Sang'udi
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 8,284
- 19,154
Acha kupotosha Mkuu.Anasahau kuwa wakati huo Mugabe alikua anatumia pesa za Mabeberu wakiokua wamemkabidhi Nchi . Wakati huo Mugabe alikua na muda wa miaka 4 tu madarakani ,na uchumi wa Zimbabwe ulikua imara sana na haikua ni Juhudi zake Huyo Hayati Mugabe kujenga uchumi wa Zimbabwe.
Mugabe Aliikuta Zimbabwe ikiwa na uchumi Mzuri sana ,akawa anachota mapesa na kufanya mambo ya Hovyo mpaka Leo ameiacha nchi hiyo ikiwa na pesa yenye samani sawa karatasi za kuchorea kama sio pampers.
Hata hivyo tunamshukuru kwa jambo hilo zuri kwa nchi yetu japo sisi tulitoa wapiganaji wetu kwa ajili ya kuikomboa nchi hiyo na wakapoteza maisha yao ambayo yanathamani kubwa kuliko kitu chochote.
Hata watu wa Magharibi wenyewe wanakiri kuwa Mugabe baada ya kuingia madarakani miaka 17 ya mwanzo "alileta" (sio aliendeleza) maendeleo na alifanya mambo makubwa sana hasa kwa Watu weusi ambao ndio walikuwa wengi (majority).
Hao ndugu zako wa Magharibi wanakiri kabisa kuwa Mugabe aliifanya Zimbabwe kuwa nchi yenye wasomi wengi kuliko nchi yoyote ya Afrika, hadi Waafrika na nchi nyingine zisizo za Kiafrika wakawa wanaitamani Zimbabwe.
Mugabe pia alisaidia sana raia wake hasa katika ya Sekta ya Afya. Haya yote yapo kwenye vyombo vya habari vya Magharibi kama BBC na vinginevyo. Kasome kabla haujaja kupotosha.
Mugabe amekuja "kuonekana" mzinguaji baada ya kuingilia Maslahi ya Wazungu, hasa Waingereza kwenye miaka ya 2000.
Pia alikuja kuharibu kung'ang'ania madarakani baada ya kushindwa mwaka 2008.
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.