Mzee Kaunda na mchango wake kwenye ukombozi wa Afrika, na uhusiano kati ya China na Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
111.jpg
Aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zambia mzee Kenneth Kaunda amefariki dunia katika hospitali ya jeshi mjini Lusaka, alikokuwa amelazwa kutokana na kuumwa. Kuumwa na kuaga dunia kwa Mzee Kaunda, sio tu kumewafanya watu wengi wakumbuke mchango wake katika ukombozi wa eneo la kusini mwa Afrika, na mchango wake katika kuhimiza uhusiano kati ya China na Zambia, na kati ya China na nchi za Afrika.

Tukianza na kuangalia juhudi zake kwenye ukombozi wa nchi za Afrika kusini mwa Sahara, itakumbukwa kuwa yeye alikuwa ni mmoja wa viongozi muhimu kwenye nchi zilizoitwa Nchi za Mstari wa Mbele katika ukombozi wa eneo la kusini mwa Afrika FLS katika kupambana na ukoloni na utawala wa wazungu wachache. Mwaka 1985 alichukua nafasi ya mwenyekiti wa nchi hizo kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, na kuifanya Zambia kuwa kituo cha wana ukombozi. Ni katika kipindi chake kulikuwa na mafanikio ya kuondoa ukoloni Namibia na utawala wa wachache nchini Afrika Kusini.

Tunakumbuka kuwa ni katika kipindi hichohicho cha ukombozi kwenye eneo la kusini mwa Afrika ndipo yeye na Mwalimu Nyerere walianzisha uhusiano wa karibu na China. Mzee Kaunda na Nyerere walionana na mwenyekiti Mao Zedong, na ni wao walimwomba mwenyekiti Mao awapatie msaada wa kujenga reli itakayosaidia kuleta ukombozi wa eneo la kusini mwa Afrika. Alikumbusha akisema walipowasilisha ombi kwa Mwenyekiti Mao na Waziri Mkuu Zhou Enlai Jibu walipolpewa ni kuwa “tutakwenda pamoja kuijenga reli hiyo”, na amesema ni kweli walikuja kama ndugu kujenga reli hiyo.

222.jpg

Mzee Kaunda pia ni kiongozi mwanzilishi na mtu mwenye uelewa wa kina wa uhusiano kati ya China na nchi za Afrika. Ameshuhudia ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika tangu wakati wa mapambano ya kupigania uhuru, ameshuhudia ushirikiano kati ya China na Zambia, na China na Afrika alipokuwa Rais wa Zambia, na pia ameshuhudia ushirikiano huo hata baada ya kuondoka madarakani. Kwa hiyo alipozungumzia uhusiano kati ya China na nchi za Afrika, alikuwa anazungumzia jambo alilolijua kwa undani na alilokuwa na uhakika nalo.

Katika miaka ya hivi karibuni wakati kuna wimbi kubwa la tuhuma za vyombo vya magharibi kuwa China inafanya uporaji wa raslimali barani Afrika, Mzee Kaunda alisema wanaoishutumu China kufanya uporaji wa raslimali barani Afrika, ndio waliofanya uporaji wa raslimali barani Afrika kwa mamia ya miaka. Alikumbusha kuwa China ilizisaidia nchi za Afrika kwenye mapambano dhidi ya ukoloni na kujipatia uhuru, na imekuwa inazisadia kuendeleza uchumi, hicho ndio China inakifanya kwa nchi za Afrika, ikiwa ni rafiki wa kweli wa nchi za Afrika.

Mzee Kaunda ni mmoja kati ya wanasiasa wachache waliobaki wa kizazi cha kwanza kwenye uhusiano kati ya China na Afrika. Yeye amewahi kuwa na uhusiano wa karibu kabisa na Mwenyekiti Mao, aliyekuwa waziri Mkuu wa China Bw Zhou Enlai na hata Bw. Deng Xiaoping, na pia amewahi kufanya ziara mara nyingi nchini China kwa hiyo anafahamiana na wanadiplomasia na maofisa mbalimbali waandamizi wa China. Moja kati ya kauli zake zinazokumbukwa ni ile aliyosema “kama China ilitusaidia waafrika kwenye miaka ya 70, wakati hakuna aliyetaka kutusaidia, kwanini sasa awatilie mashaka wachina”.

Wakati Afrika inaagana na Mzee Kaunda, ni wazi kubwa mchango wake kwenye mahusiano kati ya Zambia, Afrika na China, hauwezi kusahaulika.
 
Wakati Afrika inaagana na Mzee Kaunda, ni wazi kubwa mchango wake kwenye mahusiano kati ya Zambia, Afrika na China, auwezi kusahaulika.
Kaunda alijuana na wapigania uhuru wa Tanganyika toka mwaka wa 1953.
Soma hapo chini:

Hii makala niliandika miezi michache iliyopita Mzee Kaunda alipofikisha miaka 97:

KENNETH DAVID KAUNDA NA ALLY KLEIST 1953

Leo Kenneth Kaunda katimiza miaka 97.

Nimeangalia picha ya Kenneth David Kaunda na picha hii ikanikumbusha uhusiano wa Kaunda na Ally Kleist Sykes wakati Afrika ilipokuwa katika harakati ya kupigania uhuru wake.

Usiku umekuwa mwingi In Shaa Allah kesho nitaeleza vipi Ally Sykes na Kenneth Kaunda walifahamiana miaka ya 1950 wakati Northern Rhodesia sasa Zambia na Tanganyika zilipokuwa zinapigania uhuru wake.

Ally Sykes mzee wangu nimemvulia kofia katika kutunza kumbukumbu.

Faili la safari yake yeye na Dennis Phombeah kwenda Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa vyama vya siasa Kusini ya Ikweta naamini ndilo faili mwenyewe akilipenda kuliko mafaili yake yote yenye taarifa za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ndani ya faili hili kuna ''cuttings'' ya magazeti zikieleza mkasa mzima wa safari yake kutokea Dar es Salaam hadi Salisbury ambako yeye na Phombeah walitiwa mbaroni na makachero wa Kikaburu kama ''Waafrika Wakorofi,'' na kufungiwa ndani ya banda nyuma ya nyumba ya Mzungu usiku kucha.

Asubuhi wakaachiwa na kuamriwa kurudi Tanganyika kama wahamiaji wasiotakiwa.

Hii ni movie ni ''block blaster,'' ambayo itahitaji waigizaji mahiri kucheza nafasi ya Ally Sykes, Denis Phombeah, Kenneth Kaunda, Harry Nkumbula, Charles Mzengele kachero, kibaraka wa Wazungu walowezi wa Southern Rhodesia, kachero kibaraka wa Waingereza Tanganyika, Alexander Thobias, Trevor Huddleston Mwingereza muungwana aliyekuwa rafiki wa Waafrika.

Mwaka wa 1953 Harry Nkumbula alikuwa amechaguliwa rais wa ANC na Kenneth Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini.

Mwezi Agosti Kaunda akawa Katibu Mkuu wa ANC.

Hapa ndipo Kaunda akaanza kuwatafuta wanasiasa wenzake waliokuwa Tanganyika, Kenya na Afrika Kusini na kuwaalika kwenye mkutano Lusaka, Northern Rhodesia ambao ungewakutanisha wapigania uhuru kutoka nchi za Afrika chini ya Ikweta.

Hivi ndivyo Kenneth Kaunda na Ally Sykes walivyokuja kufahamiana kwa kuandikiana barua ambazo Ally Sykes alizihifadhi hadi mimi kuja kuzisoma miaka mingi baadae.

Katika kusoma nyaraka kama hizi ndipo nikamwelewa Ally Sykes pale alipokuwa akiniambia, ''Hawa walioandika historia ya TANU hawana moja wanalolijua.''

Mkasa wa safari hii ya Ally Sykes na Denis Phombeah kuhudhuria mkutano wa Lusaka ni kisa kirefu sana lakini chote nimekieleza katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Nimeweka picha ya Charles Mzengele kachero kibaraka wa walowezi ikifuatiwa na picha ya Kenneth Kaunda na Harry Nkumbula kama walivyokuwa katika miaka ya 1950.

Ally Sykes alikuwa akitamka jina hili kama ''Mzengele,'' lakini usahihi wa jina la huyu kachero ni Mzingeli.
 
Ukweli utawale daima,tunapoelezea jambo ni vema facts zake tuzingatie ,uhuru wa Namibia hizi Frontline state's zilisaidia ILA kuna sababu kuu zilizoleta uhuru wa Namibia,swapo haikushinda ile vita ya ukombozi,hivyo hivyo kwa Msumbiji na South Africa ilikuwa more complicated vyama vyote vilivyouchukua silaha kupambana na Makuburu hakuna hata pigano moja la kivita kati yao na uhuru wa wote wa nchi hii ulichangiwa zaidi na msukumo wa UDF na mabadiliko ya uongozi wa National party.
 
RIP Kaunda. Hawa wapigania huru wa kwanza walikuwa na ajenda pana sana. Ndio maana waliweza kuvuka mipaka kujifunza mbinu tofauti. Tubadilike. Tunapita njia tu hapa. Mbwembwe zote za nini???
 
Back
Top Bottom