Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 47,058
- 122,454
Na chekechea nao wanapelekwa Tuition, Kuna Mtu Jana nimemsikia mahali anamtumia Mwalimu pesa ya tuition ya Mtoto wa chekechea
Na chekechea nao wanapelekwa Tuition, Kuna Mtu Jana nimemsikia mahali anamtumia Mwalimu pesa ya tuition ya Mtoto wa chekechea
Say you own a Pre form one center without saying it.........
Kuna wale ambao wametoka Kayumba.. kusoma English course ni sahihi.Humu naona manyumbu na mazuzu wamekutana kukubaliana ujinga. Mfano mimi niliondoka Std 7 nikiwa sijui English kabisa. Nikaenda mjini kupiga pre form one ya English ambayo ilinisaidia sana. Kule shule ya kata nikatisha naelewa vitu wakati wenzangu waliishia kukariri tu.
Hata kwangu nimekuwa nakusanya madogo bright wa ndugu zangu wa kijijini kuja kupiga pre form one huku nikiwatafutia uhamisho wataopangiwa shule za kata. Imekuwa msaada mkubwa sana. Kama Elimu ya bongo ni kufaulu pepa,mzazi ana kosa gani kutengeneza njia ya kufaulu.
Acheni kutiana upumbavu, mzazi ataangalia mahitaji ya mwanae sio ujinga wako. Usikute nyinyi ni failure na mitihani na maisha
Wewe sasa unafanya uhuni... Wewe kaa nao nyumbani tu. Huko mtaani mnaibiwa.Hiyo pre sasa, vijukuu vya kike vipo juu juu vimevaa vitop, si mama umeshajihimu huko kutafuta,
Sasa hapo ndo shetani anaanza kujiinua, shetani mwenyewe ni hao hao bodaboda oo saa mbili umfuate binti yangu umpeleke pre kwa mwalimu fulani.
Shetani mwingine wanakutana naye huko kwenye mabus,
Shetani mwingine hao hao asiowapenda yule mwana jf.
Hapo sasa ndo shida inapoanzia
Yap..!!Shule zingine wakichukua pre form one ndo intake ya form one hiyo hiyo hawapokei wanafunzi wapya...masomo yanaanza, wakirudi next year wanaendelea. Hii inawasaidia kumaliza syllabus mapema wanaanza za form two zile nyepesi
Eti halafu anasema eti mtoto.anatakiwa apumzishe akili,huyo.mtoto.hiyo akili yake hadi kafanya nini cha maana hadi kusema ipumuzishe kagundua chochote kikubwa kama huyo Elon Musk hadi apumzike?Mweka mada kanuna..😅
Kwani mkuu hata asipoenda ndo atakuwa huyo Elon musk..?
Kama hamna ni hamna tu!
Hongera ndivyo inatakiwa mtu.kupumzika anatakiwa awe tayari ka achieve kitu.kikubwa kwenye maishaMim nilkubal ktk baadhi
Nilimalza chuo skupumzika nikaanza CPA T nikijua kichwa changu kikipoa kukamata network ni ishuu....
Kweny pre fom nikasema kwa wazaz wanaojiskia kupeleka watto wawapeleke tuu.... Usimsklze mtu bhn
Lengo la pre form one kuwajengea msingi mzuri wa lugha haswa kwa wale waliotoka shule za serikali.Kwa mzazi ambaye kichwa kina chaji hawezi ruhusu huu uhuni, hii inawezekana kwa wazazi wapumbavu pekee, ambao kiwango cha kuwaza ni zero.
Mtoto kasoma miaka 7 sasa kamaliza shule, huyu hapumziki, anaunganishwa aanze kitu kinaitwa Pre-form one, atapigishwa Pre-form one hadi December then January aanze shule.
Na wazazi wengi tulivyo wapumbavu tunaona ndio njia sasa ya kumfanya mtoto aje kuwa kama Elon Musk wa Tesla au Mark Zuckerberg wa Facebook na Whatsapp. Yaani njia ya kumfanya mtoto aweze hata kuvumbua chombo cha kwanza cha Tanzania kwenda Mwezini ni kumpelekea Pre- form one.
Watoto hawana muda wa kupumzisha akili, na hii njia za Pre-form one ni njia za Wazazi kukwepa majukumu, Wazazi wa Kiafrika hawataki kukaa na watoto wao hata kuwafundisha elimu ya Duniani, kumfundisha maisha.
Wahindi sio wajinga kwenda na Watoto wao wa miaka 6 Dukani au Offisini kwao.
Ila sisi Wabongo tunaofanya Biashara eti hatutaki kwenda na Watoto wetu kwenye maeneo ya Biashara angalau waangalie kile tunachofanya, tunadanganywa na wahuni kwamba watoto wanapaswa kwenda Pre-form one kujifunza.
Ni vitu gani wanajifunza huko Pre-form one ambavyo hawatajifunza Sekondari?
Unataka msaada upi ili uone hizo tuition ni muhimu au sio muhimu?Nakazia.
Hata tuition nyingi ni upuuzi tu, haziwasaidii watoto chochote.
Siku za nyuma na mi nilikua na uelewa mbaya kama hawa kuwa ili mtoto afanye vizuri lazima asome pre form 1 au tuition lakini baada ya kujua kwa sasa huwezi kuniambia huo upuuzi mtoto anakuwa bize hana mda wa kupumzika, kurefresh maind wala kujifunza maisha ya mtaani au kazi za nyumbani jmn tukubali tukatae wazazi kumuweka mtoto mbali na wewe kwa kisingizio eti tuition au pre form 1 ni kumharibu mtoto kaa nae muelekeza maisha na kazi ya nyumbani ili kesho ukiwa haupo aweze kusavaive na life... Akili nayo inachoka kusoma kila wakati inataka kupmzishwa.Mtoa mada unayo hoja ila wenye tuition centres na wamiliki wa shule watakurukia kama mwewe.
Sihitaji msaada mkuu.Unataka msaada upi ili uone hizo tuition ni muhimu au sio muhimu?
Wewe ulipofeli Hisabati ukaona uende tuition ,je ilikusaidia au haikukusaidia?Sihitaji msaada mkuu.
Kama wewe unaziamini wapeleke watoto wako.
Binafsi nilisoma tuition mara moja tu baada ya kufeli hesabu nikatakiwa kurudia mtihani.
Mwanangu hajawahi kwenda tuition yoyote na amekuwa best student kwa levels zote za elimu alizopita na sasa yupo chuo kikuu anaendelea vizuri.
Sijawahi kuona umuhimu lakini kama zinawasaidia wengine basi waendelee. Kupanga ni kuchagua!
Sihitaji msaada mkuu.Unataka msaada upi ili uone hizo tuition ni muhimu au sio muhimu?
Ilinisaidia. Ndio maana hapo juu nimesema mpeleke mtoto tuition kama kuna uhitaji. Mfano kuna somo linamsumbua na sio mazoea tu unampeleka tuition kuanzia darasa la kwanza hata kama yupo vuzuri unampeleka likizo yote hapumziki, kwa upande wangu sio sahihi.Wewe ulipofeli Hisabati ukaona uende tuition ,je ilikusaidia au haikukusaidia?
Anhaaa umeona sasa umekiri kwa kinywa chako kwamba zinasaidia.Sihitaji msaada mkuu.
Kama wewe unaziamini wapeleke watoto wako.
Binafsi nilisoma tuition mara moja tu baada ya kufeli hesabu nikatakiwa kurudia mtihani.
Mwanangu hajawahi kwenda tuition yoyote na amekuwa best student kwa levels zote za elimu alizopita na sasa yupo chuo kikuu anaendelea vizuri.
Sijawahi kuona umuhimu lakini kama zinawasaidia wengine basi waendelee
Ilinisaidia. Ndio maana hapo juu nimesema mpeleke mtoto tuition kama kuna uhitaji. Mfano kuna somo linamsumbua na sio mazoea tu unampeleka tuition kuanzia darasa la kwanza hata kama yupo vuzuri unampeleka likizo yote hapumziki, kwa upande wangu sio sahihi.
Na baadhi ya shule zinazojitambua hasa za masister wanakwambia kabisa hatushauri umpeleke mtoto tuition wakati wa likizo.
Nilienda tuition kwasababu nilihitaji kufanya hivyo na nilikuwa nimeshamaliza shule nilihitaji kurudia somo la hisabati ambalo nilifeli.