Mzee Mwinyi aibiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Mwinyi aibiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 10, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,495
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Mzee Mwinyi aibiwa sh milioni 37/-
  • Apanda kizimbani Kisutu kutoa ushahidi wake

  na Happiness Katabazi
  Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi, ameibiwa sh milioni 37.4 na hivyo kulazimika kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutoa ushahidi wake.

  Kwa hatua hiyo, Mzee Mwinyi anafuata nyayo za Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliyepanda kizimbani hivi karibuni kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin.

  Mzee Mwinyi ambaye alipanda kizimbani jana, anadai kuibiwa sh 37,440,000 na Abdallah Nassoro Mzombe (39) ambaye ni wakala wake.
  Mbele ya Hakimu Mkazi, Genivitus Dudu, mshtakiwa huyo, mkazi wa Kinondoni Mkwajuni, anashtakiwa kwa makosa ya kumuibia Mzee Mwinyi kiasi hicho cha kodi ya pango ya nyumba mbili zinazomilikiwa na Rais huyo mstaafu.

  Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ambayo Tanzania Daima Jumatano ina nakala yake, Mzombe anadaiwa kufanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 258 na 273 (b) (e) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Sura ya 16 ya mwaka 2002.

  Siku hiyo ya Agosti 21, mwaka huu, ilidaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, mwaka 2011 na Julai 2012 huko Mikocheni, Mzombe akiwa wakala wa Rais huyo mstaafu, alimwibia sh 17,640,000 ambazo ni pato la kodi ya nyumba yake iliyoko eneo la Mikocheni, wilaya ya Kinondoni.

  Iliendelea kudai kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho Mzombe alimwibia Rais Mwinyi kilikuwa ni kodi ya pango la nyumba namba 481, iliyoko kwenye ploti A huko Mikocheni ya mwaka 2011/2012 na 2012/2013.
  Aidha anadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, mwaka 2011 na Julai 10, mwaka huu huko Msasani Village wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa huyo alimwibia tena Rais huyo mstaafu sh 19,800,000 ambazo zilikuwa ni kodi ya nyumba namba 55 iliyoko kwenye Kitalu C .
  Kiasi hicho cha fedha kilikuwa ni kodi ya pango la nyumba hiyo la mwaka 2011/2012 na 2012/2013.

  Hata hivyo mshtakiwa huyo alikana mashtaka yote na yuko rumande hadi Oktoba 22 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa.
  Rais Mwinyi jana alitua katika mahakama hiyo huku akiongozwa na maofisa Usalama wa Taifa (TISS) kuja kutoa ushahidi katika kesi hiyo ya jinai Na. 201/2012 iliyofunguliwa na serikali dhidi ya wakala wa Mwinyi, Abdallah Nassoro Mzombe (39).

  Kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa, Mwinyi alihifadhiwa kwa muda kwenye chumba namba moja cha mahakama hiyo ili kutoa muda kwa wakili wa serikali, Charles Anindo, kumuandaa.

  Waandishi wa habari waliokuwepo mahakamani hapo kwa ajili ya kuripoti kesi hiyo, walizuiliwa kuingia, jambo ambalo lililalamikiwa vikali na wana habari hao.

  "Msiingie humu ndani haiwahusu," alisema ofisa habari mmoja, akiwazuia waandishi kuingia ndani ya mahakama hiyo.

  Mzee Mwinyi aliondoka katika viwanja vya mahakama hiyo majira ya saa 6:21 mchana na kisha kupanda gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 914 BJT.
  Hati ya mashtaka ya kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo Agosti 21 mwaka huu.
  Mei 7 mwaka huu Rais Mkapa alifika mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Elvin Mugeta, kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, na Grace Martin. Mahalu aliachiwa huru katika kesi hiyo.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu mzee ana nyumba ngapi alizopangisha? Na je, kama raia wa kawaida analipa kodi ya mapato ya nyumba za kupangisha? TRA mpo?
   
 3. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Acha naye alizwe maana aliwaliza watanzania na kuanzisha mfumo wa kifisadi unaotusumbua. Nikikumbuka yeye na Muhuni Muhiddin Ndolanga walivyouza Loliondo kwa Brig. Ali natamani ninywe damu ya hiki kibabu kinafiki na kijizi.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi, is there any way we can kick out these Arabs from Loliondo when Tanzania is finally liberated from these fisadis?
  Ni aibu.
   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Jasusi worry not time is coming to kick their asses.
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Bado natafakari jinsi huyu kijana eti anadaiwa KUMUIBIA Mzee Mwinyi!!!............halafu jamaa yuko rumande!!!..........Wakala kamuibia Mteja wake!!....halafu Mteja mwenyewe Rais Mstaafu wa URT!!!.........

  .......hii inanikumbusha kisa cha Batenga na JKN............
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  I find this to be really ridiculously stupid..kama ni kodi yetu wavujajasho ndio inayoendesha hiyo mahakama ni haki yetu kujua kilichojiri, hivo si haki kuzuia wanahabari kuingia na kutujuza kilichojiri. nadhani hawa satanists magamba wamelewa madaraka na kudhani hii nchi ni yao peke yao na vizazi vyao.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tusimulie basi kisa cha Batenga. Wengine hatukuwepo. Lakini hii si mara ya kwanza Mzee Mwinyi anaingizwa mjini. Alipokuwa anamaliza muhula wake pale Ikulu, aliondoka na baadhi ya fenicha na mfanyikazi wake mmoja naye akaondoka na baadhi ya mali zake. Alishindwa kumfungulia mashtaka.
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  .......Mheshimiwa Mzee Jasusi......heshima mbele.....ilkuwaje hii ilikupita!!?
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jasusi, maswali yanayofatia : 1. Nyumba ilianza kupangishwa tangu lini? 2. Kodi ya mapato imeanza kutolewa tangu lini?
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Surprise surprise,

  Mbowe anasema anataka utawala wa sheria. Naona washabiki wake hamtaki sheria.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,495
  Trophy Points: 280
  Swali la nyongeza Steve Dii: Je, kuna nyumba nyingine zaidi ya hii ambayo Mwinyi anapangisha!? kama (z)ipo, (z)ipo katika mji/miji ipi?

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Aliibiwa matofali
   
 14. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  KODI HAKULIPA NA WALA PROPERTY TAX SIJUI KAMA LAIPA. halafu pesa hizo kazitoa wapi kujengea nyumba za kumpatia kodi kubwa hivyo? hawa ndio waliokuwa wnatuhubiria pesa si msingi wa maendeleo , ona leo wanavytapanya mapesssa!
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  kwi!kwiiiii! Na nani?
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  Nadhani makamba jr ndo aliwahi kutoa hoja ya kurasimisha upangaji nyumba ili watu walipe kodi. Sidhani kama kuna mfumo wa kutoza kodi kwa upangishaji nyumba kwa mtu binafsi, since sheria ya kodi inabana kampuni na sio account za akiba za watu binafsi.
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa vipi? Sote tunataka utawala wa sheria na haki. Kama una mradi wa nyumba za kupangisha na unalipia kodi hamna neno. Lakini nahisi hapa Mwinyi alitumia cheo chake (kinyume na kanuni za CCM) kujipatia nyumba za kupangisha.
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Mwinyi ameibiwa na dalali?kama alimzoesha dalali afanye atakalo,mwishoni ndio pesa iingie banki lazima amuibie maana ana mapesa mengi tena mengi ameiibia serikali na sisi walalahoi kodi zetu,acha zirudi kidogo kwa walalahoi aliowaibia!kwa nini asitumie real estate agents?*natumia dalali wa mtaani?inawezekana ni ndugu yake pia!
   
 19. StayReal

  StayReal JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 519
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yes there is way, kwanza tukomboe nchi utaona wengine wanakimbia wenyewe!!!
   
 20. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wacha mafisadi nao waibiwe, huyo jamaa aliyeiba mi na-mwona ana akili sana kwa sababu ameiba kwa walionazo kuliko kwenda kuwaibia walala hoi. Hima hima majambazi, msiumize walala hoi. Wafuateni mafisadi, mkifanikiwa mara moja tu kumwibia fisadi, unastaafu na huo ujambazi. Maana mkupuo mmoja tu ni wa kutosha.

  Na huyo tusimwite mwizi, ni mwananchi anayechukua kilichoibwa kwa wananchi.
   
Loading...