Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
23,062
Points
2,000

idawa

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
23,062 2,000
Chama cha Mapindizi CCM kimeridhia kwa kauli moja kuwasamehe Nape, January Makamba na Ngeleje hata hivyo wamepewa onyo kali wasirudie tena kosa hilo.

Hata hivyo kimeagiza kwa kauli moja kuhojiwa kwa Makatibu wakuu wastaafu Kinana na Makamba pamoja na Waziri wa Zamani Ndugu Bernard Membe.

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeagiza makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, Yusuf Makamba na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe kuhojiwa na kamati ya usalama na maadili ya Taifa ya chama hicho kujibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili.

Zaidi, soma:
FB_IMG_1576245504069.jpeg

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernad Membe
FB_IMG_1576245500230.jpeg

Yusufu Makamba Katibu mkuu wa zamani wa CCM
FB_IMG_1576245492207.jpeg

Abdulrahman Kinana Katibu mkuu wa zamani wa CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanza. Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na Watanzania kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeketi leo Ijumaa Desemba 13, 2019 jijini Mwanza chini ya Rais John Magufuli.

Mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Katika mkutano huo, imewasamehe wanachama wake watatu huku wengine wakitwa kuhojiwa.

Walioitwa kuhojiwa ni makatibu wakuu wawili wa zamani wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba pamoja na Benard Membe.

Kabla ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa wajumbe walifanya ziara ya kukagua miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa katika Mkoa wa Mwanza.

Wajumbe pia walipata muda wa kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Miaka Minne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maandalizi na maudhui ya Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 – 2030 sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa kauli moja kupongeza Serikali ya Tanzania inayo ongozwa na Rais Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayo ongozwa na Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo mafanikio makubwa ya kimaendeleo yamepatikana.

Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imepokea, kujadili na kuridhia kwa kauli moja Taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili juu ya uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM wa kuwasamehe wanachama walioomba radhi kwake baada ya kukiri mbele yake kufanya makosa ya kimaadili yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake mbele ya umma.

Wanachama hao ni;-

1. Ndg. Januari Makamba (Mb)

2. Ndg. Nape Nnauye (Mb) na,

3. Ndg. William Ngeleja (Mb)

Kikao cha HKT kimewataka wanachama hao kujirekebisha na kutorudia makosa yao ama sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa katiba, Kanuni na taratibu za Chama ikiwamo kufukuzwa uanachama.

Wakati huo huo, Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeazimia kwa kauli moja na kuelekeza kwamba wanachama wafuatao;-

1. Abdulrahman Kinana

2. Mzee Yusuf Makamba na,

3. Benard Membe

Waitwe na Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ili wajibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi.

Awali Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (HKT) imefanya uteuzi wa majina ya Wagombea wa nafasi za Uongozi katika Chama na Jumuia kama ifuatavyo;-

1. Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha

a. Ndg. Batilda Salha Buriani

b. Ndg. Zelothe Stephen Zelothe

c. Ndg. Bakari Rahibu Msangi

2. Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa

a. Mafanikio Paulo Kinemelo

b. Hilary Adelitius Kipingi

c. Lucas Felix Lwimbo

3. Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Mtwara

a. Petro Mwendo Mwendo

b. Mustafa Nguyahamba Mohamed

c. Selemani Manufred Sankwa

4. Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Dodoma

a. Ndg. Damas Mukassa Kasheegu

b. Baraka Andrea Mkunda

c. Christopher Thomas Mullemwah

5. Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani

a. Mary Daniel Joseph

b. Fredrick Gasper Makachila

c. Samaha Seif Said

Licha ya hamasa kubwa waliyokuwa nayo wajumbe wa HKT kutokana na kazi nzuri ya Serikali ya CCM, Ndg. Magufuli amesisitiza kazi ya Urais ni ngumu sana na yeye ataheshimu utamaduni na desturi za CCM, Kanuni, Katiba ya CCM na Katiba ya Nchi na kwamba CCM ni kiwanda cha kuzalisha viongozi na kwa utaratibu ambao chama kimejiwekea kitampata mtu bora zaidi atakayepokea uongozi baada yake.

Nawashukuru sana viongozi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ya Chama chetu kwa kuzisimamia vizuri Serikali zetu mbili na hivyo kuwezesha kupatikana mafanikio makubwa katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Tukaendelee kujenga umoja, kuimarisha ujenzi wa Chama chetu na tunapoelekea katika chaguzi zinazokuja tukaepuke makundi, na tuendelee kuisimamia Serikali ikiwamo kukagua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yetu, amesema Ndg. Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Credit Mwananchi
IMG_20191213_165042.jpeg
IMG_20191213_165044.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
26,486
Points
2,000

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
26,486 2,000

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Messages
2,247
Points
2,000

cutelove

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2017
2,247 2,000
Habari zilizotufikia hivu punde zinasema kamati ya CCM inayoendelea na vikao vyake jijini Mwanza inasema imewaita Benard Membe,Yusufu Makamba na Abdulahman Kinana kufika Mwanza mara moja kujieleza
FB_IMG_1576245504069.jpeg
FB_IMG_1576245500230.jpeg
FB_IMG_1576245492207.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
5,001
Points
2,000

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
5,001 2,000
Mzee Makamba na Kinana msiitikie wito huo wa ajabu ajabu unaolenga kuwadhalilisha zaidi baada ya kutendewa unyama wote ule wa kudhalilishwa na Musiba na pia kudukuliwa maongezi yenu private kinyume cha sheria za faragha.
Wazee msikubali kata kata washauri watakoutumwa pembeni yenu kujifanya wanakuja kwa busara ili kuwabembeleza na kuwasihi mwende.

Huyo aliyemtuma Musiba kuwavunjia heshima mbele ya Jamii anataka awatumie nyinyi wenyewe kujisafisha kwa siasa zake zake za kuumiza wenzie.

Nyie makanali wa Jeshi na watumishi wa CCM, hamuwezi kudhalilishwa namna hii na nyie mkaenda kupiga magoti.
KUBALINI MFE KWA HESHIMA, VIZAZI VITAWAKUMBUKA, MSIENDE KUPIGA MAGOTI

Membe Kama una nia ya kugombea uraisi kupitia CCM wewe nenda kawasikilize, kama huna nia ya kugombea uraisi basi potezea maana wewe ndo umetendewa kosa, umedukuliwa mazungumzo private kabisa kinyume cha haki yako faragha na uhuru wa kutoa maoni kwa mujibu wa katiba ya nchi
 

Forum statistics

Threads 1,392,067
Members 528,535
Posts 34,097,466
Top