Mzee Mkuchika tangu kipindi cha Nyerere yupo Serikalini mpaka sasa. Ana nini cha ajabu?

Huyu jamaa alichoandika kwanza mkuchika ana rank ya captain na sio luteni, pili kuwa waziri wa utumishi na utawala Bora haina maana ww ndo mkuu wa idara ya usalama, mkuu wa idara ya usalama ni DG wa usalama na ndie mtendaji mkuu wa idara na anaripoti direct kwa raisi...unaposema mkuchika anatunza document za Siri za nchi una maana gani? Mbona mnaongea vitu vya kitoto

..Mkuchika angekuwa ni askari mzuri angebakishwa jeshini.

..wakati wa Mwalimu Nyerere kulikuwa na askari professionals na askari makamisaa wa siasa.

..nalazimika kusema kwamba Mkuchika ni mwanasiasa mzuri, lakini siyo askari mzuri.
 
Nchi bila umoja wa kitaifa na amani haiwezi kuendelea hiyo ndio injini iliyobomoa ukabila Tanzania na kuulilia mbali uchifu Tanzania na kushauri Lugha ya Taifa iwe kiswahili na kupiga marufuku matumizi ya lugha za kienyeji kwenye vyombo vya habari na maofisini na mikutano ya kampeni za kisiasa.

Huu umoja wa kitaifa unaouona hiyo ndio injini behind the scene ya Nyerere.

Jeshi kusukwa likadukika injini ni huyo mzee.

KISWAHILI:

Lugha ya Kiswahili ilikuwa imeenea Tanganyika kabla hatujapata uhuru.

Wakati wote wa harakati za uhuru mikutano ya Tanu ilikuwa ikiendeshwa kwa Kiswahili.

Ni maeneo[ mikutano ] mawili tu ambayo Mwalimu alihutubia na kuhitaji mkalimani.

Kwa hiyo si kweli kwamba Mwalimu ndio alisambaza Kiswahili Tanganyika au Tanzania.

2: UCHIFU.

Machifu walishaanza kupoteza nguvu kabla hata Mwalimu Nyerere na serikali hawajafuta Uchifu.

Kwa mfano, yako makabila ambayo yalishapiga kura ya kukataa Uchifu kabla hata ya uhuru wa Tanganyika.

Pia viko vyama vya kikabila ambavyo viliachana na harakati za jamii zao tu, na kuunga mkono harakati za KITAIFA za kudai uhuru za Tanu.

Maeneo mengi Tanu ilisimama juu ya " mabega " ya vyama vilivyoundwa kutetea maslahi ya makabila mbalimbali wakati wa utawala wa Muingereza.

3. JESHI.

Kwanini kuna habari ya jeshi kuundwa upya, lakini hatusikii kama POLISI iliundwa upya?

AFRICANIZATION ilitekelezwa ktk jeshi la Polisi kabla haijatekelezwa ktk jeshi la Tanganyika / Tanganyika Rifles.

Ucheleweshaji wa zoezi la Africanization ktk Tanganyika Rifles ulisababisha kutokee maasi ya 1964.

Kwa hiyo tulilazimika kuunda JWTZ kutokana na maasi ya Tanganyika Rifles ya 1964.

Maofisa wazawa waliokuwa ktk Tanganyika Rifles walikuja kuwa sehemu ya jeshi jipya.

Pia kuna kipindi kikosi cha jeshi toka NIGERIA kilikuja kusaidia ulinzi wa Tanganyika.

Cc Nguruvi3 , Pohamba
 
Pia kuna kipindi kikosi cha jeshi toka NIGERIA kilikuja kusaidia ulinzi wa Tanganyika

Askari wa Nigeria walikuja baada wa uasi wa jeshi 1964! Uasi wa jeshi mwaka 1964 ulizimwa na jeshi la wanamaji wa Kiingereza wakiongozwa na Mkuu wa K.A.R wakati huo Shotto Douglas.
 
Nyerere alipata kusema katika moja ya hotuba zake; "---- mimi na wazee wangu tulielewana sana bila wazee mambo hayaendi,--- ngoma ya kitoto haikeshi---".

Hiyo yawezekana ndiyo sababu Mkuchika awamu ya kwanza yumo, yapili yumo, ya tatu yumo, ya nne yumo, ya tano yumo na ya sita yumooo, labda na ya saba atakuwemo hatujui.🤣

Huwezi kumfananisha Mkuchika na watu kama Lukuvi ingawa wamedumu wote chamani kwa muda merlu. Mkuchika ni muadilifu na hana tamaa ya cheo!! Nakumbuka kuna wakati ilitokea kashfa kwenye wizara aliyokuwa anaiongoza na akajitolea kujiuzuru lakini Rais akamkatalia!!
 
Huwezi kumfananisha Mkuchika na watu kama Lukuvi ingawa wamedumu wote chamani kwa muda merlu. Mkuchika ni muadilifu na hana tamaa ya cheo!! Nakumbuka kuna wakati ilitokea kashfa kwenye wizara aliyokuwa anaiongoza na akajitolea kujiuzuru lakini Rais akamkatalia!!


Lukuvi yupoje tofauti na huyo Mkuchika??
 
Askari wa Nigeria walikuja baada wa uasi wa jeshi 1964! Uasi wa jeshi mwaka 1964 ulizimwa na jeshi la wanamaji wa Kiingereza wakiongozwa na Mkuu wa K.A.R wakati huo Shotto Douglas.

..Unachosema ni kweli kabisa.

..Maasi yalizimwa na vikosi vya British Royal Marine Commandos.

..Makomando wa Uingereza walikuja kwa meli iliyokuwa stationed Aden, Yemen.

..baada ya maasi yale kuzimwa, inasemekana Tanganyika iliomba msaada toka Algeria, Ethiopia, na Nigeria, walete askari watakaochukua nafasi ya makomando wa Uingereza waliokuwa wanaondoka.

..Kikosi cha 3 [ 3 rd battalion ] cha jeshi la Nigeria ndicho kilicholetwa kuwapokea makomando wa Kiingereza waliokuwa wanalinda usalama baada ya maasi.

 
Mwenye wasifu pls atuwekee hapa.

Huyu Mzee ana jambo gani ambalo limemfanya adumu katika vipindi vyote vya uongozi wa nchi hii? Amekuwa zaidi ya Wassira!

Hebu mnaomfahamu mtujuze kuna nini kwa huyu Mzee wetu?
Wazee ni shockabsober katika jamii
 
Ni muasisi wa Taifa la Tanzania.

Unavyoiona hii Tanzania ilivyo huyo mzee ndie aliisuka akampelekea mapendekezo Nyerere nchi iweje.

Ni mzee low profile but very powerfuk behind the scene huyo ndie alikuwa engine ya Nyerere hapendi camera za waandishi wa habari wala front page za magazeti huwa ni mtendaji mkali wa uhakika behind the scene ndio maana Maraisi wote hakuna aliyekubali kumuacha
Siyo huyu alishawahi kushinda kwa tofauti ya kura moja kweli? Au nachanganya?
 
Back
Top Bottom