Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Mkapa uliipokea nchi 1995 ikiwa na mzigo wa madeni Hazina ya Taifa ikiwa haina kitu.
Ulitushauri tufunge mkanda lkn ukasahau kutuambia kuifungua au hata kuilegeza.Ukakusanya kodi,ukalipa madeni ya ndani na nje ukairudishia nchi yetu Heshima ya kukopesheka na pia heshima ya mfanyakazi aliyekuwa amenyang'anywa heshima hiyo na mfanyabiashara.
Pia ulidhibiti mfumuko wa bei kwa kipindi chote cha miaka kumi.Wafanyakazi wakawa wanalipwa mishahara kwa wakati.
Ulilinda heshima ya chama chako kama mwenyekiti mwenye kauli yenye kuheshimika.Hukuwa unachekacheka na wachafuzi wa hali ya hewa.
Ulijenga barabara zinazoonekana kwa macho sio zakutangaziwa kwenye vyombo vya habari kwa gharama kubwa wakati wanafunzi wanakaa chini.
Ulijenga Bunge la kisasa ambalo Wasira na Komba wanachapa usingizi huku wengine wakiimba kawimbo ka Ndiooooooooo!!!
Ulinunua Rada na Ndege ya Rais ambayo hukuitumia japo Chenge na Mramba walikuzunguka
ulijenga majengo pacha ya kutega uchumi japo kaganji kalikuwepo kiana.
Hayo yote na mambo mengine uliyoyafanya yalikufanya uzunguke nchi nzima kuwaaga watanzania ukiwa kifua mbele ukiwaaminisha unakwenda kulima ukapewa zawadi mbalimbali kitu ambacho MRITHI wako hatathubutu kabisa maana hakuna mwenye shida nae kwani hana lakuwaambia watz.
Sasa Baba Mkapa ulikosea wapi kinachokusababisha ukose heshima ya kuingilia kati matatizo yanayolikumba Taifa letu walau kumshauri Jk au vyombo vya dola na msajili wa vyama vya siasa pamoja na viongozi wa vyama vyetu vya siasa au hata Bunge letu na matamko tata ya mawaziri wetu chini ya Pinda? Au na wewe unakubaliana na kauli ya Pinda kuwa Wananchi wapiga kura WAPIGWE TU KWAKUWA CCM IMECHOKA KUONGOZA?