My Mei Mosi shoutouts... (Hutaki unaacha) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

My Mei Mosi shoutouts... (Hutaki unaacha)

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mphamvu, May 1, 2012.

 1. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Well, hello guys!
  It is Mei Mosi again, zamani zetu Rais wa Jamhuri ilikuwa ni lazima atoe hotuba kwa wafanyikazi, na matarajio yetu mara nyingi ilikuwa ni kupanda kwa viwango vya mishahara. Ikifika siku ya leo, mfanyakazi lazima uhakikishe redio yako ina betri za kutosha, na ume-tune Radio Tanzania Dar es salaam (kwani kulikuwa na stesheni nyingine?), au kama uko Dar es salaam ujue Karimjee panakuhusu. Sijui kipindi hiki hali ikoje, I mean uhusiano kati ya serikali na wafanyikazi katika siku yao hii, I don’t bother anyways!

  Yangu mie leo sio hayo, ya kuwarudisha enzi za mwalimu, wala!

  Leo nataka nitoe pongezi zangu kwa makundi ya wafanyikazi wa sekta zisizo rasmi, tena ambao ni kama wanasahaulika kila yanapotajwa makundi ya wafanyikazi wengine.

  Wa kwanza ni mama lishe, au mama ntilie, kama hujanielewa, hawa ni watu wanaotoa huduma za chakula kwa bei nafuu katika vibanda vyao wenyewe, kama maisha yako ni safi au hauishi maeneo ya mjini, au kama umeoa huwezi kujua nazungumzia nini. Ndiyo, ili uwe mteja wa hawa kina mama kuna masharti kadhaa, kipato chako kiwe kidogo, uwe hujaoa na uwe mkazi wa mijini. Hawa ndio wanalisha kundi kubwa la wafanyakazi wa kiwango cha chini ambao ndio wengi na vijana. Kundi hili linalolishwa nao ndio nguvukazi ya taifa haswa, sipati picha bila huduma ya kinamama hawa maisha yetu yangekuwaje? Kazi yao ina changamoto nyingi, kushughulika na moto muda mwingi si mchezo, lakini bado hakujawa na tija sana katika biashara zao. Kutokana na kasumba, kinamama hawa hawakopesheki na mabenki, na ikitokea ni haya mashirika ya kina Iddi Simba, tena kwa riba ya asilimia 50. Biashara yao ni challenge tosha, achilia mbali matusi wanayovurumishiwa na wateja wao. Its realy painfull. My shout outs to you kinamama!

  Kundi la pili ni vibarua wa ujenzi maarufu kama wabeba zege. Hivi umeshawahi kujitwisha mfuko wa saruji wa kg. 50? Ni mzito asikwambie mtu, sasa maisha ya vijana hawa ni zaidi ya kubeba huo mfuko, ni kazi ngumu na nzito kuwahi kutokea chini ya jua. Pamoja na dharau wanayoipata kutokana na kazi yao, achilia mbali malipo duni wanayopata (Sh.T 4000/= kwa siku), ukweli ni kwamba hili ndilo kundi muhimu kabisa katika sekta ya ujenzi, hasa miradi mikubwa. Pata picha ile mijengo yote kule Posta na kwingineko, mabarabara yote nchi nzima, uwanja mkuu wa Taifa, ni kazi ya mikono yao. But when it comes to credits, everyone turns to so called ‘wakandarasi’, ambao ndio kupitia kwao majengo yanaanguka, barabara zinaumuka na uwanja hauna viwango. Nitumie kalamu hii kuwatia moyo vibarua wote wa ujenzi, natambua mchango wenu kwa taifa hili.

  Kundi la tatu ni wafanyabiashara wadogo wadogo wa vyakula na mbogamboga. Kwa sisi wakazi wa mjini tusiofuga wala kulima walau tuta moja la matembele, hawa ndio wakombozi wetu. Unajua mtu unaweza kuchukulia poa kwa vile ukihitaji nyama unaifuata tu buchani, hujui kuwa mwenzako ameamka saa tisa ya usiku kuwahi Vingunguti, na vibaka wote njiani, bado mvua haijanyesha hapo. Wauza genge vilevile huwalazimu kuamka saa 10 alfajiri ili kuwahi Kariakoo na Buguruni ili kuwaletea ninyi makulaji yenu ya kila siku, sijawasahau pia wafanyabiashara wa samaki ambao nusu ya maisha yao ni kukabiliana na lile shombo lenye harufu mbaya. Hawa niliowataja hapo juu wana maana kwenye maisha yangu ya kila siku kuliko Afisa Kilimo aliyehitimu SUA ambaye sioni delivery yake kwangu (samahani kama nimekukwaza).

  Kundi linguine katika kumbo hii ni wafanyakazi wote wa mifumo ya takataka. Yaani kuanzia wasafisha mitaro, wazoa takataka mpaka wazibua vyoo. Hizi ni kazi za kinyaa kuwahi kutokea kwenye uso wa nchi, really shit job, lakini wameifanya kwa moyo na kwa bidii siku zote za uhai wao. Hawa wana hatari kubwa ya kupata magonjwa ya kuambukiza but no one cares, hata vijisemina vya safety and precaution jamani? Wanakaa kujilaza kwenye mahoteli makubwa mpaka wanaibiwa huko, wala hawaangalii maslahi ya hawa watu. Ushawahi kufanya kazi mahali ambapo chemba ya uchafu imezibuka, hakyanani hapakaliki mahala hapo, na kama una roho nyepesi utashinda njaa siku nzima, utakulaje chakula mbele ya kinyesi? Kuhusu wazoa taka wala sina haja ya kuwaelezea sana, nadhani wote mmeshawahi kukatiza karibu na gari la taka, and you know the msala here, zimeshawahi kupita siku kadhaa bila gari ya taka kupita mtaani kwenu? How was it look like, uhm? Naomba nitambue uwepo wenu na umuhimu wenu katika kuweka mazingira tulivu kwa ajili ya kazi, masomo, na shughuli zingine.

  Wengine ni madereva, mtaani kwetu unawaita sukas. Hapa simaanishi kila mwenye leseni.\, nope! Namaanisha watu ambao udereva ndio kula yao, kuanzia madereva taksi, madereva wa daladala, wanaosafirisha abiria mikoani na wanaosafirisha mizigo ndani na nje ya nchi. Hii ni kazi ambayo hakuna uvivu, lazima unapokuwa nyuma ya usukani uwe macho muda wote na uweke akili yako barabarani, bado kuna changamoto za vyombo kupata hitlafu barabarani bila kusahau ajali, hakuna dereva anayependa ajali wakuu, hasa kwa vile na maisha yake nayo yanahusika. Na bado kikinuka, cha kwanza ni polisi kumtia pingu dereva, bila kujua kuwa si kila ajali inasababishwa na uzembe, ndo maana wengi wanakimbiaga. Bado kitengo cha usalama barabarani hakijishughulishi na kutoa elimu kwa madereva, wao ni kuandika notifikesheni tu na kupokea rushwa. Mwishoni mwa mwaka jana kama sikosei, ndio Said Salim Bakhressa aliandaa semina kwa ajili ya madereva wa mizigo wa kampuni lake na akakaribisha madereva wengine kujifunza bure, lakini waliopewa dhamana hiyo, wala hawana habari. Changamoto zingine kwa madereva ni pamoja na kuvamiwa na majambazi kwa wanaosafiri mbali na taxi drivers. Kingine ni ugonjwa wa UKIMWI hasa kwa madereva wa mizigo masafa marefu, wakati umefika kwa mashirika ya kupambana na UKIMWI yaandae semina zaidi kwa hawa madereva, wako katika hatari kwa kweli. Mbali na yote, natambua mchango wao katika kuendeleza taifa hili, wote mmeshuhudia adha ya mgomo wa madereva na mnajua madhara ya sekta ya usafirishaji kwa uchumi wa nchi.

  Kundi la mwisho katika andiko langu hili, naomba niguse wafagizi wa barabara. Kwanza hawa mara nyingi ni kinamama wazee, sijui kwanini imekuwa hivyo? Miili yao imechoka na uwezo wa kuona umepungua kwa kiasi fulani, yet wanafanya kazi katika mazingira ya kupishana na magari, aloo? Yupo mmoja ambaye ni jirani yangu, kila baada ya siku kadhaa lazima anijie na stori ya koswakoswa za magari, what a risk? Thanks god madereva wanajitahidi wawezavyo kuwajali, na matukio ya hawa kugongwa si mengi sana. Pamoja na hatari hizo, bado maslahi ya kazi yao ni kiduchu, hardly wanalipwa Tsh. 40000/= kwa mwezi, hakuna tips, per diem wala sijui nini nini allowances, lakina maisha yanasonga. Natambua mchango wao katika kuweka mazingira ya miji yetu safi, hasa kutokana na sisi kutokuwa na ustaarabu wa utupaji taka njiani. My appreciatin to you!

  Hao ndio nilioona ni vema niwaangazie katika andiko langu kwa leo, maana sidhani hata kama wanajua kuwa leo ni sikukuu yao. Hardly they work, hardly they earn!

  Mei Mosi njema!
  Mphamvu. ​
   
 2. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  May Day juu! Juu! Juu zaidi!

  Makuli mbona sijawaona kwenye uzi wako mkuu Mphamvu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Dah, kweli nimewasahau, unajua inategemea na jinsi unavokuwa na exposure, mimi sijawahi kuingia bandarini na masokoni sio mtenbeleaji sana kwa hiyi wakanitoka kidogo.
  Samahani kwa hilo mkuu gambachovu...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sisi huku kanda ya ziwa tunao pia wavuvi. wale wanao tumia kokoro(Nyavu zinazotumika kutega samaki) na mtumbwi(tena mitumbiw sio ya engineya kasia) .Aisee kazi yao ni ngumu sana. Japo tunafurahia utamuwa samhawa jamaahuwa sometime hawalali usikuhata wiki nzima .USiku kwao ni mchana namchana ni usiku

  kuna kundi lingine tata na linazua mjadala na gumzo japo siliungimkono kutokana ugumu wa kazi zao na "demokrasia ya kizungu "inabidi tukubali kweli wamejitoa.Ni madadapoa na makaka poa. Kuna mmoja nasikia aliuwawa kwarisasi na mteja wake pale makaburini kinondoni

  Kuna mmoja nasikia aliuwawa kwarisasi na mteja wake pale makaburini kinondoni
   
 5. dazipozi

  dazipozi JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 1,143
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sure maneno mazima
   
 6. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,124
  Likes Received: 23,733
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kutukumbuka sisi wavuvi, kwani shughuli yetu kwa kweli si ndogo. Kupiga kasia wakati mwingine ukishindana na upepo ni shughuli pevu...wavuvi oyee!@ Mtazamaji.
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Yegokutigigo. Waongera
  yego mwamba na yegomasika. Hahahahahaha


  Ile shughuli si ndogo sijui kulekwenu bado watu wanatumiana mamba
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,045
  Likes Received: 6,485
  Trophy Points: 280
  Mmmh kubwa mno jamani.
   
 9. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,124
  Likes Received: 23,733
  Trophy Points: 280
  Taratibu bana, watu humu wataniogopa ujue!.
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Asante sana kwa salam za sikukuu kaka.
   
 11. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Kuhusu wavuvi, ilibaki kidogo niwagusie, ila sijui shatwain gani akanipitia, kuna mahala nilitaja wafanyabiashara wa samaki, cha ajabu nikawasahau wanaowawezesha, ukizingatia huku kwetu uvuvi bado haujahodhiwa na makampuni makubwa.
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Ni kweli, makundi ya muhimu sana haya japo husahaulika.
   
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  MphamvuNa hao wengine niliowataja .mbona umewapotezea teh teh teh.Nasikia kupitai kipato chao walianzisha pub . Moja iikuwa inaitwa kamana pub.( Hii niliiona kabisa ) na nyingine ushuzi pub . Hii ya ushuzi nadhani wangeweza kupata msaada Ubalozi wa ........

  Si ndio demokrasia atiiiiii
   
 14. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Loh?
  Hawa inakuwa vigumu kuwakumbatia kwa kuwa kazi zao sio halali, for they are not enforced by law. Kwa sasa sitakuwa nao mpaka sheria itakapoainisha vingine, sory to say that. Unajua Afrika si Ulaya wala Marikani, kwetu sisi, maisha yako ni ya familia yako, ukoo na pengine kijiji chako. Uchangudoa au ushoga wako unakuwa ni fedheha kwetu wote tunaohusika na maisha yako. Wenzetu wazungu walishajikataa kila mtu anaishi maisha yake binafsi, babako au mamako akizeeka unampeleka kituo cha kulea wazee, regardless vyenye alikulea.
  Ningekuwa na uwezo?
   
 15. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Nini kubwa Mamndenyi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo hata kile kitabu cha Fasihi Andishi cha Kuli nacho hukuwahi kukisoma mkuu Mphamvu?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #17
  May 2, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  We unajitafutia ban... Eidha kwa kujua,ama bila kujua!
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  May 2, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,546
  Likes Received: 18,203
  Trophy Points: 280
  Umewasahau ma TX!. Ma HG ambao licha ya kufanya kazi za ndani, pia huwa mayaya kutulelea watoto wetu, na wengine huwasaidia hata wa mama wenye nyumba kumhandle yule "mtoto mkumbwa"!.
   
 19. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Sikuwahi kukisoma mkuu,
  ingawa nakifahamu, mara kadhaa nimekikuta kwenye marejeo ya kazi ninazozisoma (since I deal with isimu na fasihi ya Kiswahili), lakini bado nasisitiza kuwa sijakuwa karibu na kundi hili kiasi cha kuandika kwa kina kuhusu wao, ningepiga blah blah na bashiri za uongo na kweli, kitu ambacho ni kinyume na maadili ya uandishi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Loh?
  Umegusa penyewe hasa, hawa nawafananisha na kiungo namba 6 uwanjani, wanafanya kazi kubwa sana lakini hawaonekani. Na kwa familia zetu za Kiswahili, all the credits wanapata ni masimango, makaripio na mshahara wa Sh.T 20000/=
  Kwa mtu ambae ndio ana dhamana ya kukulelea wanao, ana access na chakula unachokula, unatakiwa uwe more than fair to her, basi tu ni vile hatujui hatari ya position zao endapo zitatumiwa vibaya, God forbid.
  Kuhusu kumlea mtoto mkubwa, thats a help of its kind, you're right, Pasco.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...