Pre-form One ya nini tena?

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
852
Dear walimu wa watoto wetu,

Wazazi wote wa wahitimu wa darasa la saba wako wanakimbizana kupata shule bora za watoto wetu. Na hii imekuwa biashara nzuri hasa kwa wenye shule.

Shule inatambua kabisa kuwa ina nafasi 120 za kidato cha kwanza, lakini inafanyisha usahili watoto 4,000.

Mnapata income ya watoto 4,000 kwa 30,000 sawa na mil 120. Alafu mnatoa matokeo baada ya siku mbili. Mmesahisha kwa umakini na kutoa majibu. Aksanteni sana.

Baada ya kupata hii cream bora kabisa, mnakuja kutuambia waje pre form one. Pre form one ya nini walimu wetu?

1. Sylabus ya form 1 imewekwa kwa mwaka 1, January to December. Kwa nini muda hautoshi?

2. Na sisi tulisoma, tena kayumba tulitumia miezi 4 ya kwanza kufanya English Course kabla ya kuanza masomo ya form one na tulimaliza vema kabisa.

3. Mmechukua cream kati ya watoto 4,000. Mna haraka gani kuwafanyia pre form one. Mngesema mnachukua watoto waliofeli na wasio na uwezo ndio mnawafanyia pre form one tungeona mna ukweli.

Sisi wazazi tunaruhusu huu utaratibu kuwa rasmi na kimsingi tunasahau kuwa hizi ni biashara za shule za private kuendelea kusumbua:

1. Watoto wanakosa kupumzika na kupata nafasi ya akili kupumua, mwisho wa siku tunapata wasomi waliochoka na hawana ari ya kazi

2. Wazazi wanalipa ada ya pre form one na form one baadaye. Ni hasara kwa wazazi kwa kuwa Hakuna hela ya kuchezea kwa sasa.

Imefika mahali shule zianze kuomba vibali vya kuendesha pre form one kwa watoto na iwe kwa ajili ya watoto wenye uwezo mdogo kama msaada na sio biashara ya kuingiza kipato kwa kuwachosha watoto na kutia hasara wazazi.

Mzazi mtazamaji

Pia soma: Waziri wa elimu tusaidie. Wazazi tunateseka.
 
Kwa mawazo yangu pre form one ilifaa sana kwa Wanafunziwanaotoka shule za serikali maarufu kama Kayumba.!Faida zake ni nyingi sana kwao

1. Wapate utangulizi wa Lugha ya kufundishia sekondari ambayo ni kiingereza

2. Wanafunzi wanapata muda angalau wa kufundishwa namna ya kujitambulisha kwa Kiingereza!(Self introduction)

3. Ikumbukwe wanafunzi wanaotoka Kayumba hawapati nafasi ya kufikiwa na walimu kutokana na wingi wao darasani so kupitia pre form one mwanafunzi huyu ataweza angalau kupata nafasi ya kuongea kiingereza kidogo.

4. Kijamii,Watoto kwenda pre form one ina faida sana maana maisha yetu tunajuana wenyewe Baba anatoka MAMA naye anatoka Mtoto akikaa mazingira ya nyumbani bila usimamizi wa karibu kwa miezi miwili kuna ambao watafika January ni Wajawazito TAYARI.

Ila akiwa kwenye mazingira ya kwenda kusoma pre form one angalau anakuwa busy na shule hata kusahau mambo ya shuleni inakuwa NGUMU.

5. Mwisho KABISA.Serikali ubadili lugha ya kufundishia kutoka Kiswahili kwenda kwenye Kiingereza ili likiwezekana basi itapunguza SANA faida za pre form one.
 
Kwa mawazo yangu pre form one ilifaa sana kwa Wanafunziwanaotoka shule za serikali maarufu kama Kayumba.!Faida zake ni nyingi sana kwao
1.Wapate utangulizi wa Lugha ya kufundishia sekondari ambayo ni kiingereza
FACT
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom