Mzalendo asiyependa kukaguliwa....

Mzalendo asiyependa kukaguliwa....

Kitendo cha Spika kumdhalilisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali CAG, ni dalili za wazi kabisa kuwa serikali kupitia kwa Spika ina jambo inalificha haitaki lijulikane.

Mbona watangulizi wake walikuwa wanakaguliwa wakati mwingine walikuwa wanakutwa na madudu makubwa lkn serikali zilikuwa zinakuja na majibu, ingawa mengine yalikuwa si ya kuridhisha lkn walijibu.

Kuna wanaojiuliza, inawezekana ni 1.5T alizohoji CAG, au kuna ufisadi mkubwa unafanyika kupitia miradi mikubwa ya Stieglars Gorge, ujenzi wa SGR, ununuzi wa ndege nk.

Ina maana serikali hii haina watu wenye akili ya kupangua hoja 'professionally' hadi wafunike wizi kishamba namna hii, mbona kwenye EPA walikuja na majibu, Tegeta Escrow walijibu kisomi ingawa hatukuridhika lkn walijibu.

Kwanini isiwe sasa kuna nini wanaficha? Ni uzalendo gani huo sasa wa kutataa kukaguliwa. Kama hamtaki taasisi za serikali zikaguliwe hiyo vita ya UFISADI mtaishinda vipi au ni kiini macho tu?
Hakuna vita ya ufisadi hapa ndugu yangu, hizi za mkulu ni drama tu. Werevu tulisha shituka sikunyingi tu.
Walio chelewa kumbaini, hii ni nafasi yao sasa amejiweka peupe!!!!
 
Kaone uzalendo pale chattel mkuu…….hata utafiti wa kufungua tawi la crdb alifanya yeye wkt wenye crdb yao walikataa
Hili jamaa no lifisadi likubwa kuliko maelezo. Mbaya zaidi hatumii akili ni vitisho tu.
Ninaona hatokubali kutoka madarakani huyu, kwani haya mambo yatawekwa wazi na anaye mfuata kama atakuwa mzalendo.
 
Unaweza usiipige 1.5t uweke mfukoni yote, lakini unaweza kufanya miradi ya upendeleo na katika hiyo miradi ukala 10% yako. Mfano halisi wa hizo hela ni mradi wa Chattle airport. Tunasema hivi, tunataka kujua 1.5t zilitumika kwenye nini na ruhusa ya nani fullstop. Kitisho cha pingu hakiwatoi. Huyo spika aliyejigeuza PS wa jiwe hana bahati safari hii.
Hata kuweka mfukoni inawezekana ameweka, ukiangalia anavyo gawa hela hovyo!!!!
 
WaTz tuna ugonjwa mmoja wa kusahau pindi tulabinshwapo sukari kidogo! CCM na UFISADI - iwe ni ya Nkapa, iwe ya Kikwete, au iwe ya Jiwe - ni kama Samaki na Maji. Samaki hawezi kuishi zaidi ya masaa matatu nje ya maji. Vivyo hivyo, CCm haiwezi ku-survive bila ufisadi (ni utamaduni umejengwa. unaweza kuja kwa majina na kwa namna mbalimbali, lakini ni wizi wa kimfumo). Utamaduni huu hauwezi kutoweka bila CCM kufa kwanza (yaani ikaondolewa madarakani hata kwa muhula mmoja) na pengine ikazaliwa upya huko mbeleni. Ushahidi ni Jiwe, mbali ya kutotaka kukaguliwa (tena kwa mujibu wa Katiba aliyoapa kuilinda) hata kabla ya kuwa rais ameacha stori nyingi huko mawizarani ambazo huibua maswali mengi badala ya majibu - lakini ndiye anyeonekana na kushangiliwa kuwa MZALENDO nambari wani! Kama uzalendo ndio huu, nime-declare sitataka kuwa mzalendo hata siku moja.Acha niwe wakala wa mabeberu.
Sure!
 
Hakuna vita ya ufisadi hapa ndugu yangu, hizi za mkulu ni drama tu. Werevu tulisha shituka sikunyingi tu.
Walio chelewa kumbaini, hii ni nafasi yao sasa amejiweka peupe!!!!
Mupe muruke hyo.....
Nikiku mind na kama unaskendo nakupa kesi#hyo Inaitwa

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Washamba wanawaangalia nyie waerevu na kujiuliza pamoja na uerevu wenu wote mbona washamba wanawatoa jasho? Acha kuota awamu ya 4 hapa na kukumbusha haya majeraha yake kwa Taifa hili. Vidonda bado havija pona na mkiendelea kuvikunakuna na hizo kucha zenu chafu vitatoa damu na kupata infections. Damu itakayo toka katika vidonda hivi vya Taifa/Nchi hii haita mwaacha salama Kibaka Mwenye Heshima/KIMWEHE yeyote.

CAG katangaza mwenyewe hadharani tena huko UNO kuwa hana imani na Bunge la JMT. Yeye kwanza si kati ya hao washamba, si ndio? Ajiuzulu basi tuuone uendelevu wa huo ujasiri wake. Haiwezekani akafanya kazi na asiokua na imani nao, haiwezekani! Uzuri kaliongelea USA na anajua wa aina yake huko huchukua hatua gani baada ya kutoa dukuduku zao. Asilete ujanja ujanja ajiuzulu. Kumbe mvi sio siku zote maana yake ni uzee wenye hekima.
Huwezekani tena we ni mboji ya CCM.
Lazima unaumri zaidi ya miaka 70, so kwa comment hizi!!!
 
Sijawahi kuona taasisi yoyote duniani ikagombana na auditor wake, kama ikitokea hivyo huyo CEO wake na Bodi nzima watafagiliwa next day, kugombana na Auditor huwa si kuzuri hata kidogo -
Hata benki ya Dunia huwa wanakaguliwa na wakionyesha wazembe pia wanaweza kuambiwa ni dhaifu.

Hakuna taasisi yoyote duniani isiyo na udhaifu, hata Ikulu ya marekani ina madhaifu yake sasa sembuse Bunge la TZ lenyewe ni Tukufu na litabakia tukufu milele...Mawazo ya kijima haya!!
 
Kitendo cha Spika kumdhalilisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali CAG, ni dalili za wazi kabisa kuwa serikali kupitia kwa Spika ina jambo inalificha haitaki lijulikane.

Mbona watangulizi wake walikuwa wanakaguliwa wakati mwingine walikuwa wanakutwa na madudu makubwa lkn serikali zilikuwa zinakuja na majibu, ingawa mengine yalikuwa si ya kuridhisha lkn walijibu.

Kuna wanaojiuliza, inawezekana ni 1.5T alizohoji CAG, au kuna ufisadi mkubwa unafanyika kupitia miradi mikubwa ya Stieglars Gorge, ujenzi wa SGR, ununuzi wa ndege nk.

Ina maana serikali hii haina watu wenye akili ya kupangua hoja 'professionally' hadi wafunike wizi kishamba namna hii, mbona kwenye EPA walikuja na majibu, Tegeta Escrow walijibu kisomi ingawa hatukuridhika lkn walijibu.

Kwanini isiwe sasa kuna nini wanaficha? Ni uzalendo gani huo sasa wa kutataa kukaguliwa. Kama hamtaki taasisi za serikali zikaguliwe hiyo vita ya UFISADI mtaishinda vipi au ni kiini macho tu?
hahaa inafurahisha mwizi kumkataa hakimu
 
Wajiitao wazalendo behind our back they deceive us....
 
Nd
Punguza mahaba kama aliwah kuwepo mzalendo nchi hii bac Sokoine nambar moja weng waliobaki n wazugaj tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndivyo mlivyo wanadamu wa kawaida, kumsifia mtu akishakufa...wacha wenye uwezo zaidi ya wastani tumsifie shujaa Magu akiwa hai...nyie wengine kama mtakuwa hai mtakujakutuunga mkono kutufanya hivyo wakati mwingine wakati Magu wetu shamaliza kusudi lake!
 
Back
Top Bottom