Hallooo ,
subkuch tiike wana jf
Nilikuwa na mahusiano na nurse mmoja katika mji ambako nilizaliwa, baba na mama walikua wanaishi huko.Kipindi hicho nilikuwa field huko home. Baada ya kumaliza field nurse wangu alinipatia vile vipimo vya HIV (kama vikaratasi hivi unaweka tone la damu yako then unasubiri dakika tano kuna mistari itaonekana). Kwa ajili ya kumpima mtu kabla sijamtumia.
Baada ya kurudi DSM ili niendelee na masomo yangu, pale ninapoishi ilikua nyumba ya kupanga nkakuta kuna mdada mpya kahamia kama jirani yangu. Kabla sijafika alishapewa taarifa zangu hivyo hakushangaa aliponiona. Alikua mdada mrembo, mweusi, mrefu, mwembamba ila ana umbo la kuvutia, kiumri alikua kanizidi hivyo heshima ilikuwa juu.
Basi tukaanza urafiki akiinita uncle, akawa anapika na kunikaribisha maramoja moja. Baada ya kama mwezi siku moja alikuja chumbani kwangu kucheki movie, basi katika kupiga story mara ikaingia ya kupima HIV, yeye akasema hajawahi kupima mi nkasema nshapima mara nyingi, na hapa ndani nina vipimo kama ana moyo nimpime. Akasema nimpime, Basi nikatoa vipimo vyangu nikamchukua damu nakumpima, wakati anasubiri vipimo jamaa yake akaja hivyo akaenda kuongea nae, akaaka muda mrefu mpaka jioni jamaa akawa kaondoka, huku upande wangu vipimo vikaonyesha ana maambukizi! nilijuta kumpima kwani nitamwambia nini mdada wa watu? sijui chochote kuhusu ushauri nasaha.....mh...ilikua wakati mgumu sana kwangu, nilimwonea huruma sana.
Basi baadae akaja na kuniuza majibu yake, nkamwambia yuko poa, ila akalazimisha kuona hiyo karatasi nkamwambia nimeitupa...Hakuamini akaanza kutafuta mara akaiona na kugundua ameathirika! Dah, alilia sana kwa uchungu na kutaja jina la boyfriend wake, mama yake pamoja na mwanae( kumbe alikua na mtoto mmoja). Dah, nlishindwa nifanyeje, nkajikuta nambembeleza na kushauri aende hospital kwa ajili ya kuhakiki kwani hivyo vipimo havina uhakika sana. basi baada ya mtanange mrefu alitulia.
Kesho yako alidamka kwenda kupima na kweli akakuta positive, ilikua siku ya huzuni sana kwake alitamani kujiua na kusema jamaa ndio kamletea.
Baada ya kama mwezi alikubaliana na hali na mimi nilimfichia siri na akaanza kupata dozi ya ARV. Maskini nilijuta kumpima, masihara yalinifanya nijione mkosaji... Ila nilimwonya asimwambie jamaa yake kwani itakuwa mwisho wa kupewa misaada na atatelekezwa, hii ni kutokana na kumbe jamaa alikua mume wa mtu, yeye alikua kimada tu....
Ni miaka kumi sasa imepita sijui kama bado yupo hai au alifariki dunia.....