Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,892
14,347


Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana amejitokeza na kumuomba radhi Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. John Magufuli kufuatia matukio yaliyojitokeza siku za nyuma ikiwemo mazungumzo ya simu baina yake na baadhi ya viongozi wakongwe wa CCM yakimlenga moja kwa moja Rais Magufuli.

Kauli hiyo ya Kinana ameitoa akiwa jijini Arusha, ambapo pia alipata nafasi ya kukutana na viongozi wa CCM mkoa wa Arusha akiwemo Mwenyekiti wa chama Mhe. Zelote Steven na Katibu wake Mussa Matoroka ambao wamemshukuru kwa hatua hiyo.

Kinana ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe wa CCM, baada ya kustaafu alijiikuta katika malumbano na wanasiasa wenzake na pia viongozi wake ambazo hata hivyo hakuwahi kuzizungumzia.
====

My take: Waliokuwa wanadhani JPM ni moto wa mabua sasa wametambuwa kuwa walivyodhani haikua sahihi

Zaidi, soma:

Uchaguzi 2020 - Abdulrahman Kinana asamehewa, Membe afukuzwa rasmi CCM

2), CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama
 
Source wapi mkuu ila hii habari kama ni kweli kuna watu watanuna na kupasuka, Maana tayari walishaanza kusema twende na Kinana 2020 haha, Mimi nilisha sema hakuna kitu mtu ataweza kufanya akiwa nje ya mfumo.

Yaani nchi hii hakuna mtu aliepo nje ya mfumo anaweza kutingisha mfumo never ever hao kina Kinana kwa sasa ni kama mtu uwaoondoe meno afu uwape nyama ambayo haija iva fresh. Hata mkwere anajua ukishakuwa nje ya system huna impact tena.

Ukizingatia hao wastaafu wana makandokando kibao
 
Source wapi mkuu ila hii habari kama ni kweli kuna watu watanuna na kupasuka, Mana tayari walishaanza kusema twende na kinana 2020 haha, Mimi nilisha sema hakuna kitu mtu ataweza kufanya akiwa nje ya mfumo, yani nchi hii hakuna mtu aliepo nje ya mfumo anaweza kutingisha mfumo never ever hao kina kinana kwa sasa ni kama mtu uwaoondoe meno afu uwape nyama ambayo haija iva fresh. Hata mkwere anajua ukishakuwa nje ya system huna impact tena
Ukizingatia hao wastaafu wana makandokando kibao
Hii hapa
Screenshot_20200604-172554.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Who is a dictator? A dictatorship is a form of government characterized by a single leader or group of leaders and little or no toleration for political pluralism or independent programs or media
Na kwa lugha uliyotumia sijui kama watakuelewa lugha ya mabeberu si rafiki kwao
 
Back
Top Bottom