Mzee Mwinyi: Robert Mugabe aliisaidia Tanzania wakati wa shida, ni rafiki wa kwanza wa Tanzania

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,603
2,000

Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa alipoingia madarakani mwaka 1985, ailikuta hazina ya Tanzania ikiwa haina kitu

Hali hiyo ya ukata ilitokana na Tanzania kutumia fedha nyingi wakati wa vita vya Kagera(Tanzania dhidi ya Uganda) na IFM kuisusia Tanzania baada ya Mwalimu Nyerere kukataa masharti yao

Mwinyi asema aliamua kumfuata Mwalimu Nyerere akamuuliza, afanye nini? Nyerere akamwambia Tanzania ina marafiki kadhaa, ikiwemo nchi ya Zimbabwe na India, nenda kaombe msaada

Hayati Robert Mugabe akawa kiongozi wa kwanza kuisaidia Tanzania
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,119
2,000
Anasahau kuwa wakati huo Mugabe alikua anatumia pesa za Mabeberu wakiokua wamemkabidhi Nchi . Wakati huo Mugabe alikua na muda wa miaka 4 tu madarakani ,na uchumi wa Zimbabwe ulikua imara sana na haikua ni Juhudi zake Huyo Hayati Mugabe kujenga uchumi wa Zimbabwe.

Mugabe Aliikuta Zimbabwe ikiwa na uchumi Mzuri sana ,akawa anachota mapesa na kufanya mambo ya Hovyo mpaka Leo ameiacha nchi hiyo ikiwa na pesa yenye samani sawa karatasi za kuchorea kama sio pampers.

Hata hivyo tunamshukuru kwa jambo hilo zuri kwa nchi yetu japo sisi tulitoa wapiganaji wetu kwa ajili ya kuikomboa nchi hiyo na wakapoteza maisha yao ambayo yanathamani kubwa kuliko kitu chochote.
 
prs

JF-Expert Member
Feb 22, 2013
2,642
2,000
Viongozi Africa maajabu hayawezi kuisha, Mugabe ana pesa ya kuisaidia Tz? Au ni iliyokuwa Serikali ya Zimbabwe!

Kila misaada inayotolewa na Nchi za Africa inaenda kwa Majina ya Viongozi badala ya Nchi.
Tabia mbovu kweli hii.. Hasa kwa Tanzania sasa imeshamiri.
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
55,378
2,000
Effect ya kupitia ukoloni hii, akili ishazoea kutawaliwa
Viongozi Africa maajabu hayawezi kuisha, Mugabe ana pesa ya kuisaidia Tz? Au ni iliyokuwa Serikali ya Zimbabwe!

Kila misaada inayotolewa na Nchi za Africa inaenda kwa Majina ya Viongozi badala ya Nchi.
Tabia mbovu kweli hii.. Hasa kwa Tanzania sasa imeshamiri.
 
stinger_bug

JF-Expert Member
Jul 14, 2019
856
1,000
Nina uhakika kwa asilimia mia kuwa Mugabe hakuwahi kuisaidia Tanzania hata senti tano. Mugabe kama Mugabe hakuwa na uwezo wowote wa kifedha kusaidia Tanzania. Mzee Mwinyi samahani sana, usidhalilishe taifa letu. Mtu hawezi kuisaidia nchi. Yeye kuidhinisha kutoa msaada wowote ni nchi imetoa na siyo mtu (Mugabe) katia mfukoni make, la hasha.

Hata USAID wanakuandikia kabisa ni msaada wa watu wa Marekani, lakini umeshindwa kuelewa hilo Mzee wangu? Pole sana mzee, mimi nakupinga japo sijawahi kuwa rais wa nchi. Tumia lugha stahiki, angalau basi sema serikali ya Zimbabwe iliamua kutusaidia, lakini siyo mtu aliyetusaidia. Mtu ananufaika na nchi, kamwe hawezi kuisaidia nchi. Na akipata mamlaka hufanya kwa niaba ya nchi na wananchi wote.
 
Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,777
2,000
Inahuzunisha sana namna ambavyo watu hawapewi sifa zao wakiwa hai baadala yake inasubiriwa wakifa! Smh
 
Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,777
2,000
Anasahau kuwa wakati huo Mugabe alikua anatumia pesa za Mabeberu wakiokua wamemkabidhi Nchi . Wakati huo Mugabe alikua na muda wa miaka 4 tu madarakani ,na uchumi wa Zimbabwe ulikua imara sana na haikua ni Juhudi zake Huyo Hayati Mugabe kujenga uchumi wa Zimbabwe.
Mugabe Aliikuta Zimbabwe ikiwa na uchumi Mzuri sana ,akawa anachota mapesa na kufanya mambo ya Hovyo mpaka Leo ameiacha nchi hiyo ikiwa na pesa yenye samani sawa karatasi za kuchorea kama sio pampers.

Hata hivyo tunamshukuru kwa jambo hilo zuri kwa nchi yetu japo sisi tulitoa wapiganaji wetu kwa ajili ya kuikomboa nchi hiyo na wakapoteza maisha yao ambayo yanathamani kubwa kuliko kitu chochote.
Samani?? Imekuwaje meza au kiti?
 
stinger_bug

JF-Expert Member
Jul 14, 2019
856
1,000
Pamoja na juhudi kubwa za viongozi wetu kujaribu kumpamba Mugabe aonekane mwema, ni wazi kuwa waafrika na watanzania wa sasa siyo wale wa miaka ile. Kwa kiasi kikubwa ni wazi kuwa Mugabe anaongelewa law mabaya yake zaidi ya mazuri (kama yapo) aliyoyafanya. Kuanzia mauaji ya watu zaidi ya 20,000 wa kabila la Wamatebele, kuua demokrasia Zimbabwe, kupora ardhi ya wakulima wazungu waliyokuwa wanamiliki, jambo lililopelekea kuua kabisa uchumi na sarafu ya nchi hiyo maskini. Huyu Mugabe amevuna alichopanda. Viongozi wetu waache kujipendekeza kwa marehemu. Tumwache apumzike kwa amani basi.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,028
2,000
Nina uhakika kwa asilimia mia kuwa Mugabe hakuwahi kuisaidia Tanzania hata senti tano. Mugabe kama Mugabe hakuwa na uwezo wowote wa kifedha kusaidia Tanzania. Mzee Mwinyi samahani sana, usidhalilishe taifa letu. Mtu hawezi kuisaidia nchi. Yeye kuidhinisha kutoa msaada wowote ni nchi imetoa na siyo mtu (Mugabe) katia mfukoni make, la hasha.

Hata USAID wanakuandikia kabisa ni msaada wa watu wa Marekani, lakini umeshindwa kuelewa hilo Mzee wangu? Pole sana mzee, mimi nakupinga japo sijawahi kuwa rais wa nchi. Tumia lugha stahiki, angalau basi sema serikali ya Zimbabwe iliamua kutusaidia, lakini siyo mtu aliyetusaidia. Mtu ananufaika na nchi, kamwe hawezi kuisaidia nchi. Na akipata mamlaka hufanya kwa niaba ya nchi na wananchi wote.

Uko sahihi kimantiki lakini sio kiuhalisia, kwa hizi katiba zetu rais ndiyo mwenye maamuzi ya kutoa pesa hazina bila ruhusa ya yoyote na asifanywe lolote. Rejea manunuzi ya ndege hapa nchini, je yaliidhinishwa na bunge? Huoni siku hizi hapa kwetu rais anatoa pesa kwenye miradi mbalimbali na inatajwa kuwa yeye ndio katoa, na kuna kejeli fulani kwamba huo mradi kama sio yeye mbona watangulizi wake hawakufanya?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom