Barubaru, mnazi wa siasa za kizanzibari na ubaguzi wa kieneo. Pole sana wewe kwanza kwa kushindwa kuchambua mada sawasawa na pili kwa usahaulifu. Baba ni mzazi na mlezi kwa mwanae, lakini ni Muumba. Ndio maana maisha ya mwanadamu yanawategemea wazazi kwa wakati fulani tu na si wakati wote. Si lazima kwa baba kufahamu undani wote wa mwanae, na si lazima kwa mwana kuwa kama baba. Kwa tathmini nyepesi tu, baba ambaye ni mkereketwa wa CCM hawezi kukubaliana na mtoto mwenye itikadi tofauti na yeye kichama. Kwa kukukumbusha mnamo mwaka 1995, wakati uchaguzi wa vyama vingi unafanyika kwa mara ya kwanza, Makongoro Nyerere, aligombea kupitia chama cha NCCR mageuzi, jimbo la Arusha mjini. Mwl. Nyerere (Baba mzazi wa makongoro), alimpinga na kuwaomba watu wa Arusha wasimpe kura kwa kuwa yeye na chama chake hawawezi kuongoza. Watu wa Arusha walikuwa na imani nae, na akashinda licha ya ushawishi mkubwa wa Mwalimu na CCM wakati huo. Mtu yule yule asiyefaa kuongoza, leo ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara. Dondoo nyingine ndogo tu, hata mkewe Makongoro alimwadhibu kwa kosa la kupiga honi mahakamani akiwa hakimu mkazi mahakama ya mkoa Arusha. So hayo ndo mambo ya itikadi yalivyo BARUBARU.