Myahudi ELI COHEN(MOSSAD)/KAMEL AMIN SABET(syrian undercover) na gharama ya kuokoa TAIFA

Siamini kama hawa watu wanaojulikana kuwa ni Wayahudi ni Wayahudi wa damu.....

Kama siwaamini hata story zao siziamini pia......
vizuri, unashauri tuwaamini kama wakina nani, au ni lini wayahudi wa damu walipotea ulimwenguni kama wagiriki na waarabu wa damu bado wapo hadi kesho. Tia neno kidogo hapo mkuu ila kila mtu yuko sahihi until proven wrong
 
vizuri, unashauri tuwaamini kama wakina nani,
Sijui mkuu,anza kufanya uchunguzi ili ujue lakini kwangu mimi binafsi Wayahudi sio hawa tunaoambiwa leo ni Wayahudi.....
au ni lini wayahudi wa damu walipotea ulimwenguni
Mkuu sijasema popote walipotea,labda wewe unajua hili mkuu......
kama wagiriki na waarabu wa damu bado wapo hadi kesho.
Hata Wayahudi wapo mkuu.....
Tia neno kidogo hapo mkuu ila kila mtu yuko sahihi until proven wrong
Ni kweli mkuu.....
 
Daima huwa nanung'unikaga kusikia nchi za arabuni kushambuliwa huwa nalaani sana.
Kwani nchi za arabuni ni nchi zinazoleta Ustaarabu duniani.
I love Syria, Sweden,Iraq, Moroco,Saudi Arabia and so on.
 
1478357011488.jpg
 
mfanyabiashara mkubwa ni sawa na waziri, leo hii bakhresa akienda bukoba kuzindua depo yake ya juisi utaona mkuu wa mkoa yupo amehudhuria
Au boss wa chelsea alipokuja bongoland kushangaa kidogo kilimanjaro na wanyama mambo yake binafsi tu lkn airport Kuna mwanasiasa akaforce kukutana nae. Au businessman mmoja mkubwa alivyoshutumiwa kuhusika na mauaji South Africa. Ndio maana huyu jamaa COHEN alijulikana baada ya mkuu wa intellijensia Mpya aliyechaguliwa kutokuwa na imani na mtu yoyote yule.
 
Cohen was arrested because they caught him sending information to Israel after detecting radio signals from his appartment....Syrians assisted by Russians, decided to switch all radio signals....and use detectors to see if there are radio signals sent without their knowledge or approval.
His friends who were Baath party member didn't tell him about that decision in advance.....
But on the other hand he was sending information back to Israel twice a day....very dangerous for sensitive job he was doing

Ahsante Mkuu. Now i get it why he wrote on his prison cell wall “I don’t regret what I have done, only what I could have done and didn’t have the chance to do. Sometimes close friends fail those who can act,” .

http://free.messianicbible.com/feat...aels-impossible-spy-defeated-the-syrian-army/
Ynetnews News - 'Eli knew someone betrayed him'
 
Mada tamu sana hii.

Inaonekana mbinu ya kutumia wafanya biashara wakubwa kuwa majasusi inapendwa sana, sijui kwa nini.

Niliwahi kusoma humu jamvini pia kuwa yule mbunge wetu mfanya biashara maarufu aliyeachana na siasa uchwara ni ajenti mkubwa sana wa C.I.A

Sijajua ni kwa nini mbinu hii majasusi wanapenda sana kuitumia kupandikiza deep cover agents
Rostam au?
 
Daima huwa nanung'unikaga kusikia nchi za arabuni kushambuliwa huwa nalaani sana.
Kwani nchi za arabuni ni nchi zinazoleta Ustaarabu duniani.
I love Syria, Sweden,Iraq, Moroco,Saudi Arabia and so on.
Haya mambo ni magumu mkuu. Sasa ukiangalia saudia anapigana na waarabu flani wa Yemen. Hapo Iraq walionewa na Bush na wenzake lkn Sasa wanapigana wenyewe kwa wenyewe na wengine wanatumiwa, ila kiukweli tunapaswa kunung'unikia uonevu wowote Ule sio kwa watu wa jamii fulani tu.
 
Mada tamu sana hii.

Inaonekana mbinu ya kutumia wafanya biashara wakubwa kuwa majasusi inapendwa sana, sijui kwa nini.

Niliwahi kusoma humu jamvini pia kuwa yule mbunge wetu mfanya biashara maarufu aliyeachana na siasa uchwara ni ajenti mkubwa sana wa C.I.A

Sijajua ni kwa nini mbinu hii majasusi wanapenda sana kuitumia kupandikiza deep cover agents
MO?
 
Nitie neno kidogo wakuu,

Mwaka 2007 nikiwa huko kujiendeleza kielimu nilibahatika kujifunza juu ya huyu mtu na hata kaka yake aliyeitwa Moris aliwahi kufika tulipokuwa tukiendelezwa.

Cohen alikuwa mtu smart sana kichwani lakini kuna makosa fulani aliyafanya na hili pungufu lilikuwa kwenye ripoti ya pyscho-analysis aliyofanyiwa, pungufu hili lilikuwa ni kutojali mazingira hatarishi na kujiamini kupita kiasi.

Alipofika Syria alifika huko kama mfanyabiashara, lakini maisha aliyoishi yalimtia doa. Kwanza mahali alipopata nyumba ya kuishi ulikuwa ni mtaa wa watu wazito lakini ukifika kwake na kuingia ndani palikuwa hapafanani na nyumbani kwa mfanyabiashara, hili liliwapa hofu watu wake karibu na kujiuliza ni mfanyabishara gani huyu ambaye kwake pako pa kawaida? ki meza na kiti kimoja ndani, hakuna mpishi anajipikia, anafanya usafi nk.

Jambo lingine lilikuwa ni kwamba alijitambilisha kama mfanyabiashara mkubwa lakini awapo huko hakuna biashara kubwa ya maana aliyokuwa anafanya, sanasana ilikuwa ni kurusha party na kujirusha na hao Maafisa wa Jeshi ambao alifanikiwa kujipenyeza na kuwa karibu nao.

Kaka yake Moris nae alikuwa ni mtu wa Mossad aliyekuwa akipokea taarifa kutoka kwa agents mbalimbali duniani, hakujua kama mdogo wake nae alikuwa ni mtu wa system na alikuwa akipokea taarifa nyingi toka kwa mdogo wake pasipo kujua mtumaji ni ndugu yake cohen.

Siku moja akapokea ujumbe unaosema, "mmefanikiwa kupeleka kile kichwa cha cherehani nyumbani?"" Moris alipopokea ujumbe huo na kuanza kuudecode alishindwa, akaupeleka kwa mkubwa wake wa kazi, bosi wake alipouona akajua umetoka kwa Eli ambae ni mdogo wake na Moris na huku akisita kumwambia umetoka kwa mdogo wako. Ilibidi amwambie kuwa kwa level ya nafasi yako hapa huna mamlaka ya kujua maana ya ujumbe huu na ikaishia hapo.

Jioni yake Moris alienda nyumbani kwa mdogo wake kumsalimia shemeji yake mke wa Eli Cohen, aliyeitwa Nadia binti wa Kiiraki. Alipofika akakuta kichwa kipya cha cherehani akamuuliza shemeji. Shemeji akasema kimetumwa baba mdogo wako, hapo hapo Moris akaanza kuunganisha matukio, akajiuliza hivi inawezekana mdogo wangu ndie anatuma taarifa kutokea Damascus ambae ofisini alifahamika kama ""our man in Damascus", alijiuliza kisha akakaa kimya.

Mwezi Disemba, Eli alirudi nyumbani bila taarifa mke wake akashangaa sana, lakini kwa mbinu za kijasusi jamaa alifanikiwa kumweleza na akaamini hakuna shida. Ilikuwa akae wiki tatu lakini ndani ya siku tatu, usiku wa saa kumi, simu yake ikaita ya nyumbani, alipopokea akaambiwa ratiba imebadilika unatakiwa kurudi Damascus haraka, tumeshambuliwa na adui na watu wetu baadhi wameuawa, gari itakupitia ndani ya lisaa limoja tunahitaji taarifa za kina kutoka kwa adui. Eli akajibu kwa mshangao, yaani usiku huu niondoke?! akajibiwa ndio.

Mke wake Nadia alikuwa macho, Eli akaamka na kumwambia naondoka, unaenda wapi na ulisema utakaa wiki tatu mbona ni siku tatu hata hatujaenjoy unaonaondoka? Eli akajibu hii itakuwa ni safari yangu ya mwisho nikirudi sitaenda tena tutakaa wote na kulea watoto.

Jamaa akajikusanya na muda ulipofika gari ilimchukua na safari ikaanza.

Sasa wakati yuko hapo kwa mke wake kaka yake Moris alikwenda kumtembelea na alipofika alimkuta mdogo wake. Mdogo wake alijua kaka yake yaani Moris anafanya kazi shirika la posta, sasa alipofika akakuta Eli amemletea binti yake kanda mbili zilizokuwa zimeandikwa kiarabu, kichwani kwake alishatia shaka juu ya mdogo wake, akamuuliza hizi kanda mbili za mtoto umenunulia wapi? Eli akajibu akasema Ufaransa, Moris akamuuliza siku hizi Ufaransa wanatengeneza bidhaa na kuziandika kiarabu? Eli akapotezea, Moris akazidI kuunganisha matukio.

Then moris akamuomba namba ya simu anayotumia akiwa huko ugenini, Eli akataja namba ya uongo kwa kuacha namba za mwanzo mbili kisha zingine akataja, sasa kumbe Moris anazijua namba kibao za maagenti wao, akamwambia Eli umeruka namba mbili za mwanzo ambazo ni; Akamtajia na Eli akakasirika na kumuaga kaka yake kuwa anatoka kidogo kama dakika kumi.

Eli akaenda kupiga simu kwa bosi wake na kumuuliza ni nani amemwambia kaka yake juu ya kazi yake na mahali alipo, bosi akauliza kwani kuna nini, akamwambia kaka ameniomba namba nami nikaacha kutaja namba mbili lakini akaniambia nimempa namba ya uongo na kunitajia namba, bosi akamwambia tulia hakuna shida kaka yako ni mtu wetu.

Sasa aliporudi Damascus ni kweli Eli alifanya kazi ya ziada kupata taarifa, siku moja akawa amekusanya viongozi wakubwa wa jeshi akafanya party, sasa pale kwenye party Jenerali mmoja akamwambia mwingine juu ya habari za Eli, kuwa ni kijana wao na raia mzuri wa taifa lile aliyefanikiwa katika biashara, akamtaja na jina.

Baadae Eli akafika walipo wale Majenerali na mmoja akamshukuru sana Eli kwa party hiyo na akasemana leo nimechoka sana maana nilikuwa huko kwa milima ya Golan, Eli akataka kujua zaidi, akasema kwa kuuliza Golan ulikwenda kule kufanya nini? Jenerali akamwaga vitu, akaeleza kule golan kuna nini na akamwambia nitakupeleka siku moja.

Siku ikafika wakaenda kule, jamaa akajioneka mahandaki ya Jeshi la Syria yalivyo na akapata taarifa kibao.

Aliporudi usiku fasta akatuma taarifa nchini mwake akasema leo nimefika Golan, kuna mahandaki ya adui yaliyojengwa kwa ustadi mkubwa, mkitaka kushambulia alama pekee inayoonyesha yalipo ni miti iliyopandwa juu kwa mstari, pigeni hapo na mtayasambaratisha.

Sasa Eli akawa anatuma taarifa mara kwa mara kila siku na alikuwa akituma taarifa usiku wa saa mbili kika siku, sasa jeshi la Syria lilikuwa limepata vifaa vipya vya kutambua mawimbi ya taarifa, kwa hiyo kila siku usiku wakawa wanafuatilia kila mawimbi ya sauti yanapopita kwa kuzima umeme baadhi ya maeneo, mfano; leo wanazima mtaa huu na kesho ule, wakafanikiwa kujua na kupata mawimbi yale yanapotokea, wakasuka mpango wa kuvamia nyumba ile.

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo juu ya tatizo la Eli la kujiamini kupita kiasi na kutokuchukua tahadhari katika mazingira hatarishi, walivamia nyumbani kwake alfajiri na kumkuta jamaa anaendelea kutuma taarifa, alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.

Israel ikapata taarifa na wakuu wa Mossad wakatoa ujumbe mfupi ukisema, our man in Damascus has burnt! Serikal ya Israel ikafanya jitihada nyingi sana katika kuokoa maisha yake na kuachiwa mpaka wakamtumia Papa Kiongozi wa Kanisa Katoliki aingilie kati na kuiomba Syria kumwachia huyu, jitihada hazikufua dafu.

Wakuu wakafikisha taarifa kwa mke wake Eli, Nadia akalia sana na kusema ni heri mume wangu angekuwa shoe shine na akawa hapa namuona, naomba mumlete mume wangu, wakuu wa Mossad wakamjibu, tutahakikisha anarudi akiwa salama na katika kipande kimoja na si vipande vipande.

Jamaa akashitakiwa na kuhukumiwa kifo kwa kunyongwa na alinyongwa na kaburi lake mpaka leo halifahamiki mahali lilipo huko Syria, taarifa zikapelekwa nyumbani kwa mke wake Eli pamoja na ujumbe wa barua aliyoiandika Eli kwa mke wake, mke alipomuona yule jamaa akauliza mme wangu ameuawa au mzima, jamaa akamjibu pokea Eli alikuwa mtu muhimu sana na mwenye maarifa mengi.

Huo ukawa mwisho wake.

Taarifa alizotoa dakika za mwisho ndizo ziliwapa ushindi Israel katika vita yao ya siku sita.
 
Nitie neno..
Mwaka 2007 nikiwa huko jiendeleza kielimu nilibahatika kujifunza juu ya huyu mtu na hata kaka yake aliyeitwa moris aliwah kufika tulipokuwa tukiendelezwa..
Cohen alikuwa mtu smart sana kichwan lakini kuna makosa flan aliyafanya na hili pungufu lilikuwa kwenye riport ya pyscho-analysis aliyofanyiwa...pungufu hili lilikuwa ni kutojali mazingira hatarishi na kujiamini kupita kias...
Alipofika syria alifika huko kama mfanyabiashara..lakini maisha aliyoishi yalimtia doa..kwanza mahali alipopata nyumba ya kuishi ulikuwa ni mtaa wa watu wazito lakini ukifika kwake na kuingia ndani palikuwa hapafanani na nyumban kwa mfanyabiashara...hili liliwapa hofu watu wake karibu na kujiuliza ni mfanyabishara gani huyu ambaye kwake pako pa kawaida..ki meza na kiti kimoja ndani..hakuna mpishi anajipikia,anafanya usafi nk..
Jambo lingine lilikuwa ni kwamba alijitambilisha kama mfanyabiashara mkubwa lakini awapo huko hakuna biashara kubwa ya maana aliyokuwa anafanya..sana sana ilikuwa ni kurusha party na kujirusha na hao maafisa wa jeshi ambao alifanikiwa kujipenyeza na kuwa karibu nao.....
Kaka yake moris nae alikuwa ni mtu wa mosad aliyekuwa akipokea taarifa kutoka kwa agents mbali mbali duniani...hakujua kama mdogp wake nae alikuwa ni mtu wa system ..na alikuwa akipokea taarifa nyingi toka kwa mdogo wake pasipo kujua mtumaji ni ndugu yake cohen...
Siku moja akapokea ujumbe unaosema .."mmefanikiwa kupeleka kile kichwa cha cherehan nyumbani?""moris alipopokea ujumbe huo na kuanza kuudecode alishindwa..akaupeleka kwa mkubwa wake wa kazi..bosi wake alipouona akajua umetoka kwa eli ambae ni mdogo wake na moris na huku akisita kumwambia umetoka kwa mdogo wako..ilibidi amwambie kuwa kwa level ya nafasi yako hapa huna mamalaka ya kujua maana ya ujumbe huu...ikaishia hapo..
Jioni yake moris alienda nyumban kwa mdogo kwenda kumsalimia shemeji yake..mke wa eli cohen aliyeitwa nadia binti wa kiiraki..alipofika akakuta kichwa kipya cha chereheni akamuuliza shemeji. Shemeji akasema kimetumwa ba mdogo wako...hapo hapo moris akaanza kuunganisha doti..akajiuliza hivi ibawezekana mdogo wangu ndie anatuma taarifa kutokea damascus ambae oficin alifahamika kama ""our man in damascus"..alijiuliza kisha akakaa kimya..
Mwezi december eli alirudi nyumban bila taarifa mke wake akashangaa sana..lakininowa mbinu za kijasusi jamaa alifanikiwa kumweleza na akaamini hakuna shida..ilikuwa akae wiki tatu lakin ndani ya siku tatu usiku wa saa kumi simu yake ikaita ya nyumbani ..alipopokea akaambiwa hivi..ratiba imebadilika unatakiwa kurudi damascus haraka..tumeshambuliwa na adui na watu wetu baadhi wameuawa...gari itakupitia ndani ya lisaa limoja..tunahitaji taarifa za kina kutoka kwa adui..eli akajibu kwa mshangao ..yaani usiku huu niondoke?!..akajibiwa ndio...mke wake nadia alikuwa macho ..eli akaamka na kumwambia naondoka..unaenda wapi na ulisema utakaa wiki tatu mbona ni siku tatu hata hatujaenjoy unaonaondoka?!!eli akajibu hii itakuwa ni safari yangu ya mwisho nikirudi sitaenda tena tutakaa wote na kulea watoto...
Jamaa akajikusanya na mda ulupofika gari ilimchukua na safari ikaanza...
Sasa wakati yuko hapo kwa mke wake jaka yake moris alikwenda m kumtembelea na alipofika alimkuta mdogo wake..mdogo wake alijua kaka yake yaan moris anafanya kazi shirika la posta..sasa alipofika akakuta eli amemletea binti yake kanda mbili xilizoluwa zimeandikwa kiarabu..kichwan kwake alishatia shaka juu ya mdogo wake ..akamuuliza hizi kanda mbili za mtoto umenunulia wapi?!..eli akajibu akasema ufaransa..moris akamuuliza siku hizi ufaransa wanatengeneza bidhaa na kuziandika kiarabu..eli akapotezea...moris akazid kuunganisha dot..
Then moris akamuomba namba ya simu anayotumia akiwa huko ugenini..eli akataja namba ya uongo kwa kuacha namba za mwanzo mbili kisha zingine akataja ..sasa kumbe moris anazijua namba kibao za maagenti wao ..akmwambia eli umeruka namba mbili za mwanzo ambazo ni ..akamtajia..eli akakasirika na kumuaga kaka yake kuwa anatoka kidogo kama dk kumi..eli akaenda kupiga simu kwa bosi wake na kumuuliza ni nani amemwambia kaka yake juubya kazi yake na mahali alipo..bosi akauliza kwana kuna nini..akamwambia kaka ameniomba namba nami kaacha kutaja namba mbili lakini akaniambia nimempa namba ya uongo na kunitajia namba...bosi akamwambia tulia hakuna shida kka yako ni mtu wetu..
Sasa aliporudi damascus ni kweli eli alifanya kazi ya ziada kupata taarifa..siku moja akawa amekusanya viogozi wakubwa wa jeshi akafanya party..sasa pale kwenye party generary mmoja akamwambia mwingine juu ya habari za eli..kuwa ni kijana wao na raia mzuri wa taifa lile aliyefanikiwa katika biashara..akamtaja na jina..baadae eli akafika walipo wale majenerali na mmoja akamshukuru sana eli kwa party hiyo na aasemana leo nimechoka sana maana nilikuwa huko kwwnyw milima ya goran..eli akataka kujua zaid..akasema kea kuuliza goran?!..ulikwenda kule kufanya nini?!..jenerali akamwaga vitu..akaelza kule goran kuna nini..na akwambia nitakupeleka siku moja..
Siku ikafika wakaenda kule..jamaa akajioneka mahandaki ya jeshi la syria yalivyo na akapata taarifa kibao..
Aliporudi usiku fasta akatuma taarifa nchini mwakr akasema..leo nimefika goran..kuna mahandaki ya adui yaliyojengwa kwa ustad mkubwa..mkitaka kushambulia alama pekee inayoonyesha yalipo ni miti iliyopandwa juu kwa mstari..pigen hapo na mtayasambaratisha..
Sasa eli akawa anatuma taarifa mara kwa mara kila siku na alikuwa akituma taarifa usiku wa saa mbili..kika siku...sasa jeshi la syria lilikuwa limepata vifaa vipya vya kutambua mawimbi ya taarifa...kwa hiyo kila siku usiku wakawa anawafatilia kila mawimbi ya sauti yanayipita kwa kuzima umeme maeneo flan flan..mfano lei wana zima mtaa huu na kesho ule..wakafanikiwa kujua na kupata mawimbi yale yanapotokea..wakasuka mpango wa kuvamia nyumba ile..
Kama nilivtoeleza hapo mwanzo juu ya tatizo la eli la kujiamini kupita kias na kutokuchukua tahadhari katika mazingira hatarishi...walivamia nyumbani kwake alfajiri na kumkuta jamaa anaendelea kutuma taarifa..alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi..
Israel ikapata taarifa..na wakuu wa mosad wakatoa ujumbe mfupi ukisema..our man in damascus has burnt!!..serikal ya israel ikafanya jitihada nyingi sana katika kuokoa maisha yake na kuachiwa mpaka wakamtumia papa kiongozi wa kanisa katoriki aingilie kati na kuiomba syria kumwachia huyu..jitihada hazikufua dafu..
Wakuu wakafikisha taarifa kwa mke wake eli..nadia akalia akalia sana na kusema ni heri mume wangu angekuwa shoe shine na akawa hapa namuona ..naomba mumlete mume wangu..wakuu wa mosad wakamjibu ..tunahakikisha anarudi akiwa salama na katika kipande kimoja na si vipande vipande..
Jamaa akashitakiwa na kuhukumiwa kifo kwa kunyongwa...na alinyongwa na kaburi lake mpaka leo halifahimi mahali lilipo huko syria...taarifa zikapelekwa nyumban kwa mke wake eli pamoja na ujumbe wa barua alioiandika eli kwa mke wake...mke alipomuona yule jamaa akauliza mme wangu ameuawa au mzima...jamaa akamjibu ..poke eli alikuwa mtu muhimu sana na mwenye maarifa mengi...
Huo ukawa mwisho wake..
Taarifa alizotoa dakika za mwisho ndizo ziliwapa ushindi israel katika vita yao ya siku sita...

Huyu bwana Cohen alianza kutuma taarifa "tamu" mno kwa wakubwa zake na hii pia ilichangia kushindwa kudhibiti kasi ya taarifa alizokuwa anatuma. Kiukweli MOSSAD walikuwa na nafasi ya kuepusha kukamatwa kwa Cohen kama wangesimamia misingi ya ujasusi ambayo sasa Cohen alikuwa akiivunja, ila ndio hivyo tena taarifa zake nyingi na tamu zikawatia upofu.

Ila yote kwa yote, Cohen ni moja ya "mababa" wa ujasusi!!!
 
Uko vzr nimekuelewa sana mkulu
 
story nzuri sana. nilimsoma huyu jamaa kwenye kitabu MOSSAD. jamaa walikuwa noma sana. akitaka kwenda Israel anaenda kwanza ulaya, anabadili passport na wakati wa kurudi hivyohivyo. wakati wa vita ya siku sita Waisrael walielekeza nguvu zote Misri na mpaka na Syria ulikuwa almost unprotected. pengine udhaifu aliofunua jamaa uliwasaidia kuprioritise actions za kajeshi kao kadogo.
 
Back
Top Bottom