Kiby,
Hili ni swali ambalo wengi hawataki lijadiliwe hapa.
Wengi wamekimbilia tu kumlaani mzee Mtei bila
ya kujadili kile alichosema kama kina ukweli au la
Ukweli ni kuwa JK ni mdini - sasa ameanza kujionesha
wazi wazi.
Ukweli pia ni kuwa, kama angekuwa Mkapa ndiye kateua
tume ya katiba na akaweka wakristo wengi kuliko waislam,
maandamano yangekuwa ndio chakula cha mchana na jioni
kwa wakazi wa Dar.
Well said. Tuuangalie ukweli kama ulivyo. Binafsi nilitegemea busara itumike kuunda hiyo tume hasa ukizingatia uislamu na ukristo ulioko nchini. Kusema hivi si ukabila, ni ukweli wa mambo. Hili lingetokea kwa wenzetu waislamu ungesikia kishindo chake, lakini wakristo sio watu wa malumbano na ndiyo maana wako kimya.
Tungoje tuone. Mtikila ameamua kulipeleka mahakamani.