Mzazi kuaanza kukutegemea wewe kwa kila kitu bila kujali mshahara wako mdogo

Ni wajibu wa lazima pia mtoto kumhudumia mzazi.

Wewe unataja eti sio wajibu wa kisheria hiyo sheria unayosema ni ya nani??
Inategemea wazazi bado wana nguvu kiasi gani kama bado wana nguvu za kujitafutia riziki sio vizuri kumtwisha mizigo mtoto.
 
Unacho sema ni kweli kabisa,kuna wazazi wengine bado wana nguvu ya kufanya kazi za kujiingizia kipato au kulima,lakini mtoto wao akisha pata kazi basi hawataki kufanya kazi, hawataki kwenda kulima tena.Kuwa tunza wazazi unaweza kuwatunza kutokana na mazingira mfano wazazi wamezeeka sana hawana tena nguvu za kujiudumia,tofati na hapo mzazi unakuwa una Fanya makosa makubwa sana unapomtwisha mtoto majukumu ya kukutunza na wakati uwezo wa kujitunza unao.
 
Inategemea wazazi bado wana nguvu kiasi gani kama bado wana nguvu za kujitafutia riziki sio vizuri kumtwisha mizigo mtoto.
Mzazi ni mzazi tu, kama alivyo mtoto kwa wazazi hakui.

Wawe na nguvu ama la! Ni wajibu wa lazima mtoto kumwangalia mzazi.

Japo wazazi wanapokuwa wazee wajibu huu unatakiwa uzidi.

Kwenye uislamu:
Allah anasema kwenye qur an

Surat luqman "tumemuusia mwanadamu kuwatendea wema/ihsani wazazi wawili.
Mwanadamu huwenda akajiuliza kwanini kuwatendea ihsani, allah anajibu kwenye hii hii aya mbele anasema" mama kambeba miezi tisa na kumnyonyesha miaka miwili basi nishukuruni mimi mola(allah) na wazazi wako wawili.
Utaona hapo allah kwenye surat luqman ametoa usia kwa mtoto juu ya wazazi wake wawili.

Surat israa(surat israil)
Allah anasema "amemrisha mola wako/amekata shauri mola wako kuwa umuabudu yeye(allah) na kuwatendea ihsani wazazi wawili ima akifika uzee mmoja wao au wote wawili basi ushushe huruma juu yao na wala usiwaambie" uffih"(usitoe mguno au kugeuza shingo pale wanapokuagiza ama kukwambia jambo, badala yake na useme "mola wangu wape huruma wazee wangu kama walivyokuwa wakinihurumia mimi nikiwa mdogo"
Hapa utaona mtoto hana hiyari juu ya kuwatizama na kuwahudumia wazazi wawili.

Wallahu a'alam
 
vijana wenzangu ningependa tuweksne sawa katika hili swala ambalo lina tukuta weng

kwa mfano umepata kazi wazazi nao wanategemea sana wewe kupata kazi baada baada ya wewe kapata kazi kuna maisha yako inatakiwa uyatengeneza changamoto ina kuja hapa mzazi mzazi akishajua kwamba umeshapata kazi hapo ndipo changamoto zinaanza

mzazi anaanza kuku tegemea wew kwakila kitu bila kujali mshara wako Mdogo pia afikilii kwamba nawew unahitaji kutengeneza maisha yako kwanza

hatukatai kumsaidia mzazi nilazima lakini kuna muda unaweza jikuta kwenye maisha unakwama malengo yako yana potea bila kujua nini chanzo kumbe hata wazazi wana changia wakisha jua mwisho wamwezi umekaria sim zinaanza zakuomba Pesa unajikuta malengo ulopanga kwamba nikipokea mshahara nifanye hiki unavuruga unamtumia mzazi usipo mtumia lawama kama zote

jamani wazi mtuache kwanza makampuni yenyewe saivi wana lipa mishahara midogo pengine hata Mimi mahitaji yangu haunisholezi tushsulisne hapa Vijana wenzangu hasa sisi tunao anza maisha tuwekane sawa by Fundy_samwely_tz
Andaa Kiasi ambacho Utakuwa unawapa bila kuaribu ratiba zako, usisaidia kupitiliza uwezo wako !! Siku huna waambie huna..., lawama hazijawai kuisha duniani
 
Mzazi ni mzazi tu, kama alivyo mtoto kwa wazazi hakui.

Wawe na nguvu ama la! Ni wajibu wa lazima mtoto kumwangalia mzazi.

Japo wazazi wanapokuwa wazee wajibu huu unatakiwa uzidi.

Kwenye uislamu:
Allah anasema kwenye qur an

Surat luqman "tumemuusia mwanadamu kuwatendea wema/ihsani wazazi wawili.
Mwanadamu huwenda akajiuliza kwanini kuwatendea ihsani, allah anajibu kwenye hii hii aya mbele anasema" mama kambeba miezi tisa na kumnyonyesha miaka miwili basi nishukuruni mimi mola(allah) na wazazi wako wawili.
Utaona hapo allah kwenye surat luqman ametoa usia kwa mtoto juu ya wazazi wake wawili.

Surat israa(surat israil)
Allah anasema "amemrisha mola wako/amekata shauri mola wako kuwa umuabudu yeye(allah) na kuwatendea ihsani wazazi wawili ima akifika uzee mmoja wao au wote wawili basi ushushe huruma juu yao na wala usiwaambie" uffih"(usitoe mguno au kugeuza shingo pale wanapokuagiza ama kukwambia jambo, badala yake na useme "mola wangu wape huruma wazee wangu kama walivyokuwa wakinihurumia mimi nikiwa mdogo"
Hapa utaona mtoto hana hiyari juu ya kuwatizama na kuwahudumia wazazi wawili.

Wallahu a'alam
Hata mimi ni Islaam na hicho kifungu cha haya ya Qruan nina kielewa sana,lakini wewe kama mzazi una takiwa kuangalia mazingira ya huyo mtoto unaye mtwisha majukumu ya kukulea.Haiwezekani una mashamba ya kulima na nguvu za kulima unazo lakini hutaki kufanya kazi eti kwa sababu mwanao ana kazi,na hata mwenyezi mungu na mtume wetu sidhani kama ana kubaliana na hili jambo.Lakini pia ukijaribu kuangalia kifungu hichi cha Qruan tukufu kina sisitiza zaidi kuwanyenyekea na kuwaheshimu wazazi na si kuwa tunza.
Nina sisitiza mzazi unapo kuwa na nguvu za kufanya kazi na kujiingizia kipato hutakiwi kumbebesha mtoto majukumu ya kukutunza na wakati uwezo was kujitunza unao.
 
Naam

Unajua kwa nini qur an imetumia neno "ihsani"badala ya wema?? Kwenye jambo la mzazi.

Tujifunze kwanza maana ya neno ihsani":
Ihsani maana yake ni kufanya jambo kwa ubora wa kiwango/perfection.

Mzazi hafanyiwi wema peke yake bali wema wa hali ya juu/ubora wa kiwango.

Ngoja nikupe mfano wa wema na ihsani:

Siku moja mtume wa allah alikuwa akitembea katika njia ghafla akakutana na bibi kized akilalama asaidiwd kutwishwa mzigo wake kichwani, basi kila anaepita wala hana habari nae, basi alipotokeza mtume wa allah akamsikia yule bibi akiomba msaada wa kutwishwa mzigo.
Basi mtume wa allah sio kumtwisha yule bibi bali aliamua yeye kubeba mzigo ule hadi nyumban kwa bibi yule.

Nataka nikwambie nini?

Hapa kumwisha yule bibi mzigo ilikuwa ni husna/hassana(wema) ila ihsani ni pale alipoamua kumbebea kabisa yule bibi mzigo wake hadi nyumbani.
Hapa tunasema mtume amefanya ihsani, yaani wema uliovuka mipaka.

Sasa allah ameamrisha kuwafanyia wazee wako wema wa hali ya juu sana, yaani uwafanyie ihsani ambayo ni pamoja na kuwatizama kwa hali na mali kipindi chote cha uhai wao na hili sio ombi bali ni wajibu walazima kama qur an inavyosema surat israa kuwa mola wako "amekuamrisha/amekata shauri, huna hiyari juu ya hili.
 
Tunajukumu la kuwatunza na kuwalea watoto tuliowaleta duniani, kumsaidia mzazi ni fadhila ya malezi aliyokupa lakini si jukumu.
Mkuu sky, ujue nakutatazamaga kama role model.
Kwa jibu hili ulilolitoa ni lako kweli, au mtu kaku'haki'?

Mbona umetoa jibu jepesi namna hiyo?

Ulitakiwa uingie uchimbue! Mada hii hauwezi kuweka jibu jepesi namna hiyo ukawa umemaliza.

Embu nikuulize, ingawa sielewi umri wako halisi.

Kwa mfano wazazi wako Mungu kawajaalia maisha marefu, wote kwa pa1 ama m1 wao hadi kufikia 85 ama 100, utakubali watunzwe na 'cancel' kwenye nyumba za kulelea wazee wasiojiweza wewe ukiwepo?

Wazazi wanaweza kuwa na uwezo wa mali, lakini umri unavyopinda, uwezo wa kuji'kontroo' hutoweka na kubaki tegemezi kama walivyo watoto wadogo!

Kwa hiyo ni jukumu la mtoto kuwasimamia na kuwatunza wazazi wake kwa hali na mali.

Ingawa mtoa mada kalenga wazazi vijana na wewe ukalenga hukohuko nadhani na kusahau kuwasemea wazazi wenye uhitaji maalumu kwa sababu za kimazingira juu ya umri wao, ulemavu, nk nk.
 
Sijasema tuwakimbie wazazi, kama wazazi wamefika miaka 90-100 inamaana na watoto wao watakua kwenye retirement age, kama huna majukumu ya kazi na una miradi inayokuingizia pesa, sioni sababu ya kuto watunza wazazi.

Changamoto langu kubwa ni kwa wazazi ambao wako kwenye 60, mtoto wao ndiyo anaanza maisha yuko kwenye 30 anahitaji kujenga maisha na kusomesha watoto. Wazazi hawa wameweka miguu juu wanasubiri posho kila mwezi.
 
mzazi anapaswa kumpa mtoto wake mahitji yote muhimu ikiwa ni pamoja na elimu pia mzazi anapaswa kuweka akiba kwa ajili ya uzeeni.
Suala la kumhudumia mzazi kwa Kila kitu baada ya kijana kupata kazi ni chanzo cha UMASKINI wa kudumu kwa kijana.
Baada ya kijana kupata kazi kijana anatakiwa kujipanga kimaisha ikiwa ni pamoja na uwekezaji ili kuwaandalia watoto wako mazingira mazuri yatakayowasaidia kufanikisha malengo yao na kuepuka suala la umasikini
Kuwasaidia wazazi. Kama wazazi wako ni wazee sana au ni wagonjwa kiasi cha kushindwa kuzalisha unapaswa kuwatunza. lakini kama wanauwezo wa kufanya kazi mfano kulima wakalime aisee
Umasikini wa kudumu. wazee wetu wamejenga nyumba au kununua gari kwa hela za kustafu (pensions) kwa sababu pindi wanafanya kazi waliendeleza kasumba ya kusaidia wazazi , ndugu na marafiki mwisho wa siku wakastafu utumishi with nothing.
Kulipa fadhila kwa wazazi. wazazi kwa utashi na raha yao watu wawili waliamua kunizaa wakijua wanauwezo wa kunitunza na ni wajibu wao kufanya hivo sio deni kwamba walinizaa sasa niwalipe kwa kuwapa gawio kwenye mshahara wangu. ukiendekeza mambo haya utakufa maskini
Kwenye ukingo wa thim. mwandishi wa kitabu kwenye ukingo wa thim" aliwahikusema " mila na tamaduni kandamizi za kiafrika zimefika ukingoni lesoni ya wasabato ya tarehe 2 April lilisema tujiandae kwa mabadiliko.
Ushauri wangu. wazazi wafanye kazi vijana wajipange ujanani wasije kuwa Mizigo kwa watoto wao.
 
Sijasema tuwakimbie wazazi, kama wazazi wamefika miaka 90-100 inamaana na watoto wao watakua kwenye retirement age, kama huna majukumu ya kazi na una miradi inayokuingizia pesa, sioni sababu ya kuto watunza wazazi.

Changamoto langu kubwa ni kwa wazazi ambao wako kwenye 60, mtoto wao ndiyo anaanza maisha yuko kwenye 30 anahitaji kujenga maisha na kusomesha watoto. Wazazi hawa wameweka miguu juu wanasubiri posho kila mwezi.
Hapo sawa. Nilitamani udadavue hivyo.
 
  • Thanks
Reactions: RTI
Naam

Unajua kwa nini qur an imetumia neno "ihsani"badala ya wema?? Kwenye jambo la mzazi.

Tujifunze kwanza maana ya neno ihsani":
Ihsani maana yake ni kufanya jambo kwa ubora wa kiwango/perfection.

Mzazi hafanyiwi wema peke yake bali wema wa hali ya juu/ubora wa kiwango.

Ngoja nikupe mfano wa wema na ihsani:

Siku moja mtume wa allah alikuwa akitembea katika njia ghafla akakutana na bibi kized akilalama asaidiwd kutwishwa mzigo wake kichwani, basi kila anaepita wala hana habari nae, basi alipotokeza mtume wa allah akamsikia yule bibi akiomba msaada wa kutwishwa mzigo.
Basi mtume wa allah sio kumtwisha yule bibi bali aliamua yeye kubeba mzigo ule hadi nyumban kwa bibi yule.

Nataka nikwambie nini?

Hapa kumwisha yule bibi mzigo ilikuwa ni husna/hassana(wema) ila ihsani ni pale alipoamua kumbebea kabisa yule bibi mzigo wake hadi nyumbani.
Hapa tunasema mtume amefanya ihsani, yaani wema uliovuka mipaka.

Sasa allah ameamrisha kuwafanyia wazee wako wema wa hali ya juu sana, yaani uwafanyie ihsani ambayo ni pamoja na kuwatizama kwa hali na mali kipindi chote cha uhai wao na hili sio ombi bali ni wajibu walazima kama qur an inavyosema surat israa kuwa mola wako "amekuamrisha/amekata shauri, huna hiyari juu ya hili.
Hasante sana kwa elimu kubwa ulionipa,lakini hiyo hisani anatakiwa aifanye kama atakuwa na uwezo wa kufanya, mfano Mimi ni kijana wa miaka 23 na wazazazi wangu bado ni watu wenye nguvu na baba yangu ana mashamba makubwa sana ya kahawa na migomba kwa hiyo hana shida yeyote, lakini Mimi nikitaka kwenda nyumbani siwezi kwenda mikono mitupu eti kwa sababu wazee wangu wana uwezo ni lazima niwanunulie mizawadi kama njia ya kuonesha upendo kwa wazazi wangu, Mimi nina dhani hiyo ndio hisani nzuri zaidi kuliko hii ya kulazimisha mtoto akuletee kila kitu wakati uwezo wa kufanya kazi unao. Yaani mtoto akununulie chakula wakati mashamba ya kulima na ukapata chakula na mengine kuuza yapo ,akununulie sabuni,nguo,ukiumwa akununulie dawa,chumvi,sukali,na huyo unaye tegemea akununulie hivyo vitu mshahala wake ni 500,000 kwa mwezi alafu anaishi kwenye jiji kama dar anatakiwa alipie maji,chumba ,chakula,nguo,usafiri wa kila siku wa kwenda na kurudi kazini,bado anatakiwa ajiwekee akiba kwa ajili ya matibabu iwapo ata umwa au tatizo la ghafla litakalo mkuta.Kwa hiyo kama mzazi kabla ujataka kufanyiwa hisani una takiwa uangalie je huyo anaye taka akufanyie hisani anao huo uwezo wa kukufanyia hishani?lakini pia Mwenyezi mungu ana wachukia wasio taka kufanya kazi wakati uwezo wa kufanya kazi wanao,bila shaka hayo ndio maoni yangu kuhusu hisani kama kuna sehemu nimekosea ninaomba iniweke sawa kwa sababu wewe unaonekana ni mtu mwenye elimu ya kidini kunizidi Mimi.
 
Uislam haukuwahi kumtweza mtu nguvu, kumlazimisha kufanya jambo nje ya uwezo wake.

Hili la kuhudumia wazee ni jukumu la wajibu lakini linakwenda sambamba na uwezo wa huyo mtoto, sio wewe unakula kuku wao mlenda wale mlenda tu ikiwa wanapenda kufanya hivi.

Ila la muhimu hakikisha unayafanya majukumu haya ya kuwatunza wazazi kwa uwezo wako wote(to the maximum) kwani hii ndio maana halisi ya ihsani na allah atakulipa ujira mkubwa sana hapa duniani na kesho akhera.

Na uyafanye haya juu ya wazazi wako bila malalamiko, sijui mama hivi sijui baba hivi. Fanya bila ya kulalama na ujione fahari kuwahudumia wazee wako wakati wako hai.

Mtume wa allah asema"amepata hasara, amepata hasara, amepata hasara/pua yake imegusa mchanga(ameangukia pua) yule ambaye ataishi na wazazi wake kisha wazaza wake wakafika uzee na kufa na isiwe sababu ya yeye kupata pepo"kwa ihsani hii kwa wazazi.

Kumbuka:
Mali ulizonazo ni za wazazi wako pia
Kuna swahaba aliwahi kwenda kumshtakia mzee wake kwa mtume kuwa "baba yangu amekuja nyumbani kwangu amechukua hiki na kile bila ruhusa yangu, nifanyaje??"
Mtume wa allah akajibu "anta wamaluka liabika" (wewe na mali zako ni za baba ako)
 
ukweli ni kwamba mtoto kumtendea jambo mzazi ni hiari lakini mzazi kumtendea mtoto jambo ni lazima....kwa mzazi anayejitambua sawa sawa hawezi kumuegemea mwanae kwa kila jambo na kutokana na mzazi kumuegemea mtoto kamwe umasikini hauwezi isha katika koo unakuta wewe unafamilia na pia unawadogo zako kama wawili alaf tena na mkeo anawadogo zake na pia mna wazazi hao wote wanawatazama ninyi hapo uwezi endelea mzazi anapaswa aandae maisha ya wanawe na yake ya baadae ila mtoto anapaswa pia awe na mchango wa kama 2% kwa mzazi wake kama kulipa fadhila ila kwa Africa mzazi anataka msaada wa 95% toka kwa mtoto hii ni hatari sana
 
Tunajukumu la kuwatunza na kuwalea watoto tuliowaleta duniani, kumsaidia mzazi ni fadhila ya malezi aliyokupa lakini si jukumu.
Watoto wote mtakuwa wazee,mtachoka kwa umri na magonjwa yanayoletwa na uzee,watoto wako wakikupa jibu hili utawaelewa?
 
Tunajukumu la kuwatunza na kuwalea watoto tuliowaleta duniani, kumsaidia mzazi ni fadhila ya malezi aliyokupa lakini si jukumu.
Yaani wewe una jukumu la kulea watoto wako lakini kuwasaidia waliokulea isiwe jukumu?Kama wazazi wako wanajiweza sio jukumu lakini kama hawajiwezi basi ni jukumu lako.
 
Sijuwi na mzazi angesononeka kama wewe hatuelewi ungeishia wapi...Very sad...
 
Yaani wewe una jukumu la kulea watoto wako lakini kuwasaidia waliokulea isiwe jukumu?Kama wazazi wako wanajiweza sio jukumu lakini kama hawajiwezi basi ni jukumu lako.
Ninajaribu kueleza hapa, tunayaona maisha yalivyo magumu, tujitahidi tusije kuwa tegemezi kwa watoto wetu.
 
Una uhakika usingewasaidia wazazi wako ungefanikiwa sana na kwa haraka?.Kuna wazazi walikuwa na uwezo lakini hawakuwapa watoto wao hiyo elimu waliyokupa,inawezekana wazazi wako wamejinyima sana na kuingia madeni makubwa ili wewe ufike ulipo.Kwa Waafrika kusaidia wazazi ni jambo la lazima na la kimaadili,achaneni na uzungu usiofiti kwenye mazingira yetu.Faida gani kwako mzazi wako apelekwe kwenye nyumba ya wazee na una uwezo wa kumhudumia kwa kugawana naye kidogo unachopata.Kwa roho yako hiyo laiti usingesoma,na wazazi wako wangekuwa na mali ungeweza hata kuwaua,ili umiliki mali na uonekane mwenye mafanikio.
 
Umeone eee kitu chamsing sana ila waafrica tuna pondana tena unajua mzazi nimtu wamuhimu sana nivingi anakua amekusaidia ikiwemo kukulea mpka umefikia hapo so mzazi huyohuyo isiwe kikwazo kwako cha wewe kufanikiwa kuwa
Mafanikio hayaji kwa kuwatelekeza wazazi, hivi mafanikio ni kijinyima na kula mihogo
 
Back
Top Bottom