Mzee Kikwete anawasalimuni

Mzee Kikwete anawasalimuni

Kwakweli sikua na mapenzi na KIKWETE,,,ila kwa hali ya nchi ilivyo natamani arejee IKULU hata Kesho.

Baba tunakukumbuka.
Ushamkumbuka mapema yote hii?? Nabado ndo kwanza N'gwe ya kwanza, mpaka zifike tano... Mtakoma!!!
 
Hata huyu aliyepo sasa akimaliza , miaka yake kumi (10), mtamkumbuka na mtamiss, watanzani ndio walivyo sijawahi kuwasikia wakimponda kiongozi aliyemaliza muda wake.
 
Tutakoma Mkuu.... Serious.
tena kwa sote nakumbukaga ule wimbo wetu wa mwaka unaosema tumejipanga mwaka huu mtaisoma ilikua masikhara lakin sasa naona kweli
 
Bavicha mnamkumbuka mtu mliemwita dhaifu,mkwere,mswahili,anacheka cheka na kila aina ya udhalilishaji.
Mungu amesikia kilio chenu,muacheni Mungu afanye kazi yake,kulalamika ni sawa na kumkashifu Mungu
 
JK ni Rais aliyefanya makubwa sana nchi hii. Sema kuna watu mliaminishwa au mlilishwa vibudu hasa kwenye vigango huko na nyie mkaingia mazima. Tizama mabarabara yalivyofunguka kila kona. Tazama majumba yalivyojengwa, tizama irrigation schemes zilivyoanzishwa, tizama watu walivyopokea mikopo ya masomo, tizama vyuo vilivyoshamiri, tizama utalii ulivyonawiri, tizama mahusiano ya kimataifa yalivyokuwa juu, ndiye Rais pekee aliyethubutu kuja na chanzo kipya kikubwa cha kuzalisha umeme (kinyerezi gas plant), tizama jengo jipya la MOI, tizama hospitali ya mlonganzila, tizama taasisi ya moyo, tizama kitengo cha Emergency Muhimbili, tizama juhudi za kupambana na malaria, tizama dawa za bure za ARVs, tizama chanjo za watoto, tizama shule kila kata. Chuki jambo baya sana. Hapana, hii ni adhabu kwenu watanzania na sharti muipokee.

Anko magu hebu ongeza spidi kidogo. Mwana kindakindaki Ritz hebu ongeza na kashata hapo.
 
Uzuri baba ni pale anapokuambia nenda kajitegemee au baba anapokufa. Kuna watu walikuwa wanaaminisha eti baba wewe ulikuwa dhaifu tulipambana nao sana..eti baba anachekacheka. Leo wamemiss tabasamu lako.

Lakini baba wewe ugomvi na rafiki yako wa ujanani umelicost taifa Leo. Baba ulishindwa kudictate na kutuletea chaguo lako/ langu pia..
Baba leo umefurahia mwaka mpya wenzako tunalia. Naikumbuka hotuba yako moja ivi ulisema you can make good president come forward. Naikumbuka ile hotuba yako bungeni kuhusu rafiki Kagame. Ulijua kucheza na diplomasia, japo umetukanwa ukasema yaishe..

Najua baba uliwajua wasaidizi wako ndo maana ukitaka kutuachia chagua lako na mshabiki wangu.
Binafsi nakulaumu kidogo kwann ulishindwa Ku dictate mchakato maana jamaa yako wa zamani ulishamkata..kwani wangefanya nn km ungelazimisha mwanadiplomasia awe Rais.

But namlaumu sana rafiki yako wa zamani kwa kudirect / influence nyumbu wake wasimpigie kura rafiki yetu na hasimu...laiti angejua.
Angejua...Japo baba mdogo uliyetuachia ni mkali sana..tunakuahidi tutampenda, kumuheshimu na kumkosoa kwa utii na adabu.

Mzee Kikwete najua unakutana sana na baba mdogo kwenye whisky meetings ( off- record meetings) tafadhali twakuomba mshauri japo kidogo hali ngumu.

Free mind
 
JK ni Rais aliyefanya makubwa sana nchi hii. Sema kuna watu mliaminishwa au mlilishwa vibudu hasa kwenye vigango huko na nyie mkaingia mazima. Tizama mabarabara yalivyofunguka kila kona. Tazama majumba yalivyojengwa, tizama irrigation schemes zilivyoanzishwa, tizama watu walivyopokea mikopo ya masomo, tizama vyuo vilivyoshamiri, tizama utalii ulivyonawiri, tizama mahusiano ya kimataifa yalivyokuwa juu, ndiye Rais pekee aliyethubutu kuja na chanzo kipya kikubwa cha kuzalisha umeme (kinyerezi gas plant), tizama jengo jipya la MOI, tizama hospitali ya mlonganzila, tizama taasisi ya moyo, tizama kitengo cha Emergency Muhimbili, tizama juhudi za kupambana na malaria, tizama dawa za bure za ARVs, tizama chanjo za watoto, tizama shule kila kata. Chuki jambo baya sana. Hapana, hii ni adhabu kwenu watanzania na sharti muipokee.

Anko magu hebu ongeza spidi kidogo. Mwana kindakindaki Ritz hebu ongeza na kashata hapo.
Yaani hawa jamaa zetu walivyokuwa NEGATIVE na JK akila nyama ikaonekana kwenye TV/MITANDAO basi wao watatangaza kuwa Tanzania ni nchi ya VEGETERIANS.

Sasa hivi ni msiba kila kona.

Zamani mlinzi wa PTA alikuwa anaendesha kilimo kwanza sasa hivi hata bajaji ni mtihani.

Na bado sasa hivi ndiyo tupo robo ya kwanza.
 
Back
Top Bottom