Mzee Farijala wa CCM Amshambulia Dkt. Charles Kitima

Mzee Farijala wa CCM Amshambulia Dkt. Charles Kitima

Mtaji wa ccm kwa sasa ni wazee kama hao waliojichokea na kudanganywa na pilau,shati la kijani,buku 5.Mzee Farijala ulidanganywa mwaka 2005 mtapewa mahakama ya kadhi na ccm,mpaka leo hakuna kitu,bakwata imekula deal kuna kadhi asiyetambuliwa na katiba wala sheria.

Hiyo mahakama ya Kadhi Waislamu walishapewa siku nyingi ila hawataki kuzianzisha wenyewe!
 
Salam Wana JF,

Bila kutarajia asubuhi hii nimejikuta nalazimika kuitazama television ya TBC1 kwakua mazingira niliyokuwepo ndio channel pekee ya nyumbani inayoonekana.

Mtangazaji wa TBC1 amemkaribisha studio mzee Farijala ambaye ni kada wa CCM. Katika mazungumzo yake amejikita katika kumshambulia aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) cha Mwanza Dkt. Charles Kitima, kwamba pamoja na kuwa amesomeshwa na CCM lakini amekuwa akiikisoa sana na kuilaumu serikali ya CCM.

Mzee huyo anadai kuwa anamfahamu sana Dkt. Kitima kwamba ametoka katika familia duni sana alikuwa akivaa kaniki lakini leo hii amesahau fadhila ya serikali ya CCM.

Pia amezungumzia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutofanya siasa kwa madai kuwa wako vyuoni kusoma na si kufanya siasa akitolea mifano vyuo vya SAUT TABORA NA SAUT MWANZA.

Mzee kaishiwa na hoja. Asitudanganye, CCM haijasomesha mtu yeyote. Na hakuna mtu aliyesoma bure. Fedha za kodi zetu ndizo zilizotusomesha. CCM itakufa, wananchi wataendelea kuwa na serikali.
 
Huyu mzee nilimuona akiwa anataja majina ya mapolisi na wakuu wa wilaya kama sikosei ni wiki mbili zimepita akiwapongeza kwa kazi zao. Ana uCCM kwa hiyo hata mambo ya maana anafanya ya ushabiki. Dr.Kitima hata kama alivaa kaniki yeye anataka Dr aendelee kuvaa kaniki la kifikra kama huyu mzee.
 
Kitima ninavomfahamu mimi ni Padre wa kanisa Katoliki aliyeapa kuachana na mambo yote ya ulimwengu na kuongoza waumini wa kanisa hilo kuelekea mbinguni. Why ajihusishe na siasa za ulimwengu huu? Asubirie waumini waende wakatubu dhambi zao kwake.
 
Hawa watu wa CCM na serikali yao wameshindwa kujua wajibu wa vyuo vikuu kwani wamewekeza kwenye kuwaandaa vijana kupata ajira na si kuwafanya kuwa visima vya fikra, SAUT na Fr Kitima wanayafanya haya ndiyo maana vijana kutoka chuo hiki wako tofauti na vyuo vingine hususani UDSM & UDOM ndiyo maana mzee Farijara anaropoka na kusema hayo yeye anadhani ukisomeshwa na serikali uwe mkimya ndiyo fadhira kwa serikali yako
 
Sasa huyu mzee nahisi akili yake imeshachanganyika na m.a.v.i. Ameshasema Kitima aliishi ktk umaskini na alivaa kaniki.Kwa hiyo Kitima akumbuke fadhila zipi? Angekua aliishi maisha ya kitajiri na kuvaa suti tungesema akumbuke fadhila za kuwezeshwa kuishi maisha hayo ya kifahari. Kama ameishi maisha ya kipigika kuna fadhila kweli anadaiwa hapo na CCM?
 
Sitegemei neno la maana kutoka kwa the so called KADA WA CCM. Maajuza, malofa na wafia tumbo ndio wanachama wenyewe na mtaji wa chama ni ujinga wa wananchi.

Wale wa Mtwara wametandikwa vya kutosha, lkn uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Darajani, wameshinda CCM. Hicho kizee kimeeka ubongo zaidi ya mwili
 
Wazee sasa hawana Busara na ndiyo maana Waziri hajui Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wazee hawasemi kama wanadhalilishwa wamekaa kimya kuhusu hilo. Dr anasema ukweli wanashambulia. Mzee huyo wa Busara angelikemea uozo wote unaofanyika na viongozi na wananchi wa TZ busara zingelionekana na vijana wangelijifunza. Asifangilie chama Mtu anasoma kwa jitihada zake Chama kama kinasomesha wenye kadi za chama wote wangesoma.
 
sasa kilaza kama wewe una hoja gani zaidi ya kutumika tu hapa. Kutwa usiku na mchana unajiongezea vi mia mbili mia mbili kwenye post hapa jf. Leo umeanza mapem hadi mda wa chai utakuwa na ef 3
mkuu jina lako mbona linafanana na kale kamchezo ka walibelari?
 
Mkomamanga; I like it, unajua magamba wanapenda wasomi wawe watumwa wa kifikra na inapotokea msomi anayefikiri kwa ubongo wake na kutoa maoni yake kutokana na hali halisi wanamuona ni adui, hatuwezi kuendelea kwa fikra sawa ni lazima zitofautiane na kila mtu aheshimiwe kwa mawazo yake siyo kumlazimisha afikiri kama wewe. Sasa huyu mzee Fara.jala anataka kama yeye haoni athari za ufisadi, basi kila mtu awe kama yeye!
 
Last edited by a moderator:
katika michango yote ya huyu mzee niliyo wai kumsikliza ni kwamba njaa tu ndio inayo msumbua....na wazee kama hawa sio wa kuwawekea zamana kabisa, kwani anaweza hata kupeleka umbea kwa mke wa mtoto wake...hivyo ni kuwaogopa kama ukoma....mara nyingi anavyo ongea meno ya mbele humtoka kama ngili......
 
Hivi tunatakiwa kushukuru kwa kila kitu kwa sababu ya kutimiza wajibu wako, tena kwa uwezo unaopewa na hao unaodai shukurani zao!?
 
Mkuu chama nilichoandika hapa ni kwa kifupi sana lakini kiujumla alikuwa anazungumzia personal affairs za Dkt. Kitima wakati wakati kipindi kinaanza wamesema atazungumzia bajeti ya mwaka 2013/14.
Unachosema wewe ni kitu tofauti kabisa na kinachofanyika studio kwakuwa hakuna uchambuzi wowote bali wanafanya mashambulizi dhidi ya SAUT na Dkt. Kitima hadi Marine analazimika kusawazisha mambo kwa kutaa vyuo vingine wakati kada mwenzako anazungumzia chuo kimoja tu na mkuu wake.

Shida siku hizi watu wanaweka itikadi kwenye affairs za taifa, na kwa nini huyo mzee Farijala aweke personal affairs kwenye television ya walipa kodi? kama kakosa Influence mwanza asitegemee kwa taifa. Na kwa wale waliozoea kujibu uzi kishabiki bila opinion waende facebook.
 
Mkuu chama nilichoandika hapa ni kwa kifupi sana lakini kiujumla alikuwa anazungumzia personal affairs za Dkt. Kitima wakati wakati kipindi kinaanza wamesema atazungumzia bajeti ya mwaka 2013/14.
Unachosema wewe ni kitu tofauti kabisa na kinachofanyika studio kwakuwa hakuna uchambuzi wowote bali wanafanya mashambulizi dhidi ya SAUT na Dkt. Kitima hadi Marine analazimika kusawazisha mambo kwa kutaa vyuo vingine wakati kada mwenzako anazungumzia chuo kimoja tu na mkuu wake.
Kwani Dr Kitima alikuwepo studio au ndio kipindi kilitayarishwa kumtukana Kitima na chuo cha SAUT
 
Yule kitima ni janga kuu la taifa, mtokwa povu tu. Njaa inamsumbua
Njaa inamsumbua, au anasema ukweli??. Kumbuka Dr. Kitima hagangi njaa. taaluma yake na nafasi yake kama Padre anaweza kuishi popote duniani na akafanya kazi. Kinachomsukuma kusema ukweli ni upendo alionao kwa nchi yake na watanzania. inauma kuona watu wakiishi kwenye umaskini wakati nchi inakila kitu cha kumfanya aishi kwa raha.

CCM mnaogopa kivuli chenu. Dr. Kitima hata siku moja hafikirii kugombea ubunge au urais. acha awafumbue macho vijana.... waje wachukue chao kabla hamjakitorosha chote..... acha vijana wasome SIASA...
 
hawa wote wanajifanya wanasiasa na wako tayari wazo zuri liwapite kwa sababu linakosoa makosa yao ambayo wamekuwa wakiyafanya kwa miaka mingi! Na hawa ndio wana jukumu kubwa la kusimamia utitiri wa rasilimali za nchi hii ambapo nadhani uwezo wao wa kujua anachofuata Obama na Xi Ping hapa Tanzania ni zaidi ya sifuri!
 
Mzee farijalla lazima angetoa tu lawama kwani awezi kushambulia wana ccm kwa sababu kuna madudu mengi nyuma yake ila wajue kuwa ccm imeshikwa pabaya na hawana pakutokea.

Lakini dhana hapa ni ei kwa kuwa ulisoma wakati nyerere alipokuwa Raisi, maisha yako yakabadilika basi huna budi kukubali chochote anachofanya au alichofanya, huwezi kuhoji! Ukiwa mtumwa na Mtwana akakupendelea kidogo ukawa tofauti na wengine basi wewe huwezi tena kuhoji chochote! Huu ndio ugando wa akili! Ni nani asiyejua kuwa binadamu anakua na atakuwa na maendeleo kwa jitihada zake mwenyewe- ni wangapi kwenye nchi zenye neema kibao wameshindwa kujiendeleza wamebaki mibangi tu! VIZEE VINGINE BWANA! Halafu hamjui huyo Kitina! Anafikiri kichwa chake ni chepesi kama chake!
 
FARIJALA, eti nae anajadiliwa humu ! YULE MZEE ANAMFADHAIKO WA MAISHA MAGUMU, akili zake si timamu, hata kuna kipindi niliwahi kumuona Radio Free Afrika , na siku hiyo aliibuka na matusi dhidi ya Mengi hadi ikafikia hatua ya RFA kuomba radhi.
Nilichogundua, ni Nape Nnauye ndio yuko nyuma ya yule mzee, huwa wanamuombea vipindi TV mbalimbali.
Nakumbuka hiyo siku ambayo huyo Babu alichafua hali ya hewa Star TV. Wazee waliobaki ni Warioba, Butiku na Bomani tu hawa wengine "wazee vijana"
 
Back
Top Bottom