MZEE Mustafa Jaffer Sabodo achangia tena M4C (CHADEMA) na ahadi zingine za miradi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MZEE Mustafa Jaffer Sabodo achangia tena M4C (CHADEMA) na ahadi zingine za miradi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Jul 5, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  MFANYABIASHARA maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mustafa Jaffer Sabodo amekichangia tena Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), sh. milioni 10, huku akitoa ahadi nyingine mpya ya kukipatia chama hicho mradi wa kukiingizia mapato na kuchimba visima kwa majimbo ya chama hicho kwa miaka 10.


  [FONT=&amp]Amesema kuwa kazi inayofanywa na chama hicho kutoa elimu ya uraia hadi vijijini, huku kikizidi kuimarisha mtandao wake kwenye ngazi za vitongoji na mitaa kikidhamiria kuendelea kupigania na kutetea haki za wananchi, inapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania mpenda maendeleo.[/FONT][FONT=&amp]
  [/FONT]

  [FONT=&amp]Mfanyabiashara huyo ambaye amekuwa akijitokeza waziwazi bila uoga kukichangia chama hicho cha upinzani, akisema anafurahishwa na kazi ambayo kinafanya ya kutetea maslahi na rasilimali za Watanzania kutengeneza fursa za maendeleo, ameongeza kuwa amefurahishwa na Operesheni Okoa Kusini, ambayo chama hicho kilifanya karibuni mikoa ya Lindi na Mtwara.[/FONT]
  [FONT=&amp][/FONT]
  [FONT=&amp]Akizungumza jana nyumbani kwake ambako alikutana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa kwa ajili ya kuzungumzia mchakato wa utekelezaji wa ahadi alizotoa kwa chama hicho, Mzee Sabodo aliahidi kuwa baada ya kukamilika kwa jengo la kuegesha magari linalojengwa katikati ya Jiji la Dar es Salaam, sehemu ya mapato yatatumika kuchimba visima kwa miaka 10.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mbali ya sehemu ya mapato kutoka katika jengo hilo la kuegesha magari ambalo linajengwa na Taasisi ya Khoja Shia Ithnasheri Jamaat (KSIJAMAAT), pia Mzee Sabodo alisema kuwa sehemu ya chini ya jengo hilo ambayo itakuwa na maduka, CHADEMA itapatiwa duka moja kama mmoja wa miradi ya kukipatia mapato.[/FONT]

  [FONT=&amp]"Mtapata sehemu ya mapato ili kuchimba visima kwenye majimbo yenu kwa miaka kumi…pia mtapata duka pale ili mpate mradi wa mapato. Ili kuharakisha utekelezaji wa ahadi ya visima vile vingine fanyeni survey ninyi wenyewe na mpate mkandarasi, itakuwa sehemu ya gharama ya uchimbaji…hizi milioni 10 mtapata hundi hapa mkafanye kazi za wananchi," alisema Mzee Sabodo.[/FONT][FONT=&amp]
  [/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Slaa, mbali ya kumshukuru na kumpongeza Mzee Sabodo kwa ujasiri wake wa kuendelea kujitoa kusaidia harakati za kupigania haki za wananchi, mabadiliko ya kiutawala na kimfumo nchini, aliahidi kuwa chama hicho kitaendelea kutimiza wajibu wake kwa maslahi ya Watanzania.[/FONT][FONT=&amp]
  [/FONT]

  [FONT=&amp]"Umekuwa mtu wa msaada mkubwa kwetu, umeendelea kuwatia moyo Watanzania wote wa kila namna kuacha uoga wa kuchangia harakati hizi, kwani lengo letu ni kuwatumikia Watanzania katika kila fursa tunayoipata, ambapo kwa sasa tutaendelea kuisimamia na kuiwajibisha serikali ya CCM ambayo ni dhahiri ielekea mwisho na wananchi wameichoka.[/FONT][FONT=&amp]
  [/FONT]

  [FONT=&amp]"Nasi tunawaahidi Watanzania wote kuwa tutaendelea kuwatumikia na hatutawaangusha, tunatambua kuwa katika mparanganyiko huu mkubwa, kama ugumu wa maisha, hali mbaya ya uchumi, siasa zinazoyumba, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma na migogoro katika makundi mbalimbali ya kijamii kwa sababu ya uongozi mbovu, CHADEMA linabaki kuwa ndiyo tumaini pekee kwa Watanzania," alisema Dkt. Slaa.[/FONT][FONT=&amp]
  [/FONT]

  [FONT=&amp]Dkt. Slaa aliyeambatana na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA, Antony Komu, aliongeza kuwa visima vya ahadi hii mpya kutokana na mapato ya jengo la maegesho ambayo ni tofauti na ahadi za visima vingine alizowahi kutoa mwaka jana na mapema mwaka huu, vitachimbwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania yenye kero kubwa za maji.[/FONT][FONT=&amp]

  [/FONT]
  [​IMG]

  [FONT=&amp]Mbali ya ahadi hizo mpya za jana, Mzee Sabodo na Dkt. Slaa walizungumzia juu ya mchakato wa utekelezaji wa ahadi mbalimbali zingine za mfanyabiashara huyo na kada wa CCM, ambazo amekuwa akitoa kwa CHADEMA mara kadhaa tangu mwaka 2010, zikiwemo za ujenzi wa chuo, uchimbaji wa visima, ofisi za makao makuu ya chama hicho na baiskeli 100 za walemavu.[/FONT]
   

  Attached Files:

 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  CCM apo ingekuwa hamu yao wangemlimboka au ata kumuwangwe!
  Twakutakia maisha marefu mzee wetu!
  WEnye wivu wajinyonge
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mara ya mwisho CCM walimtuma Sophia Simba kwenda kumwangukia Mzee Sabodo, safari hii sijui watamtuma nani? Labda yule msoma nukta - Nchemba!
   
 4. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sijui CCM wanajisikiaje wakione mzee Sabodo akikisaidia Chama cha CDM kiasi hiki
   
 5. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Safi sana mzee Sabodo kwa pamoja tutaikomboa Tanzania.
   
 6. varavara

  varavara JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 80
  yah! tunahitaji watu kama sabodo ambao wanachangia harakati bila mabadiliko bila woga, iwe kwa kutoa fedha au kujitoa binafsi mbele ya umma kutetea na kusimamia harakati za mabadiliko...
   
 7. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #7
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Bila shaka watakuwa wanajiandaa kukaa kikao cha kumwita ni mdini, mkanda na mkabila. Viongozi wa kikao ni wale wanaoongoza kwa kuugua CHADEMA-phobia, Wassira, Mwigulu, Yule mpayukaji wao mkuu, Martha Mlata, Stella Manyanya, Lusinde na wengine kibao kama mnavyowajua wale ambao akili zao zimejaa ubaguzi muda wote. Mchawi huwa wa kwanza kuwaita wenzake wachawi ili kupoteza lengo la mashambulizi.
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Asante baba,asante sana.
   
 9. makusanya

  makusanya JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Watamtuma mabuba,jionista na lile chemba wao kujibu mapigo ngoja uone
   
 10. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Saaaafi Sabodo..
  Hawa ndio wazalendo tunao wahitaji.. Sio VILAZA wanaochukua MIFWEZA yetu na kwenda kunenepesha wakoloni huku Serikali ikibebeshwa mzigo wa madeni na wao wakiendelea kuponda raha bila aibu.. Mungu atakupa zaidi yale wanao jinadu kwa HARAMBEE Makanisani
   
 11. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Saaaafi Sabodo..
  Hawa ndio wazalendo tunao wahitaji.. Sio VILAZA wanaochukua MIFWEZA yetu na kwenda kunenepesha wakoloni huku Serikali ikibebeshwa mzigo wa madeni na wao wakiendelea kuponda raha bila aibu.. Mungu atakupa zaidi yale wanao jinadi kwa HARAMBEE Makanisani
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Politics aside namadmire sana mzee huyu kwani hata kama tuna tofautiana kisera vitendo kama hivi vinaonyesha kweli uzalendo.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hukumbuki jibu la Nape kwa wanaojiondoa CCM ndilo linalomhusu Sabodo
   
 14. RUCCI

  RUCCI JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 1,696
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  Sera zako ni zipi?
   
 15. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninachodhani ni kwamba Mr. Sabodo anafanya biashara zake kihalali sana. Kama ingekuwa vinginevyo wangemtupia kashfa na kumchafua Magazetini kama kawaida yao. Lakini kwenye hili wanaona aibu sana na tunajua wana hasira za kufa mtu huku wakishuhudia Chadema wakila bingo kila kukicha kutoka kwa mzee Sabodo.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Something is very wrong; there is something I don't LIKE about it. Can't point it out yet but it is there...
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jul 6, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee asije akaishia Mabwepande...
   
 18. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Naona kama Sabodo anawadhalilisha Chadema kwa faida zake binafsi na chama chake cha mafisadi. Huwa siamini wafanya biashara ambao ukiwauliza walivyochuma huo utajiri utakuta ni mafisadi wa kunuka. Hakika penye udhia penye rupia. Chadema wanazidi kuingia kwenye tope la ufisadi.
   
 19. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]

  [​IMG]

   • [​IMG]
   • [​IMG][​IMG]
   [​IMG]  Sina ugomvi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wala mpenzi wake mpya Mustafa Jafary Sabodo. Nina ugomvi na staili ya Sabodo ya 'kukisaidia' Chadema. Kila akijisikia kupata publicity, huwaita viongozi wa Chadema na kuwapa milioni kadhaa za shilingi. Sijajua ni kwanini Chadema hawataki kujua historia ya 'utajiri' wa Sabodo anayejinasibu kama mjamaa aliyekuwa karibu na baba wa taifa Mwl Julius Nyerere. Kwa wanaojua ushupavu na uwazi wa Mwalimu wanashangaa ni kwanini uhusiano wao na Sabodo umekuwa maarufu baada ya kifo cha Mwalimu kama hakuna namna? Pia kuna utata zaidi ya nia ya Sabodo kusimama na kulala CCM lakini bado akajifanya ana mapenzi na Chadema. Je Sabodo ametumwa na CCM kuwahujumu Chadema kwa njia ya kuwadhalilisha ili wakati ukifika CCM watumia udhaifu huu kuwaumbua na kuwamaliza kisiasa?Je Sabodo anasukumwa na uzalendo na mapenzi wa demokrasia na Chadema au anatumwa na genge la wahindi linaloanza kuhofia maslahi yao kama CCM itapoteza dola? Je kwa namna hii si kuiweka Chadema kishawishini ili hatimaye iingie mfukoni mwa Sabodo na genge lake? Tunahofia hili kutokana na mazoea ya kuona karibu kila utawala kuanzia awamu ya pili unakuwa na mhindi nyuma yake akiwakilisha maslahi ya genge lake na watawala mafisi na mafisadi. Nani mara hii kasahau Gulamali aliyefikia hadi kumwita first lady Sitti Mwinyi Shemeji? Huyu alifika chini ya Ali Hassan Mwinyi sawa na Mohamed Raza alivyosifika chini ya Salmin Amour . Nani mara hii kasahau yule Mhindi, Sailesh Vithlani wa rada wa wakati wa Benjamin Mkapa? Nani haoni ujio wa Mohamed Dewji aka Mo anavyozidi kuwa maarufu chini ya serikali ya Jakaya Kikwete? Je Sabodo anacheza karata mbili yaani Chadema na CCM ili atayepita naye apete? Maana ni mwanachama wa CCM na 'mfadhili' wa Chadema. Wenye kujua siasa vizuri hawafurahishwi kuona viongozi tena wa juu wa Chadema wakipanga kama vitoto vya shule mbele ya mkuu wa shule kupokea cheki toka kwa Sabodo. Je Chadema emiridhika na kujishusha hadhi hadi kuwa chama kinachoweza kufadhiliwa na mtu binafsi tena mwenye madoa badala ya umma wa watanzania ambao wamekuwa wakikiunga mkono? Kwa wanaojua thamani ya imani ya umma wanashangaa kuona Chadema inavyozidi kujivua nguo kwa zawadi na ahadi ya vishilingi milioni kadhaa bila kujua kuwa hapo baadaye hili laweza kuigharimu madaraka. Nani atawasaidia na wakamsikiliza? Naomba nitoe hoja.
   
 20. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  CDM ni chama makini chenye viongozi makini. Usifananishe na CCM
   
Loading...