Mzazi jifunze kumuomba mwanao msamaha

Mzazi jifunze kumuomba mwanao msamaha

RAGNAR LOTH

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
698
Reaction score
1,613
Wengi tumewahi kutamkiwa / kuwatamkia watoto maneno makali au machafu ambayo baadae tukiyatafakari hatuamini kama hayo maneno yametoka vinywani kwetu. Ni mara nyingi tunatamkiana maneno kama
" Wewe ni hasara tupu ",
" Mbwa kabisa wewe,"
" bora nisingekuzaa huna faida hata chembe,"
" Ntakupa laana ya milele" na mengine mengi mabaya kuliko hata haya.

Ikiwa wewe ni mzazi bado ni binadamu, na katika hali ya kawaida binadamu huwakosea wanaomzunguka akiwemo mtoto. Fahamu kuwa kuomba msamaha kwa mtoto unapokosea ni jambo la busara na hasa unapogudua umemkosea na imemuumiza, inajenga pia fikra chanya kwa mtoto.


Tambua kuwa :
-Msamaha haukunyimi haki yako kama mzazi.
-Msamaha hujenga dhana ya kuheshiamiana amabyo ni moja ya malezi bora kwa mtoto,


Wazazi wa kiafrika hasa wabongo hii kitu si rahisi sana kwenu / kwetu, tumejawa na majivuno, ukaidi na udictator usio na maana tukiamini sisi ni malaika hatukosei.

Je wewe waweza kuomba msamaha unapohisi umemkosea mwanao? Mara ngapi umejishusha kwa kutambua makosa yako?
 
Katika child psychology wanafundisha kuwa jinsi unavyoongea na mtoto ndiyo unavyompa confidence ya kusimamia hoja na kuweka argument iliyoeleweka. Watoto wengi wanaozaliwa na wazazi wenye upeo wa elimu wanafundishwa mawasiliano tangia wakiwa wadogo. Mtoto anavyookuliza swali ni kuwa ana explore the world around himself/herself, wazazi wengine wanaona kero unamwambia mtoto nyamaza huko, kisa anauliza kwanini yule dada wa kwenye TV siwezi kumgusa, unampomjibu mtoto swali anaregister kwenye akili yake.
 
Katika child psychology wanafundisha kuwa jinsi unavyoongea na mtoto ndiyo unavyompa confidence ya kusimamia hoja na kuweka argument iliyoeleweka.

Sisi huwa hatuwapi hiyo confidence instead tunawa offend, sjui kwa lengo lipi hasa.
 
Back
Top Bottom