kwetu kwa masharti yao magumu. Vivyo hivyo. Viongozi wa India, Zimbabwe na Uganda wa wakati huo waliisaidia Tanzania kipindi kigumu kwa sababu ya mwelekeo na ushawishi wao. Ni nchi zao zilizotoa msaada, ndiyo, lakini ni kwa kuwa viongozi hao walitaka hivyo. Kwa upande wa pili, utaona tayari upande mmoja uko sahihi kuwasahihisha wanaokataa kuwa Mugabe hakutusaidia. Rais ana nguvu kubwa sana ya kuwashawishi viongozi wenzake kufanya jambo. Nitoe mfano wa kimataifa. Ktk miaka ya 1960 na 1970, tulipokuwa na viongozi wa Amerika na Uingereza, ambao 'wanamilki' Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, waliokuwa tayari kuridhia mahitaji ya nchi maskini, viongozi hao waliwezesha IBRD na IMF kuwezesha nchi hizo kifedha kwa masharti nafuu. Ktk miaka ya 80, iliyo'tawaliwa' na Reagan wa Amerika na Thatcher wa Uingereza, ambao walichukia mwelekeo huo, walizifanya IBRD na IMF kuwa chungu kwetu kwa masharti yao magumu. Vivyo hivyo Viongozi wa India, Zimbabwe na Uganda wa wakati huo waliisaidia Tanzania kipindi kigumu kwa sababu ya mwelekeo na ushawishi wao. Ni nchi zao zilizotoa msaada, ndiyo, lakini ni kwa kuwa viongozi hao walitaka hivyo. Kwa upande wa pili, utaona tayari kuwa uwezeshaji wa kiongozi wa nchi fulani namna hii hautegemei yeye kujichukulia madaraka au kuwa na katiba mbovu, hata kama hilo lipo kwa baadhi. Tukirudi kwa mchango wa Mugabe kiujumla, ana mengi mengine makubwa mazuri. Limo hilo la ardhi. Ni yeye hasa aliyehakikisha kuwa suala la ardhi kwa 'wazawa' linakuwa hai. Turejee historia. Ukoloni Zimbabwe uliambatana na unyang'anyi wa ardhi wa kutisha. Si tu kuwa ardhi nzuri ilichukuliwa na wazungu, bali walihakikisha wanachukua juu ya mito (upper part of rivers), kisha wakakata maji (damming) na kuacha mabonde ambako tayari Waafrika walikaa kuwa makame ajabu. Pia si kweli kuwa Wazimbabwe walinyang'anya ardhi yote waliyokuwa nayo Wazungu. Walichukua ardhi isiyotumika, ambayo ilikuwa nyingi tu. Hata hivyo iliwachukua miaka 20 baada ya uhuru kufanya hivyo. Ni hivi: Katiba ya Zimbabwe iliyokubaliwa na Waingereza iliridhia kuchukuliwa kwa ardhi hiyo baada ya miaka 10 ya uhuru kwa Uingereza kuwalipa fidia washika ardhi Wazungu. Uingereza ikakiuka makubaliano hayo mwaka 1990. Wananchi wakakasirika, wakaidai ardhi. Uongozi wa Mugabe ukawaomba wavute subira kwa kuwa itawatisha Wazungu wa Afrika Kusini waliokuwa wanamshikilia Mandela. Wakati huo Mugabe na viongozi wengine wa Kusini na kwingine Afrika walikuwa wanakaribia kukamilisha mpango wa kumtoa Mandela jela. Mugabe alichelea kuwa ardhi ikichukuliwa 1990 Zimbabwe, huenda Wazungu Afrika Kusini wasimtoe Mandela jela. Hayo yote yalipita na miaka mingine 10 zaidi ikapita kabla ya sehemu ya 'ardhi ya Wazungu' Zimbabwe kuchukuliwa. Jambo hili linajulikana wazi Zimbabwe. Linajulikana kidogo tu nje kwa sababu ya nguvu ya propoganda ya Wazungu, wanaomiliki vyombo vyote vya habari vya kimataifa. Ndiyo, utawala wa Mugabe pia ulikanyaga haki za binadamu na kuvuruga chaguzi, na Mugabe alizidisha muda kukaa madarakani, lakini alifanya mengine makubwa mazuri, likiwemo la msaada kwa Tanzania.

Mkuu samahani, nimeshindwa kusoma ulichoandika, sio kwakuwa ni kirefu au kibaya, bali kimejirudia. Ni kama umecopy na kupaste kwa bahati mbaya, huend device unayotumia ina shida. Kisha jitahidi kuweka na paragraph unapokuwa na hadithi ndefu.
 
Back
Top Bottom