Myahudi ELI COHEN(MOSSAD)/KAMEL AMIN SABET(syrian undercover) na gharama ya kuokoa TAIFA

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
5,497
Eli_Cohen-2.jpg

Eli_Cohen-4.png


Kama kuna taifa ambalo gharama ya kulilinda ni kubwa hata gharama ya kuendesha maisha ni Hii ISRAEL ya sasa iliopo eneo lililojulikana kama Palestina (according to Roman empire). Gharama hii sio ya kifedha tu inaenda mbali hadi kuwa gharama ya UHAI.

Hebu tumuangalie Huyu mmoja Eliyahu ben Shaul Cohen na kazi iliyotukuka aliyolifanyia taifa lake wenda tukajifunza nini maana ya Uzalendo kwa vitendo.

MAISHA YA AWALI

Cohen alizaliwa Alexandria Misri na familia ya Kizayuni, Baba yake(myahudi mzalendo) akihamia mji huo akitokea ALEPPO (Wote tunajua Mji huu ambao umekuwa maarufu kwa vita thidi ya ISIS huko Syria), Pia ikumbukwe eneo lote la kuanzia Syria hadi mpaka wa syria lilijuliakana kama Syria Palestina israel ikiwa imemezwa humo. Alijaribu kujiunga na Jeshi la Misri lakini kutokana na Uyahudi wake alizuiliwa, Aliacha Chuo Baada ya Kubaguliwa vijana wa MUSLIM BROTHERHOOD akiwa Chuo kikuu na kuamua kujisomea mwenyewe nyumbani. Mwaka 1947 baada ya kuanzishwa Taifa la Wayahudi/ISRAEL wayahudi wengi wakatoka misri kurudi kwao yeye akabaki amalizie masomo yake aliyokuwa anajisomea ELECTRONICS.

HUJUMA ZA AWALI HUKOHUKO MISRI

Alibaki Misri kuendelea na movement za kichinichini japo alikuwa sio trained. Waliunda kikundi cha wayahudi waliohujumu Miundombinu ya Marekani na Uingereza ili kuichonganisha Misri na Ulaya na Marekani huku wakisaidiwa kwa siri na polisi wa Israel. Kikosi cha kijasusi cha wamisri kiliwagundua na baadhi walinyongwa lakini hakukutwa na hatia maana hakuwa mstari wa mbele.

KUKATALIWA KUJIUNGA NA MOSSAD

Alishiriki kuwatorosha wayahudi wengi kwenda kwao Israel wakiwemo wazazi wake, Baadae na yeye akarudi. Alijiunga na Jeshi Kitengo cha Kiintelijensia Israel Military Intelligence (AMAN) baadae akaomba kazi MOSSAD. Alikataliwa na kuonekana hana vigezo. Kwa hasira akaachana na jeshi na kuwa raia wa kawaida. Kumbe kwa Muda wote ameacha kazi karibu miaka miwili amekuwa akifuatiliwa kwa karibu sana na majasusi wa AMAN. Siku ikafika ikapigwa hodi nyumbani anatakiwa Kujiandaa na MISSION kama AGENT wa MOSSAD.

COHEN NI NANI NA MAANDALIZI YA MISSION AMBAYO YANGEMGHARIMU MAISHA

Huyu jamaa alikuwa mtu smart tangu utotoni. Alikuwa na uwezo karibu kila kitu. Uwezo wake mkubwa wa kutunza kumbukumbu hakukumuhitaji hata kubeba karamu na karatasi. Alianza kwa kuelekezwa jinsi ya kugundua kama mtu anamfuatilia, Alifundishwa kiarabu cha syria, akianza kuhudhuria Msikitini zaidi ya mwaka Huku akikariri mistari ya Quran ambayo Muislamu yoyote mwaminifu lazima ajue, Alifundishwa jinsi ya kutengeneza microphone, na silaha ndogondogo.

Akapewa jina la kiarabu KAMEL AMIN SABET na akaandaliwa kuwa kama mfanyabiashara mkubwa wa kisyria(Furniture). Katika silaha zake zote akili ilikuwa silaha Number Moja na ya thamani.

MISSION ILIANZIA ARGENTINA
Eli alipewa VISA kwenda kuishi argentina kama Mfanyabiashara mkubwa wa Syria kwa jina la KAMEL AMIN SABET. Argentina ilikuwa nchi yenye watu wa Syria wengi wakifanya biashara huko. Alijichanganya kwenye mahoteli na migahawa na ambapo wa syria walikuwa wakikutana kama vile LA CASA ARABE nchini humo, ni huko alipokutana na mwanasiasa AMIN AL HAFIZ akiwa katika harakati zake za kujipanga kisiasa na kuwa marafiki wakubwa.

MISSION HALISI SYRIA NA JINSI ALIVYOOKOA MAELFU YA NDUGU ZAKE HASA WALIOKUWA CHINI YA MILIMA YA GORANI.

Alifika akaishi kwenye hotel kubwa pembeni ya makao makuu ya Jeshi la Syria. Akawa anaangalia miendendo yote na kuripoti huko kwao. Akajijengea Umaarufu na watu mashuhuri hasa jeshini. Kuna kipindi alitembezwa hadi Milima ya Golan na kujua kila kitu vifaru, jinsi mambo yao yote yalivyo. Ikumbukwe kwa kipindi cha miaka 20 SYRIA walikuwa wakirusha mabomu Israel hasa maeneo ya wakulima Karibu na Golani na watu waliishi kwa wasiwasi.

Huko ndiko alipodukua mpango kabambe wa kujenga bwawa ili maji yote yanayotiririka kuelekea Israel(asilimia kubwa ni jangwa) yasifike. Bwawa hilo lilishambuliwa mapema bila kujua israel wamejuaje na mpango huo ukafa. Aliendelea kujikusanyia taarifa lukuki zilizowanufaisha Israel bila kujulikana.

KIFO NA MWISHO WAKE

Alipata nafasi ya kurudi Israel kisiri na kukutana na familia yake bila kujua kumbe ndio mara ya mwisho. AMIN AL HAFIZ alitoka Argentina akaja kugombea na Kuwa raisi wa Syria. Kwa jinsi alivyokuwa karibu na Jasusi huyu bila kujua Alifikiria kumpa UWAZIRI WA ULINZI.

Kabla haya yote hayajafanikiwa siku moja kitengo cha kijasusi cha SYRIA wakisaidiana na WARUSI walinasa SIGNAL za sauti zilizotia shaka. Kwa gari maalumu walianza kutrack hadi wakagundua zilikuwa zinatokea kwenye chumba ambacho Jasusi huyu aliishi. Siku hiyo alikuwa anaripoti vitu vingi wakamsikiliza kwa muda zaidi ya masaa manne na kuvamia wakamchukua.

Aliteswa Na kulazimishwa kutuma taarifa za uongo Israel, kwa mbinu zake aliwajulisha wenzake katikati ya mazungumzo hayuko katika mikono salama. Baadae akahukumiwa kwa kosa la Uhaini. Eli alinyongwa usiku huo katikati ya Jiji la Damascus. Asubuhi mamia ya watu walipita wakimkuta akiwa ananing'inia huku amewekewa bango lenye list ya makosa yake. Huo ndio ulikuwa mwisho wake.

MATUNDA YA KAZI YAKE KWA TAIFA
Pamoja na mambo mengi, siri nyingi alizozipata ikiwemo udhaifu wa jeshi la syria ambao Israel hawakujua. Miaka miwili baada ya kifo chake taarifa zake zilisaidia Ushindi mkubwa wa Israel wa vita vya SIKU SITA. Taifa la Israel likajichukulia Milima yote ya Golani maana COHEN alikuwa ameisema yote na maficho ya vifaru, mahandaki na silaha nzito. Hadi leo japo vitendo vya Israel haviungwi mkono na watu wengi wapenda haki, Nchi hiyo ipo salama kwa mchango wa watu wachache waliojitolea uhai wao.

quote-without-continuous-personal-development-you-are-now-all-that-you-will-ever-become-and-eli-cohen-77-84-10.jpg



Karibuni, Maana naamini watu wanajua mengi zaidi.
==========

MAELEZO YA ZIADA

Nitie neno kidogo wakuu,

Mwaka 2007 nikiwa huko kujiendeleza kielimu nilibahatika kujifunza juu ya huyu mtu na hata kaka yake aliyeitwa Moris aliwahi kufika tulipokuwa tukiendelezwa.

Cohen alikuwa mtu smart sana kichwani lakini kuna makosa fulani aliyafanya na hili pungufu lilikuwa kwenye ripoti ya pyscho-analysis aliyofanyiwa, pungufu hili lilikuwa ni kutojali mazingira hatarishi na kujiamini kupita kiasi.

Alipofika Syria alifika huko kama mfanyabiashara, lakini maisha aliyoishi yalimtia doa. Kwanza mahali alipopata nyumba ya kuishi ulikuwa ni mtaa wa watu wazito lakini ukifika kwake na kuingia ndani palikuwa hapafanani na nyumbani kwa mfanyabiashara, hili liliwapa hofu watu wake karibu na kujiuliza ni mfanyabishara gani huyu ambaye kwake pako pa kawaida? ki meza na kiti kimoja ndani, hakuna mpishi anajipikia, anafanya usafi nk.

Jambo lingine lilikuwa ni kwamba alijitambilisha kama mfanyabiashara mkubwa lakini awapo huko hakuna biashara kubwa ya maana aliyokuwa anafanya, sanasana ilikuwa ni kurusha party na kujirusha na hao Maafisa wa Jeshi ambao alifanikiwa kujipenyeza na kuwa karibu nao.

Kaka yake Moris nae alikuwa ni mtu wa Mossad aliyekuwa akipokea taarifa kutoka kwa agents mbalimbali duniani, hakujua kama mdogo wake nae alikuwa ni mtu wa system na alikuwa akipokea taarifa nyingi toka kwa mdogo wake pasipo kujua mtumaji ni ndugu yake cohen.

Siku moja akapokea ujumbe unaosema, "mmefanikiwa kupeleka kile kichwa cha cherehani nyumbani?"" Moris alipopokea ujumbe huo na kuanza kuudecode alishindwa, akaupeleka kwa mkubwa wake wa kazi, bosi wake alipouona akajua umetoka kwa Eli ambae ni mdogo wake na Moris na huku akisita kumwambia umetoka kwa mdogo wako. Ilibidi amwambie kuwa kwa level ya nafasi yako hapa huna mamlaka ya kujua maana ya ujumbe huu na ikaishia hapo.

Jioni yake Moris alienda nyumbani kwa mdogo wake kumsalimia shemeji yake mke wa Eli Cohen, aliyeitwa Nadia binti wa Kiiraki. Alipofika akakuta kichwa kipya cha cherehani akamuuliza shemeji. Shemeji akasema kimetumwa baba mdogo wako, hapo hapo Moris akaanza kuunganisha matukio, akajiuliza hivi inawezekana mdogo wangu ndie anatuma taarifa kutokea Damascus ambae ofisini alifahamika kama ""our man in Damascus", alijiuliza kisha akakaa kimya.

Mwezi Disemba, Eli alirudi nyumbani bila taarifa mke wake akashangaa sana, lakini kwa mbinu za kijasusi jamaa alifanikiwa kumweleza na akaamini hakuna shida. Ilikuwa akae wiki tatu lakini ndani ya siku tatu, usiku wa saa kumi, simu yake ikaita ya nyumbani, alipopokea akaambiwa ratiba imebadilika unatakiwa kurudi Damascus haraka, tumeshambuliwa na adui na watu wetu baadhi wameuawa, gari itakupitia ndani ya lisaa limoja tunahitaji taarifa za kina kutoka kwa adui. Eli akajibu kwa mshangao, yaani usiku huu niondoke?! akajibiwa ndio.

Mke wake Nadia alikuwa macho, Eli akaamka na kumwambia naondoka, unaenda wapi na ulisema utakaa wiki tatu mbona ni siku tatu hata hatujaenjoy unaonaondoka? Eli akajibu hii itakuwa ni safari yangu ya mwisho nikirudi sitaenda tena tutakaa wote na kulea watoto.

Jamaa akajikusanya na muda ulipofika gari ilimchukua na safari ikaanza.

Sasa wakati yuko hapo kwa mke wake kaka yake Moris alikwenda kumtembelea na alipofika alimkuta mdogo wake. Mdogo wake alijua kaka yake yaani Moris anafanya kazi shirika la posta, sasa alipofika akakuta Eli amemletea binti yake kanda mbili zilizokuwa zimeandikwa kiarabu, kichwani kwake alishatia shaka juu ya mdogo wake, akamuuliza hizi kanda mbili za mtoto umenunulia wapi? Eli akajibu akasema Ufaransa, Moris akamuuliza siku hizi Ufaransa wanatengeneza bidhaa na kuziandika kiarabu? Eli akapotezea, Moris akazidI kuunganisha matukio.

Then moris akamuomba namba ya simu anayotumia akiwa huko ugenini, Eli akataja namba ya uongo kwa kuacha namba za mwanzo mbili kisha zingine akataja, sasa kumbe Moris anazijua namba kibao za maagenti wao, akamwambia Eli umeruka namba mbili za mwanzo ambazo ni; Akamtajia na Eli akakasirika na kumuaga kaka yake kuwa anatoka kidogo kama dakika kumi.

Eli akaenda kupiga simu kwa bosi wake na kumuuliza ni nani amemwambia kaka yake juu ya kazi yake na mahali alipo, bosi akauliza kwani kuna nini, akamwambia kaka ameniomba namba nami nikaacha kutaja namba mbili lakini akaniambia nimempa namba ya uongo na kunitajia namba, bosi akamwambia tulia hakuna shida kaka yako ni mtu wetu.

Sasa aliporudi Damascus ni kweli Eli alifanya kazi ya ziada kupata taarifa, siku moja akawa amekusanya viongozi wakubwa wa jeshi akafanya party, sasa pale kwenye party Jenerali mmoja akamwambia mwingine juu ya habari za Eli, kuwa ni kijana wao na raia mzuri wa taifa lile aliyefanikiwa katika biashara, akamtaja na jina.

Baadae Eli akafika walipo wale Majenerali na mmoja akamshukuru sana Eli kwa party hiyo na akasemana leo nimechoka sana maana nilikuwa huko kwa milima ya Golan, Eli akataka kujua zaidi, akasema kwa kuuliza Golan ulikwenda kule kufanya nini? Jenerali akamwaga vitu, akaeleza kule golan kuna nini na akamwambia nitakupeleka siku moja.

Siku ikafika wakaenda kule, jamaa akajioneka mahandaki ya Jeshi la Syria yalivyo na akapata taarifa kibao.

Aliporudi usiku fasta akatuma taarifa nchini mwake akasema leo nimefika Golan, kuna mahandaki ya adui yaliyojengwa kwa ustadi mkubwa, mkitaka kushambulia alama pekee inayoonyesha yalipo ni miti iliyopandwa juu kwa mstari, pigeni hapo na mtayasambaratisha.

Sasa Eli akawa anatuma taarifa mara kwa mara kila siku na alikuwa akituma taarifa usiku wa saa mbili kika siku, sasa jeshi la Syria lilikuwa limepata vifaa vipya vya kutambua mawimbi ya taarifa, kwa hiyo kila siku usiku wakawa wanafuatilia kila mawimbi ya sauti yanapopita kwa kuzima umeme baadhi ya maeneo, mfano; leo wanazima mtaa huu na kesho ule, wakafanikiwa kujua na kupata mawimbi yale yanapotokea, wakasuka mpango wa kuvamia nyumba ile.

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo juu ya tatizo la Eli la kujiamini kupita kiasi na kutokuchukua tahadhari katika mazingira hatarishi, walivamia nyumbani kwake alfajiri na kumkuta jamaa anaendelea kutuma taarifa, alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.

Israel ikapata taarifa na wakuu wa Mossad wakatoa ujumbe mfupi ukisema, our man in Damascus has burnt! Serikal ya Israel ikafanya jitihada nyingi sana katika kuokoa maisha yake na kuachiwa mpaka wakamtumia Papa Kiongozi wa Kanisa Katoliki aingilie kati na kuiomba Syria kumwachia huyu, jitihada hazikufua dafu.

Wakuu wakafikisha taarifa kwa mke wake Eli, Nadia akalia sana na kusema ni heri mume wangu angekuwa shoe shine na akawa hapa namuona, naomba mumlete mume wangu, wakuu wa Mossad wakamjibu, tutahakikisha anarudi akiwa salama na katika kipande kimoja na si vipande vipande.

Jamaa akashitakiwa na kuhukumiwa kifo kwa kunyongwa na alinyongwa na kaburi lake mpaka leo halifahamiki mahali lilipo huko Syria, taarifa zikapelekwa nyumbani kwa mke wake Eli pamoja na ujumbe wa barua aliyoiandika Eli kwa mke wake, mke alipomuona yule jamaa akauliza mme wangu ameuawa au mzima, jamaa akamjibu pokea Eli alikuwa mtu muhimu sana na mwenye maarifa mengi.

Huo ukawa mwisho wake.

Taarifa alizotoa dakika za mwisho ndizo ziliwapa ushindi Israel katika vita yao ya siku sita.
 
Naam... jambo hili linamafunzo ya aina yake huku kwetu tunadidimizana sisi kwa sisi! heri kwa waasisi waiteteao taji ya nchi yao kiuhalali kuliko kula rushwa na kukandamiza wanyonge.
mataifa makubwa mbinu hii ishakuwa kitega uchumi chao sasa namashaka makubwa na hawa wawekezaji sidhani kama wanakuja bure hasa wakina master!
 
Eli Cohen like all other great spies, paid the ultimate price of spying...death.

Mpaka leo Mosad wanatafuta Wapi alizikwa huyu shujaa wao.
Kweli jiwe la msingi la kifo chake liko kwenye Bustani maarufu Jerusalem, "the garden of the missing solders".

Intelligence ya Syria kuepusha Israel wasifanye mission ya kuufuata mwili wake. Walimzika mara Tatu sehemu zisizofahamika. Serikali ya uturuki mwaka 2007 walijtahidi kuwapatanisha Syria na israel ili mabaki yake yarudishwe lkn haikufanikiwa 2008 ikathibitika alizikwa mahala pasipofahamika.

Kweli ukiona vyaelea vimeundwa
 
israel imekua ikisurvive kwa style hio..hata kwe ulimwengu wa leo wayahudi weng sana wamesambaa kwe nchi za kiarabu wakiish kam wakaz wazawa wa maeneo hayo lakin weng wao ni spies wanakazi ya kutuma intel nyumban...IRAN wamekuwa wakiandamwa na assassinations za nuclear scientist wao,wanajua kama kuna watu ndan ya iran wanahusika kuspy lakin hawajawah kufanikiwa kufumua huo mtandao
 
Inadaiwa kuwa mara ya mwisho akiwa gerezani huko Damascus kuwa kuna watu wa karibu waliusika na kukamatwa kwake na kunyogwa huo 1965. He was great person and said to have been an important factor in Israel's success in the Six Days War.

"I don't regret what I have done, only what I could have done and didn’t have the chance to do. Sometimes close friends fail those who can act" - Eli Cohen
 
Mada tamu sana hii.

Inaonekana mbinu ya kutumia wafanya biashara wakubwa kuwa majasusi inapendwa sana, sijui kwa nini.

Niliwahi kusoma humu jamvini pia kuwa yule mbunge wetu mfanya biashara maarufu aliyeachana na siasa uchwara ni ajenti mkubwa sana wa C.I.A

Sijajua ni kwa nini mbinu hii majasusi wanapenda sana kuitumia kupandikiza deep cover agents
 
Back
Top Bottom