Mzee Mbarouk Mshimba wa Chadema amkana Hadharani Mwanawe Uzini

Mzee Mbarouk Mshimba wa Chadema amkana Hadharani Mwanawe Uzini

... kama anataka ushindi ni lazima akamwangukie babaye ili amridhie.
Ni lazima !!! Hivi wagombea waliofiwa na wazazi wao huwa wanapata ridhaa ya nani? Barubaru bana, utadhani waluwalu !!
 
Tatizo hapo Baba ni CUF/CCM. So anamwona mwanawe kama msaliti kwa kuingia CHADEMA. Yanatokea haya! Upuuzi!
 
sijawahi kuona mzazi aliyeishia darasa la tatu ivo hajui kusoma wala kuandika,anamzaa mtoto ambaye kwa bahati nzuri anapata PhD ya education,sasa mtoto anaenda kuomba kazi ya u lecturer basi babake anawahi chuo kuueleza utawala kuwa mwanae hana uwezo wa kufundisha,ni wazi kila mtu atajua mzee anazeeka vibaya...nitalazimika kumuona uyu mzee kama anazeeka vibaya!
 
moja ya gazeti hapa nchini limedai Baba Mzazi wa mgombea wa Chadema jimbo la uzini amemkana mwanawe hadharani.
amedai mwanawe huyo hana uwezo wa kuongoza kwa hivyo asipewe kura kwani hana imani naye.

Nadhani Habari leo ndio limeandika.
my take nadhani Mtoto achane na siasa, maana hata radhi zinaweza kumtoka

We mtu akiku-attack humu jamvini na kukuita wewe ni zezeta utaacha kupost threads humu Jf.?
 
Barubaru, mnazi wa siasa za kizanzibari na ubaguzi wa kieneo. Pole sana wewe kwanza kwa kushindwa kuchambua mada sawasawa na pili kwa usahaulifu. Baba ni mzazi na mlezi kwa mwanae, lakini ni Muumba. Ndio maana maisha ya mwanadamu yanawategemea wazazi kwa wakati fulani tu na si wakati wote.

Si lazima kwa baba kufahamu undani wote wa mwanae, na si lazima kwa mwana kuwa kama baba. Kwa tathmini nyepesi tu, baba ambaye ni mkereketwa wa CCM hawezi kukubaliana na mtoto mwenye itikadi tofauti na yeye kichama.

Mtu yule yule asiyefaa kuongoza, leo ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara. Dondoo nyingine ndogo tu, hata mkewe Makongoro alimwadhibu kwa kosa la kupiga honi mahakamani akiwa hakimu mkazi mahakama ya mkoa Arusha. So hayo ndo mambo ya itikadi yalivyo BARUBARU.

Nina uzoefu mkubwa sana wa kule nilikozalika Unguja. Nawajuwa watu wa huko kindakindaki na kujua mila, desturi na sirka zao kiundani zaidi.

Nafikiri kile nilichobainisha kimetimia. Mgombea lazima ashindwe uchaguzi na ameshindwa.

Sasa imebaki kuwehuka na kuwa kama duniani hayupo na akhera ajafika.

Nitakupa na mifano halisi. Mtafutr Salum Msabaha aliekuwa mwakilishi wa mji mkongwe, Naila Jidawi aliyewahi kuwa kiongozi wa Upinzani Bungeni CUF na wengine.

Lakin pia viongozi wa Chadema walikuwa wazito sana kusoma alama za nyakati. Siasa za Znz ni tofauti sana na ndio maana CUF walisoma alama za nyakati na hawakutia nguvu sana.

Kunahitajika Uongozi ulio na haraka katika kujua mambo.



 
Subiri matokeo kama hautasikia kaangukia pua.

Kwa mpango huu naweza kusema pasi na shaka yoyote ushindi kwake ni sawa na ngamia kupenya katika tundu la sindano.

Mpeni pole mgombea wenu na kumsihi aende kumwangukia mzazi wake ili mambo yawe sawa.

Maneno yametimia.

Mimi naweza kusema kuwa katika viongozi wakuu wa juu 10 (kumi). Hakuna hata mmoja mwenye uzoefu wa uongozi Serikalini na kisiasa.

Wanahitajika watu kama akina Bosi wangu Mzee Mtei Edwin au Mzee Makani walijue hilo na kutafuta watu wenye uzoefu mkubwa katika kuongoza kiserikali na kisiasa ili kuweza kujua na kuelewa upepo wa uongozi serikalini au kisiasa unakwendaje.

Poleni sana Chadema na mgombea wake wa Uzini.

 
Back
Top Bottom