Geza Ulole
Platinum Member
- Oct 31, 2009
- 75,720
- 107,169
When most of the Western world was still sunk in the darkness of the Middle Ages, Zanzibar was already a meeting place for traders from the great Oriental cultures – China, Persia and Arabia. It nestled in the middle of a mercantile civilisation, stretching from Somalia in the north down the coast of East Africa to Mozambique in the south. This kingdom and its inhabitants were known as the Swahili – the people of the coast.
They traded gold, ivory and cloth with visitors from across the Indian Ocean, built handsome stone houses and had well developed systems of government. Envoys, merchants and even pirates from as far away as Japan and Russia came to Zanzibar and its environs in sailing ships, blown across the seas by the northeast monsoon and returning, their holds laden with trade goods, on the southwest wind.
The first Europeans to ‘discover' Zanzibar were the Portuguese, who arrived in the late 15th century. In keeping with their conduct in the rest of their empire, they had little interest in the place beyond keeping it out of the hands of their enemies. They built a fort or two, introduced the sport of bullfighting to Pemba, and added a few choice words to the Swahili language. In fact, the Portuguese words still in use in Kiswahili give a fairly good impression of how the Portuguese spent their time here: Meza - table. Mvinyo - wine. Pesa - money.
Wengi wao hawajui hata asili yao, kuna jamaa mmoja anajiita yeye ni mzanzibari nilifanya naye interview katika shirika fulani la Umma hapa Dar na kwa bahati nzuri wote tulipata kazi katika kuja form mbalimbali kuna form mija ilikuwa na sehemu ya kujaza kabila, jamaa hakujaza kwa kuwa hajui kabila lake na hajawahi kubother kutafuta, mpaka leo ile nafasi iko wazi haijajazwa kabila lake, He was very honest kwamba hajui kabila lake.
Kitu kimoja ni mtu "kujinasibisha" yeye mwenyewe, kwa utashi, maslahi, mapenzi yake; kitu chengine ni asili ya mtu.Wazanzibari wengi wao ni waarabu, hata wale weusi kama mimi wanajitambulisha kama "waarabu"
Nina rafiki yangu Mzenji sijui kama anaifahamu hii forum, ngoja nimtumie hii linki pengine atakuwa na mawili matatu.
Ila nadhani wazanzibari wanaji "nasibisha" zaidi na waarabu kuliko wabantu.
I stand to be corrected.
Bila ya kutafuta makabatini, kwa kifupi Mzanzibari ni kila mzaliwa wa Zanzibar. Unaweza kuongeza vizazi viwili vitatu nyuma, kwa maana ya kuwa ikiwa babu na bibi yake mtu alzaliwa Zanzibar, inatosha kumfanya, kwa sifa ya uzawa wake, kuwa huyo ni Mzanzibari.
Kwa maneno mengine, kutokana na historia na jiografia ya Zanzibar, Wazanzibari ni mchanganyiko wa watu wenye asili tafauti (Watanganyika, Wakenya, Wakomoro, Wamakonde wa Msumbiji, Wahindi, Waajemi, Waarabu, Wachina...). Kuhusu hawa mwisho, kule Mkoani Pemba na Malindi Unguja, kuna Wachina wa zamani hata kabla ya kuja Waarabu; kwenye Msitu wa Ngezi/Kiuyu Pemba na Dole Unguja, kuna Wamakonde wa hata kabla ya Wareno. Makunduchi kuna Makumbaro (aina ya Wahindi) hata kabla ya Sultani; Kizimkazi kuna watu wenye asili ya Bagamoyo hata kabla kuja Mjerumani.
Hawa wanazuka leo na kusema asili ya Zanzibar ni Watanganyika au Waarabu, Waislamu au Wakristo, hiki ni kizazi cha watu muflis wa mawazo, kwani Zanzibar ina michanganyiko yote hiyo. Kwa hivyo, ama Zanzibar ni ya wote au si ya yeyote.
Wana JF,
Imefika wakati sasa kuanza kuhoji nani haswa ni Mzanzibari Asilia kihistoria maana tunakoenda sasa si huko na katika kujua haya inatupasa kupitia historia yetu hata kabla Waajemi na Waomani hawajatua Zanzibar yaani wakati huo visiwa hivi vikiwa na majina ya Kiasili ya kiafrika yaani Unguja n.k. na pia kipindi cha Wareno pia kipindi cha Wajerumani hadi Waingereza na pia siasa na utaifa wa Kizanzibari baada ya uhuru na mapinduzi ya Zanzibar
Tuanze na historia ya Unguja kabla ya mwarabu kuja; inasemekana kulikuwa na waafrika (ngozi nyeusi) wakiishi huko wengi wao walikuwa ni wale wavuvi wanaotoka pwani ya Tanganyika wakiienda huko kutokana na shughuli za uvuvi na hata baadhi yao kuwa na makazi yao huko na pwani pia; watu hawa walikuwa na dini za kiasilia wakifanya matambiko na yale yote yanayofanywa na wenzao wa Pwani yaani makabila ya Pwani kiutamaduni.
Haya yote yalianza kubadilika pale Mwarabu toka Oman alipotia nanga katika visiwa vile kwani utawala wa Asili haukuwa na nguvu ya kumzuia Mwarabu kufanya anachotaka maana alikuwa na silaha za kivita yaani bunduki iliyokuwa bora zaidi ya mkuki, mshale au sime. Kwa mantiki hiyo basi uhuru wa Mwafrika halisi ukapotea pale tu Mwarabu alipotia mguu katika visiwa vile. Mbali na hayo biashara haramu kama utumwa ilianzishwa na Mwarabu na pia biashara ya pembe za ndovu zilizomlazimisha kwenda hadi Ujiji kusaka vipusa hivyo
Historia hii itaendelea.....
Ni Mwanadamu aliye Mwenye rangi ya brown aliyetoka bara, alichukuliwa bara kama Mfanyakazi au Mtumishi au Mtumwa lakini akapendwa na Bwana yake (Kiongozi wa anayewatunza hao watumwa) na kuwabakisha na kuwapa haki kidogo baada ya Mfalme kupewa nchi na Waingereza alihakikisha wanafuata DINI yake ya KIISLAMU na pia kwasababu waarabu walikuwa wachache walitumia system inayoitwa ASSIMILADO - ni ya kofauti uwafanya waafrika wa huko kufikiri kama wao ni waafabu kiutamaduni , kimazingira, kula na hadi jinsi ya kuongea na hadi damu yao na ya kiarabu ni sawa tofauti ni rangi za miili yao kuwa tofauti lakini kila kitu ni sawa huko Zanzibar.
[video] http://www.mzalendo.net/habari/video...tu-wa-zanzibar[/video]