digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 7,901
- 14,363
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana amejitokeza na kumuomba radhi Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. John Magufuli kufuatia matukio yaliyojitokeza siku za nyuma ikiwemo mazungumzo ya simu baina yake na baadhi ya viongozi wakongwe wa CCM yakimlenga moja kwa moja Rais Magufuli.
Kauli hiyo ya Kinana ameitoa akiwa jijini Arusha, ambapo pia alipata nafasi ya kukutana na viongozi wa CCM mkoa wa Arusha akiwemo Mwenyekiti wa chama Mhe. Zelote Steven na Katibu wake Mussa Matoroka ambao wamemshukuru kwa hatua hiyo.
Kinana ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe wa CCM, baada ya kustaafu alijiikuta katika malumbano na wanasiasa wenzake na pia viongozi wake ambazo hata hivyo hakuwahi kuzizungumzia.
====
My take: Waliokuwa wanadhani JPM ni moto wa mabua sasa wametambuwa kuwa walivyodhani haikua sahihi
Zaidi, soma:
Uchaguzi 2020 - Abdulrahman Kinana asamehewa, Membe afukuzwa rasmi CCM
2), CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama