Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,186
- 10,924
Miongoni mwa mataifa muhimu katika ushirika wa kuiadhibu Israel ni Syria ambayo tangu vita vianze hapo Oktoba 7 walikuwa wako kimya.
Kwa mara ya mwanzo leo wanamgambo walioko mashariki ya Israel na nyuma ya Jordan walirusha makombora machache kuelekea ndani ya Israel.
Hakuna madhara yaliyoripotiwa na jeshi la Israel japo jeshi hilo limetoa taarifa ya kufanikiwa kujua sehemu makombora hayo yaliporushiwa ndani ya Syria na kurudisha mapigo.
Hiyo inaweza kuwa ni habari mbaya kwa Israel kwani tayari ina mapambano kutokea kaskazini kutoka kwa Hizbullah na kusini kutoka kwa Houth wa Yemen na magharibi yake kutoka kwa Hamas.
Ikumbukwe kuwa Syria bado ina uchungu mkubwa na milima yake ya Golan ambayo ilitekwa na Israel wakati wa vita vya Yom Kipuri na kwamba milima hiyo pindi Syria ikianza kuidai kwa vita na kufanikiwa kuitia mkononi ni eneo ambalo linatazamana moja kwa moja na miji yote mikuu ya Israel ikiwemo Telavivi.
Wapiganaji wowote wa Syria wakiwa milima ya Golan wana uwezo wa kuchagua kituo chochote kukishambulia kwa makombora ya kawaida tu.