Mzee Farijala wa CCM Amshambulia Dkt. Charles Kitima

hakuna mfuko ulioandaliwa na CCM kuajili ya kuwasomesha watanzania bali huyo Dr kitima kasomeshwa na kodi za watanzania na sio CCM kama asemavyo huyo mzee......

Vilevile anapokataza wanafunzi wa vyuo wasifanye siasa vyuoni angeeleza ni siasa zipi hizo?,maana mbona hata vyuo vikuu kuna matawi ya vyama vya siasa na vilevile kuna course za siasa?

HIVI MZEE NIKIKUITA MBURURA NITAKUA NIMEKOSEA!?
 
Salam Wana JF,

Bila kutarajia asubuhi hii nimejikuta nalazimika kuitazama television ya TBC1 kwakua mazingira niliyokuwepo ndio channel pekee ya nyumbani inayoonekana.

Mtangazaji wa TBC1 amemkaribisha studio mzee Farijala ambaye ni kada wa CCM. Katika mazungumzo yake amejikita katika kumshambulia aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) cha Mwanza Dkt. Charles Kitima, kwamba pamoja na kuwa amesomeshwa na CCM lakini amekuwa akiikisoa sana na kuilaumu serikali ya CCM.

Mzee huyo anadai kuwa anamfahamu sana Dkt. Kitima kwamba ametoka katika familia duni sana alikuwa akivaa kaniki lakini leo hii amesahau fadhila ya serikali ya CCM.

Pia amezungumzia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutofanya siasa kwa madai kuwa wako vyuoni kusoma na si kufanya siasa akitolea mifano vyuo vya SAUT TABORA NA SAUT MWANZA.


Ukisikia ujinga ndiyo huu....watu wenye fikra kama hizi ujue ni mbumbumbu kuliko neno lenyewe...!
TBC 1 nayo wanazidi kulidumaza taifa letu; mara zote wanawahoji watu wenye fikra mgando!
 
huyo mzee ni tapeli tu anajifanya kutafutia watu kazi kumbe hana chochote,ameshawaliza watu wengi tu eti anatafutia vijana uDC mara anajuana na rais mara mawaziri,hana lolote huyo,hapa anachoonge ni kama haoni nchi ilivyo kwa sasa
 
Jamani kodi za wananchi ndizo zinazo somesha watanzania. Huyo Mzee amevimbiwa na uji nga .....CCM imetufikisha hapa kwa ufisadi wa Mali zetu watanzania
 
NI kweli mimi mwenyewe nimemuona,tatizo lake huyo kada ni njaa,yeye anaona nchi ilipo fikia ni sawa kwakuwa yeye na familia yake wanaishi sehemu nzuri(jiji lisilo na plan) maendeleo ya CCM nchi ambayo wakazi wake zaidi ya 30% hawajui kusoma na kuandika,simlaumu yeye ni njaa yake ila imepanda mpaka kwenye AKILI,unajua ata MITHALI27:22 inasema ukimtwanga mpumbavu na ngano katika kinu ata baki na upumbavu wake,SO KADA FARIJALA NI MPUMBAVU TU MUACHE ABAKI NA UPUMBAVU WAKE

COPY TO NNAPE,KINANA,NCHEMBA,PINDA,MWANA KIJIJI
 
uzuri wa dr kitima ni kwamba si mtafunaji/mpindishaji wa maneno hasa kwenye issues ambazo zinaigusa jamii moja kwa moja kitu ambacho watawala/serikali ya ccm hawapendi kusikia so si jambo la kushangaza kwa huyo mzee(farijala) kumshambali dr kitima
 
Kama huyo Farijala ni mmoja wa wale wazee wa Dar Es Salaam ambao huwa wanazungumza na JK mara panapotokea serikali kukwaruzana na wananchi wake, basi haishangazi hiyo. Tunamuombea uhai ashuhudie jinsi inavyoparaganyika kwa mikono yao wenyewe iliyojaa damu za raia wake wema.
 
Salam Wana JF,

Bila kutarajia asubuhi hii nimejikuta nalazimika kuitazama television ya TBC1 kwakua mazingira niliyokuwepo ndio channel pekee ya nyumbani inayoonekana.

Mtangazaji wa TBC1 amemkaribisha studio mzee Farijala ambaye ni kada wa CCM. Katika mazungumzo yake amejikita katika kumshambulia aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) cha Mwanza Dkt. Charles Kitima, kwamba pamoja na kuwa amesomeshwa na CCM lakini amekuwa akiikisoa sana na kuilaumu serikali ya CCM.

Mzee huyo anadai kuwa anamfahamu sana Dkt. Kitima kwamba ametoka katika familia duni sana alikuwa akivaa kaniki lakini leo hii amesahau fadhila ya serikali ya CCM.

Pia amezungumzia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutofanya siasa kwa madai kuwa wako vyuoni kusoma na si kufanya siasa akitolea mifano vyuo vya SAUT TABORA NA SAUT MWANZA.

...hilo kopo na mako mengine sampuli hiyo,muda wake wa matumizi ulishaisha,lilitakiwa liwe chini ya aridhi...hapo-lilipo sasa hivi lipo ki-makosa na linatuchafua tu mazingira...
 
hii ndo sampuli ya wazee wasio na akili nadhan ndo wale waliokua wanakua wamwisho darasani.... kwani wale wanaokuaga wa mwisho darasani wanakufaga si wanakua wakubwa??? alafu pili anatakiwa ajue kua sisi tuliosoma bure hatujasomeshwa na ccm kama anavyotaka watu wamuamini kwani sisi tumesomeshwa na wazazi wetu na watanzania wenzetu kwa jasho lao wenyewe through kodi hakuna mtu wa ccm aliyenisomesha!!!!
 
Msomi wa chuo kikuu?! Kwa taarifa yako huko vikuu ndio kuna wasomi wanao tumika kuliko unavyofikiri! Hivi unajua mbunifu wa kauli mbiu "Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya?", unamjua mbunifu wa kauli mbiu "Maisha bora kwa kila mtanzania?" Ni mtu mahiri aliye chuo kikuu! Ukiulizwa kauli mbiu zake zimefanyaje kazi kupitia mtu aliye muandikia utashangaa! Au hujui kuwa hata aliye sema "We will mafucture teachers" naye ni msomi wa chuo kikuu cha dsm?! Au hujui kuwa hata aliyesema kuwa "Sijui sababu za wananchi wangu kuwa maskini?" Naye ni mshika shahada wa chuo kikuu bora Afrika

Muambie huyo msomi wako wapenda vya bure ni wale wanao hongwa chumvi, kofia, t shirt na khanga ili wachaguliwe.

Tumia akili usitumike tu bila kushirikishaa ubongo wako.

Hajui kwamba hata Pinda ni msomi wa chuo kikuu katika fani ya sheria, lakini Juzi ameagiza polisi kupiga mtu asiye tii sheria, amesahau kabisa kwamba mahakama ndo inajua mtu wa hivyo afungwe jera au apigwe bakora kiasi gani. Na kwasasa polisi akiwa atasema ameua bahati mbaya akiwa anatekeleza maagizo ya serikali
 
waaaaaaap? mkalale tu,au hamna hoja za mana wote! ccm ndo wote wana KOTI moja? au chadema ndo wana koti moja? toa hoja bnafc c kuweka had watu wasio hucka.
 
Yule kitima ni janga kuu la taifa, mtokwa povu tu. Njaa inamsumbua

naona kila kitu kwenu ni janga la taifa, ila kwa hizi pumba zako huwezi kujilinganisha na dr kitima. ila ushauri punguza ku coment kila muda au ndo wale wa per day?
 
Hii ni nchi yetu sote, hatuwezi kuwaachia CCM waididimize. SAUT tutakuwa chachu ya mabadiliko na chemchemu ya fikra huru. Najivunia kuwa zao la chuo hiki. Ndio chuo pekee kilichobaki kupigania wananchi masikini baada ya UDSM kufungwa mdomo. Heko Dr Charles Kitima. Kwanza ni upotoshaji mkubwa kusema kwamba amesomeshwa na serikali. Kitima amelelewa na kusomeshwa na kanisa pale Kibosho seminari, baadae akaenda kusoma BA (theology) Pontifical Urban ROME, then akasoma PHD(laws) Lateran University Rome. Ni wapi hapo serikali imemsomesha?.
 
Back
Top Bottom