CODEX GIGAS; Kitabu cha kale chenye historia ya ajabu

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
FB_IMG_1684767165680.jpg
FB_IMG_1684767165680.jpg

KUTOKA KWA NYEMO CHILONGANI.

Tuanze kupiga mastori kadhaa kuhusu mambo mbalimbali yaliyowahi kutokea miaka hiyo ya nyuma. Nataka leo nikwambie kitu kimoja kuhusu kitabu kikubwa sana, kitabu kisicho cha kawaida ambacho watu wengi wanasema ni Biblia ya Shetani.

Usishtuke sana, acha tupige mastori kidogo. Kitabu hiki kinaitwa CODEX GIGAS, Kina ukubwa wa urefu wa sentimita 92 na upana wa sentimita 22. Na kitabu hiki kina uzito wa kilo 75, kwa maana hiyo kuna watu wengi humu ndani hawawezi kukibeba kitabu hiki kutokana na uzito wake.

Kitabu hiki pia kinaitwa Biblia ya Shetani. Kiliandikwa karne ya 13 ndani ya mji mmoja ambao kwa sasa ni nchi iitwayo Jamhuri ya Czech.

Codex Gigas kimefanyiwa binding kwa mbao, karatasi zake au velum ambapo maandishi yake yameandikwa zimetokana na ngozi za punda wapatao 160. Kitabu hiki kina jumla ya kurasa 320 lakini kwa sasa zipo kurasa 310, watu wanajiuliza je, karatasi kumi ndani ya kitabu hicho zipo wapi? Hakuna ajuaye.

Kuna stori nyingi kuhusu hiki kitabu, maelezo yake ni mengi sana na nikianza kuyaelezea mahali hapa hatutofika mwisho. Ngoja nirukeruke chapuchapu halafu niangukie kwa mtu aliyekiandika kitabu hicho.

Kitabu hiki kiliandikwa na jamaa mmoja aliyeitwa kwa jina la Herman The Recluse huko Czech ambaye alikuwa Monk. Kama unavyojua jinsi washkaji walivyokuwa na sheria kali, sasa siku moja Monk huyu alifanya kosa kubwa ambalo alitakiwa kufa mara moja, aina ya kifo ambacho alitakiwa kuadhibiwa ni ‘walled up’. Hii ni aina ya kifo unaingizwa kwenye chumba kidogo cha ukuta, halafu unaachwa humo, yaani umesimama tu kama mlingoni, utaachwa mpaka kifo chako.

Sasa siku moja kabla ya kuadhibiwa kufa, Herman akauomba uongozi aache kitu ambacho kitawafanya watu wamkumbuke kwa miaka mingi, uongozi ukakubaliana naye na hivyo kuanza kukiandika kitabu hicho.

Kumbuka ana usiku mmoja tu wa kukiandika, hatoweza kukimaliza kwa kuwa ni kitabu kikubwa mno, alichokiomba ni kumwambia shetani amsaidie kukiandika kitabu hicho na angeitoa roho yake kwake, inasemekana kwamba shetani ndipo alipotokea na kuanza kukiandika.

Kitabu hiki kina kurasa 390. Kiliandikwa chote kwa usiku mmoja tu. Hakuna mtu ambaye alijua jamaa aliongea nini na shetani wakati akikiandika kitabu hicho lakini kwenye ukurasa wa 290 kuna picha ya shetani, picha inayomuonyesha yupo uchi wa mnyama.

Hiyo picha ndiyo iliyobatiza jina la Biblia ya shetani. Ukifungua kitabu hicho kimeandikwa na mwandiko mmoja wenye rangi tofauti kama nyekundu, kijani, bluu na dhahabu.

Ni ngumu kusema moja kwa moja kwamba mchoro huo ni wa shetani lakini kwa sababu katika kipindi hicho hakukuwa na michoro mingi ya bwana huyo, watu wakakubaliana kwamba huyo aliyechorwa alikuwa ndiye shetani mwenyewe ambaye alimsaidia monk huyu kukiandika kitabu hiki kirefu ndani ya usiku mmoja tu.

Ukiachana na mchoro huo, pia kuna picha moja ya mji fulani ambao umechorwa ndani ya kitabu kile. Ni mji gani? Hakuna mtu anayejua mpaka leo hii, hawajui kama huo mji ulikwishawahi kuwepo duniani ama unakuja kuwepo huko mbeleni.

Hicho ni kitabu cha uchawi, kitabu chenye nguvu za ajabu, ni miongoni mwa vitabu vilivyopitia sekeseke kubwa sana kwenye uwepo wake hapa duniani. Maktaba iliyokuwa imekihifadhi kitabu hicho iliwahi kuteketea moto, vitabu vyote viliungua lakini hicho hakikuungua kwa sababu mwanaume mmoja aliamua kukitupa nje, kwa kuwa ilikuwa ni ghorofani, kikamuangukia mtu mmoja aliyekuwa amesimama chini, huyo mtu alijeruhiwa vibaya.

Kwa sasa kitabu hicho kilichukuliwa na watu wa Sweden, wakakaa nacho huko miaka mingi mpaka mwaka 2007 walipoamua kukirudisha nchini Czech kama zawadi kwa Malkia Christina.

Kitabu hicho kimehifadhiwa ndani ya kioo kikubwa ambacho hakiwezi kupasuka kwa urahisi wala kuvunjwa kwa risasi (Bullet Proof).

Ukitaka kuona mfano wa kitabu hiki japo kwa kidogo tu na kujua kina nguvu kiasi gani, nenda kaitazame filamu iliyotoka majuzi ya Evil Dead Rise.
 
Utawazi wote huu hamna soft copy zaidi ya hilo zigo la kilo 75?

Shetani yeye hataki kujipambanua kwa watu mpaka afiche kitabu chake??
 
View attachment 2631366View attachment 2631366

Stori za kutunga hizi.

Yaani maelezo mengi hivi lakini hata picha ya kitabu hakuna?
 
Nimependa maelezo yako.elimu hizi zilikuwepo. Rudi ukasoma ghayatul hakam( wazaungu wanaita picatrix) ndio utaona sasa namna elimu hizo zinatumika mpaka leo.
Nikusahihishe huyo monk aliomba ili asamehewe kosa lake alitoa ahadi ya kuandika kitabu kwa usik mmoja cha elimu zote,akakubaliwa na akaanza kuandika ila mpaka usiku wa manane kaz ikawa ngumu ndio jamaa akafanya maombi ndipo akaingia mkataba na devil kumsaidia kuandika kitabu na asubui akawa ameokoka na adhabu ila ndio kalost his soul.
Wanasayans wanasema aina ya mwandiko ni huo huo kuonesha aliyeandika wala hakuchoka na alitumia muda mchache sana kuandika. Kiliporwa kama ngawira za kivita na waswedish mpaka 2007 ndio kikarudi Czech slovakia.
 
Back
Top Bottom