MZEE Mustafa Jaffer Sabodo achangia tena M4C (CHADEMA) na ahadi zingine za miradi

[h=3][/h]



    • sabodo.jpg
    • 0000001asabodo.jpg
    attachment.php



Sina ugomvi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wala mpenzi wake mpya Mustafa Jafary Sabodo. Nina ugomvi na staili ya Sabodo ya 'kukisaidia' Chadema. Kila akijisikia kupata publicity, huwaita viongozi wa Chadema na kuwapa milioni kadhaa za shilingi. Sijajua ni kwanini Chadema hawataki kujua historia ya 'utajiri' wa Sabodo anayejinasibu kama mjamaa aliyekuwa karibu na baba wa taifa Mwl Julius Nyerere. Kwa wanaojua ushupavu na uwazi wa Mwalimu wanashangaa ni kwanini uhusiano wao na Sabodo umekuwa maarufu baada ya kifo cha Mwalimu kama hakuna namna? Pia kuna utata zaidi ya nia ya Sabodo kusimama na kulala CCM lakini bado akajifanya ana mapenzi na Chadema. Je Sabodo ametumwa na CCM kuwahujumu Chadema kwa njia ya kuwadhalilisha ili wakati ukifika CCM watumia udhaifu huu kuwaumbua na kuwamaliza kisiasa?Je Sabodo anasukumwa na uzalendo na mapenzi wa demokrasia na Chadema au anatumwa na genge la wahindi linaloanza kuhofia maslahi yao kama CCM itapoteza dola? Je kwa namna hii si kuiweka Chadema kishawishini ili hatimaye iingie mfukoni mwa Sabodo na genge lake? Tunahofia hili kutokana na mazoea ya kuona karibu kila utawala kuanzia awamu ya pili unakuwa na mhindi nyuma yake akiwakilisha maslahi ya genge lake na watawala mafisi na mafisadi. Nani mara hii kasahau Gulamali aliyefikia hadi kumwita first lady Sitti Mwinyi Shemeji? Huyu alifika chini ya Ali Hassan Mwinyi sawa na Mohamed Raza alivyosifika chini ya Salmin Amour . Nani mara hii kasahau yule Mhindi, Sailesh Vithlani wa rada wa wakati wa Benjamin Mkapa? Nani haoni ujio wa Mohamed Dewji aka Mo anavyozidi kuwa maarufu chini ya serikali ya Jakaya Kikwete? Je Sabodo anacheza karata mbili yaani Chadema na CCM ili atayepita naye apete? Maana ni mwanachama wa CCM na 'mfadhili' wa Chadema. Wenye kujua siasa vizuri hawafurahishwi kuona viongozi tena wa juu wa Chadema wakipanga kama vitoto vya shule mbele ya mkuu wa shule kupokea cheki toka kwa Sabodo. Je Chadema emiridhika na kujishusha hadhi hadi kuwa chama kinachoweza kufadhiliwa na mtu binafsi tena mwenye madoa badala ya umma wa watanzania ambao wamekuwa wakikiunga mkono? Kwa wanaojua thamani ya imani ya umma wanashangaa kuona Chadema inavyozidi kujivua nguo kwa zawadi na ahadi ya vishilingi milioni kadhaa bila kujua kuwa hapo baadaye hili laweza kuigharimu madaraka. Nani atawasaidia na wakamsikiliza? Naomba nitoe hoja.



Umenipootezea muda, hauna point yoyote!!!! Nilidhani utatoa ushahidi wa mali zake!!!!

@PJN at Mtwara Gas City
 
sidhani kama kinachonitatiza ni Sabodo kuchangia; la hasha. Kuna vitu ambavyo sidhani kama vimekaa sahihi... ngoja nirudi nyuma kidogo..

Ama kweli CDM ni wachaga....... Mnambagua Sabodo kwa sababu ya udini na uhindi........

Angekuwa Dr Mengi, mngepga vigelegele....

Shame on you


@PJN at Mtwara Gas City
 
Tunakushukuru Mzee wetu Sabodo, Hakika anatutakia mema. Mzee Sabodo ana utashi mkubwa, na ameona kazi nzuri inayofanywa na M4C. May the Almight God abide with Mzee Sabodo! Amen.
 
CHADEMA WAJIFUNZE KUTOKA KWA YALIYOMKUTA NICOLAS SARKOZY BAADA YA KUTUHUMIWA KUHONGWA NA MWANAMKE TAJIRI WA UFARANSA, KWANI SI VIZURI KUPOKEA KIWANGO KIKUBWA CHA PESA KUTOKA KWA INDIVIDUAL, NI WAZI KWAMBA SABODO SIO MJINGA LAKINI INAONEKANA KUNA MCHEZO WANAUCHEZA. HAINA UBISHI KWAMBA CHADEMA NDIO CHAMA MBADALA, NA MPAKA SASA WANANCHI WAMESHAICHOKA CCM, SO CHADEMA SHOULD PLAY THEIR CARD VERY WISELY AND TRICKILY, VINGINEVYO JUMBA BOVU LITAWAANGUKIA NA WATAKUWA KATIKA SAME PATH (UFISADI) NA CCM.

Stay Tuned!!
 
Nyie endeleeni kupokea hiyo misaada mwisho wa siku mtakuja kujuta usicheze na Wahindi kabisa, hakuna hata Pro-Chadema JF hata mmoja anajua Sabodo anafanya kazi gani zaidi watakuambia mfanyabiashara.
 
Mleta mada mbona unaleta habari nusu nusu, Mzee Sabado kasema Chadema itapatiwa duka moja kwenye jengo la kuegesha magari kama mradi wa chama, duka moja si litaleta ugomvi kwenye chama.
 
user-offline.png
mpayukaji
CCDM kupokea pesa toka kwa huyu ndg si kosa kumbuka kuwa CDM kwenye mikutano yake ya hadhara imekuwa ikipokea michango toka kwa wananchi wanahudhuria mikutano hiyo na wenye mapenzi mema na chama pia nchi hii tofauti yake ni kiwango cha pesa tu

issue ya namna pesa zinavyo patikana hilo ni suala la serikali yetu. Labda sema kinacho weza kuwaua CHADEMA ni transpancy dhidi ya matumizi ya hizi pesa na umakini mkubwa kufanya kile kilicho kusudiwa tena kwa WAKATI kama
Kimbunga anavyo lalamika.

Mkuu

Huna haja ya kuwa na wasiwasi kama Kimbunga. Zitatumika accordingly kwa ajili ya maendeleo ya watu.

Lakini pia tu ni vyema kukumbuka, kuzingatia na kutumia vyema kifupi cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Vinginevyo utaingia kwenye mitego ya CCM. Angalizo tu.
 
Mleta mada mbona unaleta habari nusu nusu, Mzee Sabado kasema Chadema itapatiwa duka moja kwenye jengo la kuegesha magari kama mradi wa chama, duka moja si litaleta ugomvi kwenye chama.


Naona kama kawaida yenu. Unaanzisha topic katikati ya topic, kisha unajipatia majibu. Ugomvi wa wana-CHADEMA ni mmoja tu, ufisadi wa CCM na serikali yake dhidi ya maendeleo ya Watanzania. Ugomvi mbele yetu ni ubadhirifu, wizi wa mawaziri wa CCM, mauaji yanayofanywa na serikali ya chama hicho dhidi ya raia wasiokuwa na hatia, ikiwa ni dalili ya mporomoko wa kasi kuelekea bahari ya kusahauliwa.
 
Tumaini Makene ..mfano mzuri ni jirani zetu wa kenya, waangalieni vyama vya upinzani wanavyouana wenyewe kwa wenywe wakati mzee moi katulia kwake...shame siasa za tz hakika sitopiga kula kamwe maisha..huyu sabodo halipi kodi sasa ameona ahamie upande wa pili wa shilingi hasije sumbuliwa 2015, chadema fikirila hii kitu itawacost


Kamanda Kigoma 'kwenu'

Asante sana kwa kuzidi kutuonesha na kudhihirisha kuwa Serikali ya CCM hii sikivu ni CORRUPT KIASI HIKI.

Lakini pia mbona mfano wako hauwiani na hoja yako unayoibua hapa...nway fine, kama Sabodo halipi kodi kama ambavyo wewe unaonekana kujua zaidi kuliko serikali na vyombo vyake, basi weka ushahidi hapa kisha utuambie kwa nini serikali hii sikivu ya CCM haikamati wakwepa kodi. Mwalimu alituambia moja ya sifa ya serikali corrupt, ni kutokukusanya kodi (contextual meaning here kutokuwa na uwezo wa kudhibiti wakwepa kodi).

Uamuzi wako wa kutopiga kura maisha yako yote ambao unapaswa kupuuzwa na mtu yeyote makini na akili timamu...haumkomoi mtu yeyote bali utaendelea kukutafuna wewe mwenyewe na kukutesa ndani ya moyo wako...

Asante kwa kutuonesha kuwa serikali ya CCM ni CORRUPT mpaka hapo utakapoonesha otherwise.
 
Tumaini Makene Mkuu ukisikia uzalendo wa kweli kwa Mtanzania ndio huo, bila kujali dini kabila wala chama anafanya kile kinachotakiwa kufanywa na Watanzania wote!!!VIVA MZEE SABODO VIVA MAKAMANDA WA CDM, DAIMA MBELE NYUMA NI MWIKO!!!



Mi nitasema nini tena bwana, wakati wewe ulishasema ni "Mtumishi wao", tehe tehe tehe. Lakini walivyo wa ajabu hawatasita kumpachika udini, ukanda na ukabila, chezea akili akina naniii wewe...tuwaelimishe.
 
Something is very wrong; there is something I don't LIKE about it. Can't point it out yet but it is there...

Kuhusu huo mkono wa kushoto ambaoametumia kutoa hundi? maana mara zote anatoa kwa kutumia mkono wa kushoto sijui ni kwa nnini anafanya hivyo?
 
Sabodo kwa matendo yake unajua kuwa ni CHADEMA kwani moyoni alishahama CCM.Sabodo amewapa CCM fedha nyingi sana lakini wanatafuna tu na ndio sababu amewakimbia.
 
Kuhusu huo mkono wa kushoto ambaoametumia kutoa hundi? maana mara zote anatoa kwa kutumia mkono wa kushoto sijui ni kwa nnini anafanya hivyo?


Kamanda Ngosha, kenehe wang'u father. Mpe pole Mzee Sabodo. Amepooza upande huo ambao ulitaka ufanye kazi ya kukabidhi hiyo hundi mara hizo zote unazofahamu. Mwaka wa 13/15 sasa unasumbuliwa na kupooza.

Hata kusaini hundi au tuseme kuandika, anatumia mkono huo wa kushoto, hata kutembea anatembea kwa shida sana, yaani mguu wa upande huo pia haufanyi kazi. Kama unamjua vyema, hata kuongea pia hawezi kuzungumza vyema.

Mpe pole plz kamanda. Na bila shaka muombee aendelee kupata heri katika afya yake na kuendelea kuwatoa uoga na kuwajaza ujasiri Watanzania. Tusonge mbele.
 
Mkuu Kimbunga uchimbaji wa visima huamki tu asubuhi na kuanza kuchimba ni lazima kuwe na survey ya kutosha na uhakika wa maji yatakayokuwepo kwa muda mrefu. Otherwise utajikuta mmetumia raslimali pesa vibaya na tutaanza kuwanyooshea vidole chadema kwa matumizi mabaya ya pesa. Ndo maana hata yeye kawaambia hiyo jana kuwa watafute wakandarasi wenyewe wa wafanye detailed survey wenyewe ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi.

Mkuu Mr.Professional muda unaenda lakini hata mchakato sijausikia! Huo ndio wasiwasi wangu
 
Last edited by a moderator:
[h=3][/h]




Sina
ugomvi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wala mpenzi wake
mpya Mustafa Jafary Sabodo. Nina ugomvi na staili ya Sabodo ya
'kukisaidia' Chadema. Kila akijisikia kupata publicity, huwaita viongozi
wa Chadema na kuwapa milioni kadhaa za shilingi. Sijajua ni kwanini
Chadema hawataki kujua historia ya 'utajiri' wa Sabodo anayejinasibu
kama mjamaa aliyekuwa karibu na baba wa taifa Mwl Julius Nyerere. Kwa
wanaojua ushupavu na uwazi wa Mwalimu wanashangaa ni kwanini uhusiano
wao na Sabodo umekuwa maarufu baada ya kifo cha Mwalimu kama hakuna
namna? Pia kuna utata zaidi ya nia ya Sabodo kusimama na kulala CCM
lakini bado akajifanya ana mapenzi na Chadema. Je Sabodo ametumwa na CCM
kuwahujumu Chadema kwa njia ya kuwadhalilisha ili wakati ukifika CCM
watumia udhaifu huu kuwaumbua na kuwamaliza kisiasa?Je Sabodo anasukumwa
na uzalendo na mapenzi wa demokrasia na Chadema au anatumwa na genge la
wahindi linaloanza kuhofia maslahi yao kama CCM itapoteza dola? Je kwa
namna hii si kuiweka Chadema kishawishini ili hatimaye iingie mfukoni
mwa Sabodo na genge lake? Tunahofia hili kutokana na mazoea ya kuona
karibu kila utawala kuanzia awamu ya pili unakuwa na mhindi nyuma yake
akiwakilisha maslahi ya genge lake na watawala mafisi na mafisadi. Nani
mara hii kasahau Gulamali aliyefikia hadi kumwita first lady Sitti
Mwinyi Shemeji? Huyu alifika chini ya Ali Hassan Mwinyi sawa na Mohamed
Raza alivyosifika chini ya Salmin Amour . Nani mara hii kasahau yule
Mhindi, Sailesh Vithlani wa rada wa wakati wa Benjamin Mkapa? Nani
haoni ujio wa Mohamed Dewji aka Mo anavyozidi kuwa maarufu chini ya
serikali ya Jakaya Kikwete? Je Sabodo anacheza karata mbili yaani
Chadema na CCM ili atayepita naye apete? Maana ni mwanachama wa CCM na
'mfadhili' wa Chadema. Wenye kujua siasa vizuri hawafurahishwi kuona
viongozi tena wa juu wa Chadema wakipanga kama vitoto vya shule mbele ya
mkuu wa shule kupokea cheki toka kwa Sabodo. Je Chadema emiridhika na
kujishusha hadhi hadi kuwa chama kinachoweza kufadhiliwa na mtu binafsi
tena mwenye madoa badala ya umma wa watanzania ambao wamekuwa wakikiunga
mkono? Kwa wanaojua thamani ya imani ya umma wanashangaa kuona Chadema
inavyozidi kujivua nguo kwa zawadi na ahadi ya vishilingi milioni kadhaa
bila kujua kuwa hapo baadaye hili laweza kuigharimu madaraka. Nani
atawasaidia na wakamsikiliza? Naomba nitoe hoja.

kafie mbali M4C inakuja and you and your dam pals cannot do a dam thing to stop the peoples power!
 
Back
Top Bottom