Mzazi mpime mwanao mimba kabla hajaenda shule

Ushauri ni kuwa mkamtafute muhusika mumuulize ana mpango gani na mzigo wake? Tujue wazo lake ni lipi?
 
Mzee...Polee ila
Usitutie majaribuni kwa Mola wala Jamhuri,
Lea watoto wote.

SAUTI SOL - NELEA Feat AMOS & JOSH
 
Pole sana mkuu, kwa hili sina la kukushauri ingawa nina mengi ya kusema.
 
Kanunue beseni, nepi, Pampers za dyker, sabuni, mafuta, taulo, dishi na vingine.

Usitoe mimba ulee mtoto, ukitoa mimba utalea mdoli na kulea wa wengine.
 
Eti ana ujauzito wa wiki 6 na binti hajaambiwa, nikisema umetumia nini kujua kuwa mimba ina mwezi mmoja na wiki mbili sijui utanipa jibu gani? mkuu kuwa serious, unafanya muda mwingine tuhisi mada haina uhalisia. Anyway kaka tuachane na hayo, twende ktk mada mwanaume mwenzangu ili tuchambue kidogo.

Mtoto kuzaa mapema kwa kipindi hiki huko mbeleni kwaweza msababishia matatizo ktk shingo ya kizazi, inaweza ikapelekea hata kansa.

Kikubwa jaribuni kukaa na mtoto na kumuahidi mtakuwa nae begabega, hii itasaidia asichukue maamuzi mazito kama Abortion ya kienyeji, kutoroka nyumbani, kujiua n.k

Muda mwingine ktk kesi kama hii kwa faida ya familia na mtoto Abortion kwa kutumia bomba ni suluhisho bora kabisa, hizi dawa za misopristol unless awe chini ya uangalizi wa Doctor na miso kwa umri wa huyo binti sio nzuri maana kizazi bado hakijakomaa sana, ila Abortion ni dhambi mbele za Mungu.

Kimwili umetatua tatizo ila kiroho tayar kumeshapasuka.

Mkuu, leeni tu hiyo mimba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdogo wng anaenifuata alipata ujauzito akiwa form two, ilileta tafrani Kwenye familia kwakuwa aliyempa mimba alikuwa kijana asiyeeleweka na familia yao nilikuwa duni sana na kijana alikimbia, so mimba ililelewa na akajifungua badae akapiga QT na akaendelea na certificate na diploma kwasasa anafanya kazi kampuni flani na alishaolewa anafamilia, mwanae ninae kwangu anasoma dalasa la sita maisha yanaendelea so lazma hapo mtulie vinginevyo mimba itatolewa!

Sent using kidole gumba
 
Binti hajaambiwa?Mlimpaje bila yeye kujua?Mlichukuaje mkojo wake?

Why asiulizwe? Apate mimba na muogope kumuuliza?..hizi story za kutunga?
Jf ina watu wenye uelewa mpana, hahaha binti hajaambiwa kama ana mimba, tena wao wamejua kuwa ina wiki 6. Binti kutojijua ninaweza nikaelewa lakini najaribu kutafakari wao wamejuaje mimba ina umri huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichojifunza tangu kufungwa kwa shule hapa Bongo ni kuwa wazazi wengi ni mbumbumbu wa kulea mabinti zao na wanawaachia walimu kuwalelea ndo maana kelele za mimba zimetawala kila mzazi akiomba watoto waende shule.
Kuna wengine wameshindwa hata kudhibiti misele isiyo ya lazima kwa watoto wao ndo maana vitoto vinazurura mitaa yote mithiri ya mbwa wanaopandana.

Lakini ni wazazi hawa hawa wanaowaponda walimu kila kukicha hali ndo wanaowalea watoto na kuwakinga na mimba za utotoni.

Sasa wacha walee na japo kwa miezi sita tu halafu tuone wangapi watabeba mimba na wangapi watavuta bangi na kukwaa ngoma
 
Niliwahi andika humu wakati wa corona

Wazazi kuweni makini sana, kuna ngono zembe inafanyika jamaani

Yaan watoto wengi watafungua wakiwa ama na MIMBA au MAGONJWA MAKUBWA MAKUBWA yaenezwayo kwanjia ya ngono hususani HIV.



Nawasihi sana, wazazi Fanyeni mnaloweza kuwalinda watoto .


Serikali nadhan itumie vyombo vya habari kuanzisha upya kampeni kabambeee , nakuhakikisha wanatoa elimu ya jinsia pamoja na uwepo wa Kondomu na matumizi yake.



KUNA NGONO ZEMBE INAFANYWA KIPINDI HIKI SIJAWAHI ONA.






Mtoto anatakiwa kuendelea na shule.


Wazazi watumia Hekima sana kuongea na mtoto ,hapa Mama mzazi atumie akili sana kuongea naye kama mtu na shoga yake atatajiwa alompa mimba.



Mkishatajiwa... MIAKA 30 ni mingi mnooo nausikute kapewa na mtoto mwenzake., na huyo kijana anaweza naye KUJIUA ...maana ndio vijana waleo.

Mkae kama wazazi pamoja, Mjadili... Kikubwa MPIGISHANE FAINI TU basi muokoane .. miaka 30 ni mingi mnooo , kuna hapo atajiua au kutorokea pasipojulikana.


Wazazi wabinti wakishamjua kijana alompa mimba, wawaite wazazi hao kwao ..wasiende kwao na kijana ( yaan kijana hapa ikiwezekana asijue au ajue kupitia wazazi wake baada ya kua wameshapata Solution na wazazi wa binti )......


(kama ni kijamaaa sio kitoto ,hakisomi, ni kihuni tuuu chenye akili timamu, basi kipigwe iyo 30 , Kua fundisho kwa wengine)



YOTE KWA YOTE MIMBA IWE TERMINATED !!........ dawa wanauza 35--50 tena iyo ni masaa tu inatemeka . Hosp ukimpata mwana , basi unampa chake anawasaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom