Mzazi mpime mwanao mimba kabla hajaenda shule

IKIRIRI

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
2,673
2,000
Wazazi wenzangu nawasihi sana shule zikifunguliwa jitahidi umpime mimba mwanao unaweza mpeleka hospital.

Watoto wa siku hizi hawaaminiki hata kidogo, ni vema uchukue tahadhari mapema kabla ya hatari

Ikitokea ana mimba ni rahisi kuchukua hatua kabla haijagundulika shuleni\

======
UPDATE
======

Jana nilitoa uzi hapa juu ya wazazi kuwapima watoto ujauzito. Nimepata DM kutoka kwa member mwenzetu kaenda kuwacheck watoto wake. Imetokea mwanae wa kidato cha 2 anaujauzito wa wiki 6.

Sasa kaniuliza afanyaje au achukue hatua gani? Mpaka sasa binti ajaambiwa pia mtoto anasoma shule ya gharama kubwa sana.

Naomba ushauri kwa niaba yake, mimi nimeamua kulileta hapa ili apate mawazo ya watu wengi.
 

Hamdan

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
350
500
Mimi naona wazazi wangejikita zaidi katika kuwachunga watoto zao, ili wasije kufikia huko.

Kuliko kusubiri kuja kuwapima mimba.

Na hii ndio tahadhari nzuri, maana mimba hata kama mtoto ataificha itajulikana tu, labda aitoe.
 

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
3,224
2,000
Afu hii ni kweli Alhamis iliyopita kuna mmama alienda kumchukua bint yake baada ya kupigiwa simu na kaka yake(mjomba) kuwa mtoto wake anaumwa na alipopewa pesa ya kwenda hospital vipimo vinaonesha ana malaria na ametumia dawa lakini hapati nafuu.

Yule mama alipoenda kumchukua moja kwa moja akaja kwenye kituo chetu baada ya kuchukua history jambo la kwanza kumshauri yule mama bint apimwe kipimo cha mimba yule mama alikubali majibu kutuka presha ilipanda nusura yawe makubwa bint wa miaka 16 ni mjamzito...kilichoendelea sijajua hukowaendako.


WAZAZI PIMENI MABINTI ZENU MAPEMA

Sent using Jamii Forums mobile app
 

GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
4,716
2,000
Mabazazi yamejaa humu yanakodoa tu.

Kila uzi unaoletwa humu unahamasisha kuwaharibu watoto na wanafunzi.

Mara sijui kula kimasihara... lakini watu wanaona sawa tu. Na wengine ni wazazi lakini wanashangilia kama machizi.

Wengine wanawalawiti watoto wao wa kuwazaa. Wapo humu wanapongezana na kushangilia.

Unaweza ukaona ni jinsi gani tulivyo na jamii ya sexual deviants, wafiraji, wanajisi na waharibifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

IKIRIRI

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
2,673
2,000
Sijajua mahusiano ya uzi na ujumbe wako
Mabazazi yamejaa humu yanakodoa tu.

Kila uzi unaoletwa humu unahamasisha kuwaharibu watoto na wanafunzi.

Mara sijui kula kimasihara... lakini watu wanaona sawa tu. Na wengine ni wazazi lakini wanashangilia kama machizi.

Wengine wanawalawiti watoto wao wa kuwazaa. Wapo humu wanapongezana na kushangilia.

Unaweza ukaona ni jinsi gani tulivyo na jamii ya sexual deviants, wafiraji, wanajisi na waharibifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom